Ugonjwa wa Marek katika ufugaji wa kuku

Ugonjwa wa Marek katika ufugaji wa kuku

Suip

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2010
Posts
1,375
Reaction score
852
Kwa wana Jf anayefahamu kama naweza kupata chanjo ya ugonjwa wa marek unaosumbua vifaranga vyangu,hili lilinitokea mwaka jana nilipoatamisha kuku zangu 12 wakanipatia vifaranga 112 baada ya wiki 2 wakaanza kulemaa vifaranga 22 na badaye ya wiki 1 vifaranga 16 kati yao walipona na 6 walikufa.Hao waliopona afya yao haikuwa nzuri walionyesha kama kaulemavu fulani na kuonyesha kama mifupa ya miguu kuvimba.
Mwaka huu nilikuwa na mpango wa kutoa vifaranga kama 200 ila nimesita kwa ajili ya huo ugonjwa nikaamua kutoa vifaranga 60 na vifanga 3 wameugua huo ugonjwa na wamepona wote na sasa vifaranga hao na umri wa miez 2 na wanaendelea vizuri japo hao waliougua naona wanatatizo kwenye miguu kama uvimbe wa mifupa.
Hivyo wataalamu wa humu JF naomba msaada kwani makala za humu ndio iliyoniwezesha kuhamasika kufuga kuku wa kienyeji kuinua pato na nigependa kama naweza kupata chanjo hiyo Arusha na naweza kuchanja mwenywe?
 

Attachments

  • IMG_20141017_105726.jpg
    IMG_20141017_105726.jpg
    249.8 KB · Views: 399
Pole mkuu mimi pia vifaranga wangu baadhi walipata hilo tatizo na sikupata chanzo ila toka hapo nimekuwa nikiwapa sana aloe vera sijaona tena hilo tatizo hata vifaranga walipoanguliwa tena na tena... Pia jua ni muhimu na mchanganyiko wenye dagaa
 
Pole mkuu mimi pia vifaranga wangu baadhi walipata hilo tatizo na sikupata chanzo ila toka hapo nimekuwa nikiwapa sana aloe vera sijaona tena hilo tatizo hata vifaranga walipoanguliwa tena na tena... Pia jua ni muhimu na mchanganyiko wenye dagaa

Nashukuru Prishaz kwa respond pia kwa upande wa chakula nawapatia chakula cha kununua Starter mash wakiwa na siku moja na kwa kadri wanavyokua nawabadilishia chakula kutokana na umri wao.Na dalili ya huo ugonjwa ni Marek kwani mguu moja unaenda nyuma na mwingine mbele, nitajaribu hiyo tiba mbadala.
 
Last edited by a moderator:
Mareks sio ugonjwa wa hatari na hauko kabisa kwenye rist ya magonjwa hatari na hata % ya vifo vyake huwa ni ndogo sana, na Mareks unashauriwa kuwachanja vifaranga endapo unatotolesha vifaranga wengi sana kuchaja vifaranga 100 au 200 mareks ni hasara kubwa sana kwa sababu chanjo yenyewe ni ghari sana na chanjo inatosha vifaranga 1000, kama unatoa vifaranga wachache haiana haja ya kuchanja, Mareks na kuna magonjwa mengi yanayo fanana na Mareks. Ila kuna Dawa ya OTC 5 sijajua kama iko Bongo hii niliambiwa ndo mbadala wa chanjo ya Mareks
 
Chasha uko sahihi sana OTC ni antibiotic nzuri mimi huwa nawapa vifaranga siku tano baada ya kutotolewa.
 
pole sana, jitahidi kuangalia usafi wa banda na kuku wakianza kuonyesha dalili ya kuugua watenge haraka ili wasiambukize wengine.
 
samahani suip kwa kuingilia uzi wako, lakini mimi pia nina tatizo, kuku wangu wameugua ugonjwa wa infectious coryza na wameathirika vibaya macho, nilikua na kuku 300 lakini nimeshapoteza 30 hadi sasa (ndani ya wiki 3 tangu ugonjwa uanze), nimejaribu kutumia dawa ta mafua fluquin na antibiotics kama oxytetracycline na CTC 20% lakini bado hazijanisaidia kuondoa tatizo hususani kwa kuku ambao wamekwishaathirika macho. naombeni ushauri nitumie dawa gani ili kupambana na tatizo hili maana linanipukutishia kuku.
 
Chasha uko sahihi sana OTC ni antibiotic nzuri mimi huwa nawapa vifaranga siku tano baada ya kutotolewa.

OTC 20% unawapatia kijiko kidogo cha chai maji Lita 5 kwa muda siku tano.
 
Back
Top Bottom