Sokomoko
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,915
- 127
Na James Magai
SERIKALI imeutangaza ugonjwa wa mafua ya ndege kuwa ni moja ya majanga ya kitaifa yanayoikabili nchi.
Hayo yalisemwa jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akizindua mpango tahadhari na udhibiti wa ugonjwa wa mafua ya ndege nchini, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
"Baada ya kutambua tishio la ugonjwa huu ni kubwa na lina athari kubwa, serikali imeamua kutangaza ugonjwa huu ni moja ya majanga ya kitaifa. Kwa maana hiyo serikali imeamua kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na ugonjwa huo," alisisitiza Pinda.
Waziri Mkuu Pinda alisema kuna uwezekano mkubwa wa ugonjwa huo kuingia nchini kwa kuwa tayari umeenea Kusini mwa nchi ya Sudan.
"Kwa vile virusi vya ungonjwa huu vinaenea kupitia ndege warukao kuna uwezekano mkubwa kabisa wa kuenea Uganda na hatimaye kuingia hapa nchini kwetu, hivyo hatuna budi kuchukua tahadhari," alisema Pinda.
Pinda alisema endapo ugonjwa huo, utaingia nchini unaweza kusababisha vifo vingi kwa kuwa watu wengi na hasa wanakula nyama ya kuku na mayai.
"Mahitaji ya mazao ya kuku yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka. Hii inatokana na walaji wengi kupendelea sana kula nyama na mayai ya kuku wa asili na wa kisasa," alisema.
Alisema Tanzania ina kuku wengi na kwamba hivi sasa inakadiriwa kuwa nchi yetu ina kuku wa asili karibu milioni 34 wanaofugwa, kuku wa kisasa wapatao milioni 20, Bata milioni 1.2, Bata Mzinga 900,000 na Kanga 400,000.
Awali, akimkaribisha Waziri Mkuu,Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli alisema kutokana na tishio la ugonjwa huo, Serikali ilipiga marufuku uingizaji wa kuku au nyama kutoka nje hasa zilizoathirika na ugonjwa huo.
Magufuli alisema ili kupamba na ugonjwa huo, serikali imejenga maabara kubwa ya kuchunguza maambukizi ya ugonjwa huo badala ya kupeleka vipimo hivyo nje ya nchi.
Hata hivyo aliwatoa wananchi hofu na aliwaeleza kuwa tahadhari kubwa zimechukuliwa na Serikali ili kukabiliana na ugonjwa huo na kwamba katika sampuli 3,000 zilizofanyiwa uchunguzi, hakuna virusi vyovyote vilivyobainika.
Source: Mwananchi