Ugonjwa wa NIMONIA una tiba?

Aug 26, 2017
63
66
Wakuu poleni majukumu.

Wakuu naombeni msaada kwenye jambo hili kwa wataalumu wa magonjwa hususani kwa watoto.

Naombeni kufahamu kwamba Je NIMONIA ina tiba?

Kama tiba ipo je mtoto wa mwaka mmoja atapewa tiba gani na Dawa zipi ambazo zina uwezo wa kumuondolea ugonjwa wa NIMONIA unao msumbua?.

Na kama zipo dawa zinazotibu ugonjwa huo ni zipi

Nitashukuru sana kupata majibu kutoka kwenu wataalam.
 
Poleni sana, Huo ugonjwa unatesa sana. Kwa sasa jitahidi kufanya haya ni Masada Mkubwa.

Msimpe KARANGA au chochote chenye KARANGA.
Msimpe aina yoyote ya Dawa ya maji yenye Rangi Kama PANADOL ya MAJI.
Msimpe PIPI, BISCUITS, CHOCOLATE, TIKITI MAJI, NDIZI YA KUIVA, JUICE YA DUKANI YOYOTE na SODA PIA.
Msimpe Dagaa hata mchuzi.
Muepushe na VUMBI.
MUEPUSHE na UVUNDO, usimvalishe Nguo ambayo ina uvundo, usimuweke jirani na uvundo wa ZULIA au GODORO na VUMBI LAO.
Msimuogeshee SABUNI zenye KUNUKIA.
Nyote MSITUMIE SABUNI AU PERFUME.
Msitumie DAWA ZA MBUU ZA KUPULIZA AU ZA KUCHOMA. Ni HATARI SANA.

Hayo Machache na Allah awafanyie wepesi InshaAllah.
 
Poleni sana, Huo ugonjwa unatesa sana. Kwa sasa jitahidi kufanya haya ni Masada Mkubwa.

Msimpe KARANGA au chochote chenye KARANGA.

Msitumie DAWA ZA MBUU ZA KUPULIZA AU ZA KUCHOMA. Ni HATARI SANA.

Hayo Machache na Allah awafanyie wepesi InshaAllah.
Nashukuru sana mkuu kwa ushauri wako asante sana.
 
Mazingira anayoishi mtoto mnalinda na kutopatwa na hali ya pneumonia?

Je, mnampa vyakula kwaajiri ya kumsaidia kupambana na hiyo hali isimpete kwa kinga yake ya mwili kuwa imara?!
Tunajitahidi mkuu.

Nipe ushauri wa aina ya hivyo vyakula ambavyo tunaweza mpatia kwa ajili ya kinga mwili
 
Nanukuu: "Naombeni kufahamu kwamba Je NIMONIA ina tiba?"
Jibu ni:- Ndiyo. NIMONIA (Pneumonia) inatibika kabisa Hospitali. Cha msingi ni kujihakikishia kama kweli ni Nimonia au ni Mzio(Allergy). Rudi tena Hospitali na uwaombe wafanye vipimo au nenda maabara binafsi(Private) mtoto afanyiwe vipimo kuthibitisha kama ni kweli ana NIMONIA au ni mzio( allergy) au ni dalili za pumu(Asthma). Poleni sana - Mungu awajalie wepesi tatizo hilo lipate ufumbuzi mapema iwezekanavyo.
 
Wakuu poleni majukumu.

Wakuu naombeni msaada kwenye jambo hili kwa wataalumu wa magonjwa hususani kwa watoto.

Naombeni kufahamu kwamba Je NIMONIA ina tiba?

Kama tiba ipo je mtoto wa mwaka mmoja atapewa tiba gani na Dawa zipi ambazo zina uwezo wa kumuondolea ugonjwa wa NIMONIA unao msumbua?.

Na kama zipo dawa zinazotibu ugonjwa huo ni zipi

Nitashukuru sana kupata majibu kutoka kwenu wataalam.
Hivi ni nimonia au pneumonia (ukitamka nyumonia)

Wengune nasikiaga wanaita limonia.
 
Nanukuu: "Naombeni kufahamu kwamba Je NIMONIA ina tiba?"
Jibu ni:- Ndiyo. NIMONIA (Pneumonia) inatibika kabisa Hospitali. Cha msingi ni kujihakikishia kama kweli ni Nimonia au ni Mzio(Allergy). Rudi tena Hospitali na uwaombe wafanye vipimo au nenda maabara binafsi(Private) mtoto afanyiwe vipimo kuthibitisha kama ni kweli ana NIMONIA au ni mzio( allergy) au ni dalili za pumu(Asthma). Poleni sana - Mungu awajalie wepesi tatizo hilo lipate ufumbuzi mapema iwezekanavyo.
Nashukuru sana kwa ushauri wako mkuu wangu.
 
Nimejaribu kucheki nimeona kwa kiswahili pneumonia ndio inaitwa nimonia.
Hongera.Ni Ugonjwa wa mapafu na njia ya kupukulia complicated kidogo unaosababishwa na Bacteria pseudomonas aureginosa ,strptococcus pneumoniae n.k. lakini pia vipo vitu vingine vinavyoweza kusababisha dalili kama za pneumonia e.g. perfumes, vumbi, vyakula fulani au vinywaji ikiwa ni pamoja na aina ya mazingira n.k. n.k.
Endelea kujifunza .
 
Shukrani mkuu, je mzingira ya baridi yanaweza kumsababishia mtu huu ugonjwa?
 
Nenda hospitali ya Burhan kule posta dsm watakusaidia utapona

Kuna ndugu yangu alikua anaumwa kila hospitali wanaambiwa ni allergy hasa hizi local hospital wanatibu kimazoea sana

Nenda Burhaan au Hindu Mandal watachukua vipimo mpaka Xray then utapewa dawa utapona
 
Ila sasa inabidi usikae mazingira yenye hewa ya unyevunyevu, unapolala vaa sweta,

Karanga,pombe,soda ,juisi ,na hizi energy drink inabidi u stop kwa muda ka alivosema mdau huko juu

Pia awe ana deki chumba ,asilale karibu na dirishani usiku and on top awe anafanya mazoezi ya pumzi kingine amuombe MUNGU wake na hili nalo litapita tu
 
Shukrani mkuu, je mzingira ya baridi yanaweza kumsababishia mtu huu ugonjwa?
Sio kivile ila mazingira ya baridi yanachangia sana kuwepo kwa ugonjwa huo hususan kama hakuna tahadhari inayochukuliwa e.g. huvai nguo nzito kukinga baridi, hauli vyakula vyenye kuutia mwili joto au unajiachia kupigwa na baridi e.g. kuendesha pikipiki bila mavazi maalum n.k. na zaidi kama mwili wako tayari ni dhaifu au kuna ugonjwa mwingine unaoshambulia mwili.
 
Back
Top Bottom