Ugonjwa wa mafua ya ndege watangazwa janga la kitaifa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa mafua ya ndege watangazwa janga la kitaifa Tanzania

Discussion in 'JF Doctor' started by Sokomoko, Apr 28, 2008.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Na James Magai

  SERIKALI imeutangaza ugonjwa wa mafua ya ndege kuwa ni moja ya majanga ya kitaifa yanayoikabili nchi.

  Hayo yalisemwa jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akizindua mpango tahadhari na udhibiti wa ugonjwa wa mafua ya ndege nchini, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

  "Baada ya kutambua tishio la ugonjwa huu ni kubwa na lina athari kubwa, serikali imeamua kutangaza ugonjwa huu ni moja ya majanga ya kitaifa. Kwa maana hiyo serikali imeamua kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na ugonjwa huo," alisisitiza Pinda.

  Waziri Mkuu Pinda alisema kuna uwezekano mkubwa wa ugonjwa huo kuingia nchini kwa kuwa tayari umeenea Kusini mwa nchi ya Sudan.

  "Kwa vile virusi vya ungonjwa huu vinaenea kupitia ndege warukao kuna uwezekano mkubwa kabisa wa kuenea Uganda na hatimaye kuingia hapa nchini kwetu, hivyo hatuna budi kuchukua tahadhari," alisema Pinda.

  Pinda alisema endapo ugonjwa huo, utaingia nchini unaweza kusababisha vifo vingi kwa kuwa watu wengi na hasa wanakula nyama ya kuku na mayai.

  "Mahitaji ya mazao ya kuku yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka. Hii inatokana na walaji wengi kupendelea sana kula nyama na mayai ya kuku wa asili na wa kisasa," alisema.

  Alisema Tanzania ina kuku wengi na kwamba hivi sasa inakadiriwa kuwa nchi yetu ina kuku wa asili karibu milioni 34 wanaofugwa, kuku wa kisasa wapatao milioni 20, Bata milioni 1.2, Bata Mzinga 900,000 na Kanga 400,000.

  Awali, akimkaribisha Waziri Mkuu,Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli alisema kutokana na tishio la ugonjwa huo, Serikali ilipiga marufuku uingizaji wa kuku au nyama kutoka nje hasa zilizoathirika na ugonjwa huo.

  Magufuli alisema ili kupamba na ugonjwa huo, serikali imejenga maabara kubwa ya kuchunguza maambukizi ya ugonjwa huo badala ya kupeleka vipimo hivyo nje ya nchi.

  Hata hivyo aliwatoa wananchi hofu na aliwaeleza kuwa tahadhari kubwa zimechukuliwa na Serikali ili kukabiliana na ugonjwa huo na kwamba katika sampuli 3,000 zilizofanyiwa uchunguzi, hakuna virusi vyovyote vilivyobainika.


  Source: Mwananchi
   
 2. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Habari za kutisha zilizopatikana sasa hivi zinasema kuwa wilaya ya Mbulu imekumbwa na ugonjwa huu kwa kasi kubwa, na sasa wamefikia 79 kutoka 53 wa wiki iliyopita.
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kaitaba... Hii ndiyo bongo, hiyo homa ipo ilisambaa sana hapa Dar two weeks ago lakini walitoa takwimo ndogo kwasababu hapakuwa na proper diagnosis kwahiyo wengi tuliponea majumbani

  Hata huko mbulu wanapiga saxaphones thanks to Haydom hospital, huo ugonjwa upo sehemu nyingi mazee

  Bongo New York Bana!!
   
 4. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kinyume chake wengi wasijefia majumbani maana hakuna data kamili.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kweli kabisa mkuu...

  Bado sana kwenye prevention na usahihi wa takwimu hapa kwetu
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Na Jackson Odoyo na Aziza Athuman

  WAKATI serikali ikijitahidi kuziba mianya mbalimbali inayoweza kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa mafua ya nguruwe nchini jumla ya wagonjwa 105 wa ugonjwa huo wamelazwa katika mikoa ya Dar es Salaam na Manyara.

  Mbali na wagonjwa hao 105 kulazwa katika mikoa hiyo pia Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Blandina Nyoni amesema tayari mgonjwa mmoja ameshafariki dunia akiwa na ugonjwa.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam juzi, a Nyoni alisema wagonjwa hao wamelazwa katika Mkoa wa Manyara Wilaya ya Mbulu na Dar es Salaam.

  Hata hivyo wakati katibu Mkuu huyo akitangaza uwepo wa ugonjwa huo nchini pia alisema kuwa mpaka hivi sasa ugonjwa huo hauna chanjo, hivyo wananchi wajitahidi kuwa wasafi muda wote ikiwa sanjari na kutambua dalili za ugonjwa.

  "Wagonjwa watano wamelazwa Dar es Salaam na 100 wamelazwa Wilaya ya Mbulu," alisema Nyoni.

  Habari kutoka Mbulu zilisema , serikali wilayani humo imezuia sherehe zozote zikiwemo za mahafali ya wanafunzi wa shule mbalimbali ili kupunguza maambukizi.

  Lakini watalaamu wa afya wameiomba serikali kuhamishia maabara wilayani humo ili iwe rahisi kupima wagonjwa wote kabla ya kuanza kuwapatia dawa.

  Mbali na taarifa ya ugonjwa huo kugundulika katika Mkoa wa Manyara, awali Serikali kupitia taarifa yake iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Septemba mwaka huu ilitaja Mkoa wa Dar es salaam na Mkoa wa Manyara, Wilaya ya Mbulu kuwa ndizo zilizobainika kuwa na wagonjwa.

  "Ugonjwa huu wa mafua ya nguruwe upo nchini katika Mikoa ya Dar es Salaam mara na Manyara na mpaka hivi sasa kuna jumla ya wagonjwa 1,038 kati yao 985 walichukuliwa vipimo na 339 wakagundulika kuwa na ugonjwa huo" alisema Nyoni na kuongeza:

  "Mbali na idadi hiyo ya wagonjwa waliogundulika kuwa na maambukizi watu 530 hawakubainika kuwa tatizo lolote".

  Nyoni alisema nao Mkoa wa Mara ulikuwa na wagonjwa 16 waliochukuliwa vipimo na waliobainika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo ni wanne.

  Kuhusu idadi ya kubwa ya wagonjwa katika Wilaya hiyo ya Mbulu alisema pengine Wilaya hiyo imekubwa na idadi kubwa ya wagonjwa kutoka na tabia ya wakazi wa Wilaya hiyo.

  "Wakazi wengi wa Mbulu ni wafugaji na wana maisha ya kuhamahama wakitafuta malisho ya mifugo yao hivyo yawezekana hiyo ni moja ya sababu ya ugonjwa huo kukumba watu wengi" alifafanua.

  Aliongeza kwa kusema kuwa "Wakazi hao pia hawana uelewa mpana juu ya ugonjwa huo hivyo serikali inajitahidi kuwaelemisha ili wapate uelewa mpana zaidi"

  Kuhusu changamoto zinazo wakabili alifafanua kuwa ,Wizara yake inakabiliwa na tatizo la kusafirisha sampuli za vipimo vya ugonjwa kutoka mikoa yote nchini hadi Dar es Salaam.


  Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=15478
   
 7. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mahujaji wanne wafa kwa homa ya mafua ya nguruwe Written by Administrator Monday,

  23 November 2009 06:52 MECCA,Saudi Arabia

  MAOFISA wa Serikali ya Saudi Arabia wamesema,mahujaji wanne wamekufa kwa homa ya mafua ya nguruwe wakati wakihudhuria ibada ya Hijja inayofanyika katika mji mtakatifu wa Mecca.

  Walisema jana kuwa waliopoteza maisha baada ya kukumbwa na ugonjwa huo ni mwanamke raia wa Morocco, wanaume wawili kutoka Sudan na India ambao umri wao unakadiliwa kuwa ni kati ya miaka 70 wakati mahujaji wanne ni binti wa miaka 17 raia wa Nigeria.

  Wizara ya Afya ya nchi hiyo ilisema kuwa kati ya waathirika hao wanne wa kigeni hakuna hata mmoja aliyekuwa amechanjwa dhidi ya virusi vya homa hiyo ya H1N1.

  Takwimu mpya za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinaonesha kuwa hadi sasa homa hiyo imekwishateketeza maisha ya watu 6,750 ulimwengu mzima.

  Shirika la Habari la Ufaransa AFP liripoti kuwa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo, marehemu wote walikuwa na matatizo kiafya, ukiwemo ugonjwa saratani na pumu.

  Lilieleza, mahujaji watatu walipoteza maisha katika mji wa Medina wakati mmoja wao alifia mjini Mecca.

  Kwa mwaka huu zaidi ya waumini milioni tatu wa madhehebu ya dini ya kiislamu kutoka kila pembe ya dunia wanahudhuria ibada hiyo takatifu licha ya maofisa wa afya kuwa na wasiwasi wa kuwa mkusanyiko huo unaweza kusababisha kusambaa virusi vinavyosambaza homa hiyo ya mafua ya nguruwe.

  Hata hivyo Serikali ya Saudia imekuwa ikijaribu kukabiliana na hali hiyo kwa kuweka kamera kwenye viwanja vya ndege na bandari pamoja na wafanyakazi wa sekta ya afya wapatao 15,000 huku ikihakikisha kunakuwepo na mamia ya vitanda vya ziada.

  Msemaji wa Wizara ya Afya, Dkt. Khaled Marghlani aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa mahujaji wengine 16 walikumbwa na homa hiyo na wengine wanne bado wamelazwa hospitalini huku hali zao zikiwa mbaya.

  Alisema kuwa mahujaji wengine 12 walipata nafuu baada ya kupewa matibabu.

  Serikali ya Saudia ilisema kuwa mahujaji wote wanatakiwa kuonesha vyeti vya chanjo kabla ya kupewa hati ya kuingia nchini humo.

  Mwezi Septemba mwaka huu Serikali ya Misri ilipiga marufuku mamia ya mahujaji wa kiislamu kusafiri kwenda Mecca kwa sababu ya kuhofia kuhusu ugonjwa huo.(AFP)

  Source:Majira

  Maoni yangu: Kutokana na msongamano ambao huwapo hapo nafikiri
  serikali zote zilitakiwa kuhakikisha kila raia awe
  amepata chanjo ya kuzuia huu ugonjwa, na kama
  serikali haina chanjo ya kutosha ni bora kuwazuia
  watu wasiende kwenye hija,kwa usalama wao.
   
 8. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Inaonekana allah alikuwa amechukia.

  Poleni wafiwa.
   
 9. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  poleni kwa misiba. laki/ni kama ni mafua ya nguruwe si itakuwa hatari hasa ukizingatia msongamano wa watu?
   
 10. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Sasa mafua ya Nguruwe kwenye hija, vipi na vipi wakuu. Kwani Waislam siku hizi wanakula Nguruwe?
   
 11. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  23 November 2009 06:52 MECCA,Saudi Arabia

  MAOFISA wa Serikali ya Saudi Arabia wamesema,mahujaji wanne wamekufa kwa homa ya mafua ya nguruwe wakati wakihudhuria ibada ya Hijja inayofanyika katika mji mtakatifu wa Mecca.

  Walisema jana kuwa waliopoteza maisha baada ya kukumbwa na ugonjwa huo ni mwanamke raia wa Morocco, wanaume wawili kutoka Sudan na India ambao umri wao unakadiliwa kuwa ni kati ya miaka 70 wakati mahujaji wanne ni binti wa miaka 17 raia wa Nigeria.

  Wizara ya Afya ya nchi hiyo ilisema kuwa kati ya waathirika hao wanne wa kigeni hakuna hata mmoja aliyekuwa amechanjwa dhidi ya virusi vya homa hiyo ya H1N1.

  Takwimu mpya za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinaonesha kuwa hadi sasa homa hiyo imekwishateketeza maisha ya watu 6,750 ulimwengu mzima.

  Shirika la Habari la Ufaransa AFP liripoti kuwa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo, marehemu wote walikuwa na matatizo kiafya, ukiwemo ugonjwa saratani na pumu.

  Lilieleza, mahujaji watatu walipoteza maisha katika mji wa Medina wakati mmoja wao alifia mjini Mecca.

  Kwa mwaka huu zaidi ya waumini milioni tatu wa madhehebu ya dini ya kiislamu kutoka kila pembe ya dunia wanahudhuria ibada hiyo takatifu licha ya maofisa wa afya kuwa na wasiwasi wa kuwa mkusanyiko huo unaweza kusababisha kusambaa virusi vinavyosambaza homa hiyo ya mafua ya nguruwe.

  Hata hivyo Serikali ya Saudia imekuwa ikijaribu kukabiliana na hali hiyo kwa kuweka kamera kwenye viwanja vya ndege na bandari pamoja na wafanyakazi wa sekta ya afya wapatao 15,000 huku ikihakikisha kunakuwepo na mamia ya vitanda vya ziada.

  Msemaji wa Wizara ya Afya, Dkt. Khaled Marghlani aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa mahujaji wengine 16 walikumbwa na homa hiyo na wengine wanne bado wamelazwa hospitalini huku hali zao zikiwa mbaya.

  Alisema kuwa mahujaji wengine 12 walipata nafuu baada ya kupewa matibabu.

  Serikali ya Saudia ilisema kuwa mahujaji wote wanatakiwa kuonesha vyeti vya chanjo kabla ya kupewa hati ya kuingia nchini humo.

  Mwezi Septemba mwaka huu Serikali ya Misri ilipiga marufuku mamia ya mahujaji wa kiislamu kusafiri kwenda Mecca kwa sababu ya kuhofia kuhusu ugonjwa huo.(AFP)

  Source:Majira
   
 12. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #12
  Nov 23, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Hii ndio dini ya allah, Sasa anawachinja kwa mafua ya nguruwe, Kaazi kweli kweli,
   
 13. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Inaonekana kuwa, allah alikwenda Safari na akasahau kuwa kuna watu wanamswalia mtume.

  Kweli huyu allah ni kashesheshe huyu, sasa anawapa ugonjwa wa mafua ya nguruwe.

  Haramu huyu allah.
   
 14. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Allah vipi tena, lol
   
 15. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #15
  Nov 24, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Inawezekana kuwa na llah naye kafa kwa mafua ya nguruwe, si unajuwa tena allah huwa na yeye anakula nguruwe kwa siri. lol
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,423
  Likes Received: 19,747
  Trophy Points: 280
  du sasa wewe unajitafutia ligi humu nadni wenyewe bado hawajaiona
   
 17. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Inaoneka wanakula, tena wale wa Umangani, kaazi kweli kweli.
   
 18. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #18
  Nov 24, 2009
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika mikusanyiko kama hii, magonjwa ya mlipuko ni ya kutegemewa...
   
 19. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hili gonjwa lilikuwepo na kila mtu alikuwa analifahamu sio gonjwa la mlipuko.
   
 20. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #20
  Nov 24, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Waanapakimbia hapa, yani ni kaazi kweli kweli allah anapo kula nguruwe, tena Macca. lol
   
Loading...