Danken Mbombo
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 651
- 339
Kila mwaka ni ugonjwa wa kipindipindu. Hatua zinazochukuliwa na wataalam wetu ni kipiga marufuku uuzaji vyakula vya mama ntilie, nyama choma na pombe za kienyeji, ndicho wanachokiamini kuwa suluhisho la kupambana na kipindupindu. Nijuavyo mimi kipindupindu kinatokana na kinyesi chenye vimelea.
Miji yetu mingi ikiwemo Dar es Salaam imetapakaa kinyesi. Ukienda Kariakoo kuna maeneo wafanyabiashara wanauza bidhaa za chakula sambamba na kinyesi kilichotapakaa. Hata katikati ya jiji la Dar baadhi ya barabara kwa muda mrefu zimefurika kinyesi. Kuna mgahawa mmoja jijini Dar ili uingie ndani lazima uruke au ukanyage kinyesi kilichotapakaa mbele ya mgahawa huo.
Haya yote yanajulikana vizuri na mamlaka husika tena kwa miaka mingi tu lakini hakuna kinachofanyika labda mpaka wafanyiwe ziara za ghafla. Kama wataalam wetu wakitaka kumaliza tatizo la kipindupindu waachane na mawazo yao mgando, wakae chini, watumie elimu yao na kutafakari njia sahihi ya kuondoa tatizo la kipindupindu.