Ugonjwa wa Mwakyembe: JK abebeshwa zigo!

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,047
RAIS Jakaya Kikwete ametakiwa kutoa kauli dhidi ya ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, baada ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda, kutoa kauli zinazopingana. Sambamba na hilo, kiongozi huyo wa nchi amebebeshwa mzigo wa Dk. Mwakyembe, kwa madai kuwa ugonjwa uliompata ni matokeo ya Serikali ya Rais Kikwetekushindwa kuwashughulikia mafisadi waliotajwa na Dk. Mwakyembe katika ripoti ya uchunguzi kuhusu sakata la zabuni ya Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Bashir Ally, alisema ukiachia suala la viongozi waandamizi kutoa kauli za kupingana, chanzo cha ugonjwa wa Dk. Mwakyembe ni serikali kushindwa kuukabili ufisadi. “Ukiweka kando suala la viongozi kutoa kauli za kujikanganya kuhusu ugonjwa wa Mwakyembe kwamba amelishwa sumu au la, lakini ukiliangalia jambo hili utabaini kuwa chanzo chake ni ufisadi, na niseme kwamba hatua hii, mafisadi wameteka dola na hii ni hatari sana kwa taifa,” amesema.

Amesisitiza kuwa mafisadi wameteka dola kwani hata waliohusika na wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), wapo mitaani wakiendelea kuishi na wale walioibua ufisadi huo, hali ambayo ni hatari. Akizungumza kwa kujiamini, Dk. Bashir amesema kama serikali ya Rais Kikwete ingetekeleza mapendekezo ya ripoti ya Dk. Mwakyembe, leo hii hofu kwamba kalishwa sumu, isingekuwepo na ugonjwa wake ungeonekana wa kawaida.

Akizungumzia suala la viongozi kutoa kauli za kujikanganya katika mambo muhimu yanayolihusu taifa, Dk. Bashir amesema hiyo ni aibu, kwani si mara ya kwanza kwa viongozi wa serikali kupishana kwenye kauli zinazohusu mambo muhimu ya taifa. Aliitaka serikali kukata mzizi wa fitina kwa kutoa kauli sahihi kuhusu ugonjwa wa Dk. Mwakyembe ili wananchi wajue ukweli. Naye Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari wanawake nchini (TAMWA), Ananilea Nkya, amesema ni aibu kwa serikali kuwa na kauli za kujikanganya kuhusu afya ya naibu waziri huyo. Amesema hali hiyo si tu kwamba ni aibu bali pia inaonyesha serikali inataka kucheza na afya ya kiongozi huyo.

“Serikali imewaweka wananchi njia panda kuhusu afya ya Dk. Mwakyembe, hawajui washike lipi, waziri mkuu anasema lake, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, naye katoa kauli tofauti na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, DCI Manumba, hapa wananchi washike lipi?” alihoji Nkya. Mkurugenzi huyo wa Tamwa alisema kwa hatua iliyofikiwa ni bora Rais Kikwete akazungumzia tukio hilo ili kurejesha imani kwa wananchi, vinginevyo watabaki njia panda, wasijue wamwamini nani.

Alisisitiza kuwa suala la ugonjwa wa kiongozi yeyote haliwezi kuwa siri kiasi cha serikali kushindwa kuzungumzia, kwani siku zote viongozi huenda kutibiwa nje kwa gharama za kodi za wananchi. Katika hatua nyingine, baadhi ya askari polisi wameelezwa kushangazwa kwao na kauli ya bosi wao, Manumba. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, huku wakiomba majina yao yahifadhiwe, askari hao walisema DCI Manumba asingezungumzia kabisa suala hilo kwani bado liko kwenye uchunguzi.

“Wiki takriban mbili zimepita tangu Waziri wa Mambo ya Ndani aliposema serikali imeamua kuchunguza sakata hili. Kwa vyovyote vile uchunguzi unaendelea, yeye taarifa kwamba uchunguzi umekamilika na Mwakyembe hajalishwa sumu ameipata wapi?” alihoji askari mmoja wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini. Juzi Manumba alikaririwa na vyombo vya habari akisema kwamba uchunguzi wa ugonjwa wa Mwakyembe umekamilika na kwamba hajalishwa sumu.

Kauli hiyo ilimuibua Dk. Mwakyembe ambaye kupitia taarifa yake alisema haamini kama taarifa aliyosoma DCI Manumba ni yake, kwani haikuwa sahihi na imejaa upotoshaji. Taarifa za Dk. Mwakyembe kulishwa sumu mara ya kwanza ziliibuliwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta. Ugonjwa huo umesababisha kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, anyonyoke nywele, kope, vinyweleo na ndevu, huku vidole vya mikono na kucha zake zikiwa nyeusi, hali inayomfanya avae ‘gloves’ muda wote.

Halikadhalika miguu ya Dk. Mwakyembe ambaye kwa sasa amerejea nchini India kwa matibabu imevimba na kupasuka na wakati mwingine hutoa damu, hali inayomsababishia maumivu makali.

Source: Tanzania Daima
 
Sumu kuhusu Mwakyembe, Slaa, Sitta na Mwandosya etc ilielezwa wazi kabisa hapa JF, aliyeleta, waliokaa kikao cha kupanga kuwapa watu sumu, anayetoa order hizo wote wamo humu JF.
 
Kama wababe wameteka dola, akitoa kauli tu yeye anakula Plnm 210. Wanyakyusa wanasema tulimbujuju
 
JK hawezi toa tamko ataishia kuwatumia watu kama Manumba on his behalf akiwa aside anaangalia mnyukano!
 
He's part of this scam, directly or indirectly! My accusing fingers are pointing at EL and AR. If, and only if I could be in a position to meet these bums in secluded place, I'd had knifed them dead!!

Eti yote hii ni kutaka urais come 2015 na RA akiendelea kupora mali za umma.
 
Mie nasubiri taarifa ya mgomo wa madaktari nilisikia angeitoa tangu yupo mwanza sasa mbona kimya au anajua yamekwisha
 
Rais kawekwa kibindoni atazungumza sa ngapi?
Jamani mizigo mingine mnayompa sio yake. Ni kama vile nchi hii haina Taasisi husika zinazoweza toa maelezo. raisi atakuwa anatoa maelezo mangapi?
Ufisadi, migomo ya Waalimu, migomo ya Waastafu EAC, Migomo ya wanafunzi na mikopo yao, madai ya waalimu, mgao wa umeme, malipo ya dowans, ubadhilifu wizara ya mali asili, ugonjwa wa mwakyemebe na wa mwandosa, utendaji mbovu Reli(TRL), msongamano Dar, wanaoishi mabondeni, malipo ya waathiriwa kwa mabomu Ukonga na Mbagala, kukatika kwa maji Dar, kufeli mitihani ya Form four etc.
Haya mengi ukiyaona yanapaswa kutolewa maelezo na Taasisi husika ambao zina watu wanalipwa mishahara na wanapaswa waajibike na raisi abaki na yale yanayohitaji maamuzi ya juu. Taasisi zipo, wizara zipo, baraza la Mawaziri lipo kama zote haziwezi kumaliza mambo hayo na kuyatolea maelezo basi tuko katika hali ngumu.
 
Nitashangaa sana kama Kikwete atatoa kauli yoyote kuhusu ugonjwa wa Mwakyembe. Tusubiri.

Hivi watu wanafikiri Kiwete anaweza akatoa kauli yoyote kuhusu ugonjwa wa Mwakyembe??? Forget!
Ule msemo wa LIKE SON LIKE DADDY una hold hapa. Usitegemee Kiwete azungumze tofauti na hao vihiyo wake aliowateua mwenyeeeewe!
 
Jamani mizigo mingine mnayompa sio yake. Ni kama vile nchi hii haina Taasisi husika zinazoweza toa maelezo. raisi atakuwa anatoa maelezo mangapi?
Ufisadi, migomo ya Waalimu, migomo ya Waastafu EAC, Migomo ya wanafunzi na mikopo yao, madai ya waalimu, mgao wa umeme, malipo ya dowans, ubadhilifu wizara ya mali asili, ugonjwa wa mwakyemebe na wa mwandosa, utendaji mbovu Reli(TRL), msongamano Dar, wanaoishi mabondeni, malipo ya waathiriwa kwa mabomu Ukonga na Mbagala, kukatika kwa maji Dar, kufeli mitihani ya Form four etc.
Haya mengi ukiyaona yanapaswa kutolewa maelezo na Taasisi husika ambao zina watu wanalipwa mishahara na wanapaswa waajibike na raisi abaki na yale yanayohitaji maamuzi ya juu. Taasisi zipo, wizara zipo, baraza la Mawaziri lipo kama zote haziwezi kumaliza mambo hayo na kuyatolea maelezo basi tuko katika hali ngumu.


Kweli huu mzigo si wake na wanaosubiri tamko watasubiri mpaka kiama. Mwakamyembe analo faili la ugonjwa wake wote ambalo kapewa na Madaktari wa Apollo India na alishirikishwa katika hatua zote za uchunguzi huko india kwani ndio utaratibu wa hospitali ya apollo. Baada ya kupata uhakika huo kuwa kapewa sumu kwa nini hachukui hatua mapema/ Akifa nani atachukua hatua? Kuchelewa kwake sasa mafisadi wanatumia fedha zao kuchakachua taarifa inayomhusu yeye. Kwani hajui kuwa Manumba DPP Feleshi na Nahodha wote wanaripoti wa Edward Lowassa kupata mgao wa mali? TAMKO ANALO MWENYEWE MWAKYEMBE NA SI WENGINE!!!!!!!
 
Kwa hili tunambebesha JK mzigo usio wake,sioni kama kuna umuhimu wa raisi kutolea kauli jambo kama hili.Nadhani wa kwanza anayepaswwa kutupa kauli ni Dr Mwakyembe mwenyewe kwa kuwataja anaosema wamemlisha sumu,halafu na Sitta anapaswa kutudhibitishia ukweli huu kwa kukandamiza kabisa ushahidi wa wazi usio na shaka.

Vinginevyo sioni kama kuna haja ya kumbebesha mkuu wa kaya hili zigo,labda kama nae akitajwa kuwa sehemu ya watu waliosuka huu mpango,hapo nadhani anapaswa kutolea kauli,maana nchi itakuwa imekosa imani nae zaidi,maana hata sasa wananchi wengi wamekosa imani na JK kwa asilimia kubwa.
 
Atatoa kauli gani wakati yeye ndo Mhusika mkuu?


Kwa hili serikali isipoangalia inaweza kuondolewa madarakani kwa nguvu ya umma kutokana na ugonjwa wa Mwakyembe, tena wanaccm watatangulia kabla ya wanaChadema na wananchi wengine. Maana mwakyembe ni mwanaccm, watuhumiwa ni wanaccm. Time will tell.

 
Jamani mizigo mingine mnayompa sio yake. Ni kama vile nchi hii haina Taasisi husika zinazoweza toa maelezo. raisi atakuwa anatoa maelezo mangapi? Ufisadi, migomo ya Waalimu, migomo ya Waastafu EAC, Migomo ya wanafunzi na mikopo yao, madai ya waalimu, mgao wa umeme, malipo ya dowans, ubadhilifu wizara ya mali asili, ugonjwa wa mwakyemebe na wa mwandosa, utendaji mbovu Reli(TRL), msongamano Dar, wanaoishi mabondeni, malipo ya waathiriwa kwa mabomu Ukonga na Mbagala, kukatika kwa maji Dar, kufeli mitihani ya Form four etc. Haya mengi ukiyaona yanapaswa kutolewa maelezo na Taasisi husika ambao zina watu wanalipwa mishahara na wanapaswa waajibike na raisi abaki na yale yanayohitaji maamuzi ya juu. Taasisi zipo, wizara zipo, baraza la Mawaziri lipo kama zote haziwezi kumaliza mambo hayo na kuyatolea maelezo basi tuko katika hali ngumu.

Usifikiri kuwa wenzako hawajafikiria kwanini wanataka JK atoe maelezo.

Kwanza, hao unaotaka watoe maelezo ni watendaji walio chini ya JK na amewateua mwenyewe. Hao wateule wake baadhi wameshindwa kutoa maelezo, hivyo yeye awawajibishe kwa kutotoa kauli au yeye mwenyewe atoe maelezo.

Pili, baadhi ya wateule wa JK wanatoa maelezo yanayopingana, hivyo yeye ndiye anayepaswa kurekebisha hayo kwa sababu mamlaka yao ya nidhamu yako kwake. Hukumbuki kuhusu nyongeza za posho za wabunge jinsi waziri mkuu, spika na katibu wa bunge walivyopingana hadi rais akatoa maelezo kuwa hajaridhia nyongeza za posho? Unafikiri Watanzania hatumjui rais wetu?

Tatu, kabla ya Dr. Mwakyembe kupatikana na hilo suala la kulishwa sumu aliwahi kutoa maelezo polisi kuwa anatafutwa ili auawe. Hilo jambo lilikuwa zito lakini polisi waliopaswa kufanyia kazi madai yake ndiyo hao wanaojikanganya, sisi tumtegemee nani tena?

Nne, huyo rais ambaye unataka kumpunguzia majukumu yuko Longido akigawa ng'ombe. Mbona hilo jukumu la kugawa mifugo hutaki kumpunguzia? au unadhani hayo ndiyo majukumu yake?

Hata ukimwonea huruma rais wako haitatusaidia kitu maana kama jukumu la uongozi wa nchi alishindwa yeye mwenyewe atuambie na wala hakuna sababu ya watu wengine kumtetea hata katika mambo yaliyo wazi.
 
View attachment 47796
Mwenyezi Mungu amsaidie Dr. Mwakyembe kwa kweli! maana kwa hali yake nina wasiwasi yanaweza kumkuta kama ya huyo jamaa hapo juu (Alexander Litvinenko (R.I.P)) kwani ile sumu ikishaanza kushambulia mwili ni hatari sana nadhani mmeona picha zake. tusifanye mchezo. Amina na mumewe wako wapi? ni bahati mbaya hatukuona picha zao wakiwa vitandani hospitalini, Wapumzike kwa amani! nakuombea Dr. Mwakyembe upone na familia yako ipate nafuu ya mashaka katika kipindi hiki kigumu!
 
Back
Top Bottom