Ugonjwa wa Mwakyembe: JK abebeshwa zigo!

Nitashangaa sana kama Kikwete atatoa kauli yoyote kuhusu ugonjwa wa Mwakyembe. Tusubiri.

Raisi mwenyewe naye alihusishwa katika taarifa ile ya RICHMOND; sasa hapa naye pia amehusika katika kutaka kumtoa kafara Mwakyembe. Hivi tunafikiri Raisi atasema nini.

Je anaweza kuwa jasiri na kujitaja mwenyewe kuwa amehusika??

TUSUBIRI HATA MIMI NITASHANGAA KAMA RAISI ATAPATA UJASIRI HUO


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hii tabia ya kutaka Raisi kusemea kila kitu - ni kuondoa madaraka ya watendaji wengine. Juzi juzi hapa tulitaka tamko kwa wagonjwa - posho za wabunge - leo tena afya ya mwakyembe! Du! mimi nadhani akaa chini na kufikiri na kucha na risala ndefu ya kurudisha imani kwa watanzania na kufafanua mgawanyo wa madaraka
 
Mie nasubiri taarifa ya mgomo wa madaktari nilisikia angeitoa tangu yupo mwanza sasa mbona kimya au anajua yamekwisha

kuhusu hili bado tunasubiri tarehe 03 March 2012.

Mwache ale raha tu. CCM kugawa ng'ombe wanaweza lakini kuhudumia wananchi wake hawawezi.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
He's part of this scam, directly or indirectly! My accusing fingers are pointing at EL and AR. If, and only if I could be in a position to meet these bums in secluded place, I'd had knifed them dead!!

Eti yote hii ni kutaka urais come 2015 na RA akiendelea kupora mali za umma.

Ma tz majin ga sana yaani yako mil 44 yanasumbuliwa na EL na RA yaani yako kama manyumbu yanavyofukuzwa na simba wawili. Shauri yao mimi simo
 
labda Mwakyembe ateme Uwazili ubunge ahamie Chadema tuanze ppls power tuyaondoe kwa nguvu haya magamba plus ndipo haki itapatikana.
 
Haihitaji kuwa Intelijensia kutambua wahusika wa huu mchezo mchafu aliofanyiwa Mwakyembe.
Nahisi hata anayetakiwa hapa atoe taarifa alishashiriki kwenye tafrija ya kupongezana kwa kazi nzuri ya kumuangamiza Mwakyembe.
Kama huyu anayehitajika kutoa tamko alidiriki kuwawekea kifua wezi wa EPA inakuaje mtu kwa akili nyepesi tu kushindwa kuona picha halisi ya Wahusika wa jambo hili?.Wengi wa wanaoathirika na matukio haya ndani ya CCM wanaponzwa na kutojiamini kuwa kuna maisha ndani ya Nchi hii hata kama uko nje ya mfumo wa CCM na kwamba CCM ya baada ya Nyerere si chama cha Watanzania tena.
 
Katika gazeti la Tanzani Daima la leo limeandikwa kichwa cha habari kuwa JK abebeshwa lawama kuhusu afya ya Mwakyembe.

Katika hali iliopo ni kweli JK anatakiwa kubeba lawama. Inapofikia chombo muhimu cha usalama wa raia kushindwa kufanya uchunguzi dhidi ya madai alioyatoa Mh. Dr. Mwakyembe hata kabla ya hali alionayo kumfika, hii inaonyesha Jeshi la polisi si tena lipo kwa ajiri ya raia wa kawaida na watu wanaotetea rasirimali za nchi bali lipo kwa interest la kutetea wezi/mafisadi ambao viongozi wa polisi wanafaidika nao.

Kitendo cha JK kukaa kimya na wala kutoonyesha hata kutoa maagizo kwa mteule wake Saidi Mwema kufanya uchunguzi juu ya mambo alioripoti Mwakyembe kuhusu njama za mauaji kwenye Jeshi la polisi, hii inaleta hisia kuwa KUNA SIRI NZITO CHAFU nyuma yake ambayo ina baraka zote. Haiwezekani mkuu wa dola asishituke wakati mambo yanaenda ndivyo sivyo.

Watanzani tusubiri utawala huu upite tupate utawala mwingine ambao naamini utakuwa safi mambo makubwa yatakuwa hadharani, tusubiri subira ya vuta heri.
 
Back
Top Bottom