Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa: Fahamu Chanjo, Dalili na namna ya kudhibiti

Helicobacter pylori

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
419
277
KICHAA CHA MBWA.

Kichaa cha mbwa (Rabies) ni ugonjwa unaowapata wanyama wote wanyonyeshao (Mbwa, Paka, Binadamu, Ng’ombe nk)
Ugonjwa huu unasababishwa na kirusi (Rabies Virus)
Virusi hawa wanashambulia mfumo wa fahamu.

USAMBAAJI/UENEAJI WA KICHAA CHA MBWA

IMG_4463.JPG

Ugonjwa huu Huenea kwa njia ya mate.
Mate haya yanakua na Virusi yanaweza kumfikia mnyama mwingine kwa njia ya kuuma au kumtemea mate kwenye maeneo yenye vidonda,machoni, puani, mdomoni.
Virusi Husafiri toka sehemu waliyoingilia/iliyong’atwa na kwenda mpaka kwenye Ubongo kisha huzaliana na kurudi tena kwenye tezi za Mate (Mdomoni).
Dalili hujitokeza kati ya siku 14- 80 tangu apate Maambukizi.

DALILI

IMG_4464.JPG

1. Mabadiliko ya kitabia (kuwa na hasira kali, kula vitu kama karatasi, kinyesi,fimbo, nyaya na mawe /kushambulia watu na wanyama kwa meno, kucha,pembe na kwato bila hata ya kuwachokoza, kuona vitu visivyoonekana(maruweruwe) hataki kusikia kelele)
2. Maumivu na muwasho sehemu iliyoumwa na mnyama hujitokeza (50%) Wanyama wakiwa na hasira kali sana wanaweza kuuma watu na vitu bila ya kughadhibiwa.

3. Dalili za mfumo wa upumuaji na chakula hujitokeza (kutoka mate mengi mdomoni, kuhema kwa nguvu, kushindwa kula)
4. Maumivu na muwasho sehemu iliyoumwa na mnyama hujitokeza (50%) Wanyama wakiwa na hasira kali sana wanaweza kuuma watu na vitu bila ya kughadhibiwa

5. Dalili za mfumo wa fahamu (Kupooza na kuanguka) Katika hatua hii maambukizi yamesambaa sana kwenye ubongo na virusi wameanza kuharibu. Kupooza huanza kuonekana kuanzia kwenye koo la chakula (kushindwa kumeza) na mashavu. Hali hii husababishwa kutokwa na mate mengi na machozi na kushindwa kufumba Mdomo. Mnyama huwa si mkali na hawezi kuuma.

6. Kuchanganyikiwa na kupata kizunguzungu, kupooza kunakoongezeka, hatua kwa hatua kunakopelekea kifo cha mnyama.

Lakini wanyama wengine wanaweza kufa haraka bila hata ya kuonyesha dalili halisi za ugonjwa.
Kwa kawaida mnyama hufa ndani ya siku saba tangu kuonekana kwa dalili.

UTAMBUZI WA UGONJWA
Si rahisi kutambua ugonjwa huu kwa kutumia dalili.
Dalili hizi zitasaidia kuhisi kuwa mnyama anaweza kuwa na ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
Utambuzi kamili unafanyika kwenye
maabara kwa kupeleka kichwa (ubongo) wa mnyama aliyehisiwa kuwa na ugonjwa.

JINSI YA KUKABILIANA/KUDHIBITI
1. Kutoa taarifa ya mnyama anayehisiwa kuwa na ugonjwa wa kichaa cha umbwa kwa Daktari au Afisa Mifugo aliyeko karibu nawe.
2. Kumfungia mnyama mwenye kuhisiwa kua na ugonjwa wa kichaa cha mbwa ili asiweze kudhuru wanyama na binadamu.
3. Kuzuia wanyama katika eneo lililo na mnyama mwenye ugonjwa kwa kuweka karantini ili ugonjwa usisambae.
4. Kuchanja mbwa na Paka wote kwa wakati mmoja na kuendelea kuchanja mbwa na Paka wote watakaozaliwa.
5. Kudhibiti mbwa na Paka wanaotangatanga (mbwa wasitembee ovyo) na kuangamiza mbwa wote ambao hawajachanjwa.
6. Kutoa elimu ya kukabiliana na ugonjwa huu kwa Raia, wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari na Umuhimu wa kutunza Wanyama vyema.

CHANJO
Chanjo ya kichaa cha Mbwa hutolewa kwa Mbwa na paka kuanzia wiki ya 12 na kisha kuridiwa kila mwaka ama kulingana na Sheria za nchi husika katika namna ya kukabiliana na Ugonjwa huu.

Mambo ya kuzingatia.
1. Usichanje Mbwa au Paka Mwenye kuonyesha dalili zozote za Ugonjwa Wowote.
2. Hakikisha Umepewa cheti cha kudhibitisha Mbwa au Paka wako amepewa chanjo.
3. Kwenye hiko cheti Tarehe ya kuchanja na kurudia chanjo lazima vionyeshwe.
4. Kuwepo na kibandiko (stika) ya Chanjo husika.
5. Muhuri au sahihi na Jina la Mganga/Daktari au Afisa mifugo aliyetoa chanjo hiyo.

IMG_4465.JPG
(Mfano wa cheti cha kudhibitisha Mbwa amechanjwa)​

Kwa kubofya kiunganishi hiki utaweza kuona athari za ugonjwa kwa mbwa.


TAMBUA KWAMBA NI TAKWA LA KISHERIA KUCHANJA MBWA NA PAKA DHIDI YA KICHAA CHA MBWA.

TUTAENDELEA SEHEMU YA PILI YA UGONJWA HUU KWA BINADAMU (
KICHAA CHA MBWA KWA BINADAMU, Fahamu Chanzo, Uenezaji, Kinga na Matibabu - JamiiForums)

Pitia na hii pia.
Fahamu Minyoo hatarishi kwa Afya ya Binadamu toka kwa wanyama.
https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/Fahamu-Minyoo-hatarishi-kwa-Afya-ya-Binadamu-toka-kwa-wanyama..1565632/

NB: Kama Hukumbuki au Hujawapatia chanjo Mbwa au Paka wako basi wasiliana nasi
Sipy Vet centre. (Kwa Ushauri, Chanjo na Matibabu)
Kanyama, Kisesa MWANZA,
+255 625 753 791
odhisjamach89@gmail.com
 
Je ugonjwa huu umetapakaa kiasi gani Tanzania au maambukizi yake yako Juu.wastani au chini.

Sent using Jamii Forums mobile app

Aksante.
Ugonjwa huu kwa Tanzania Umesharipotiwa karibia mikoa yote, na Waathirika wakuu huwa ni watoto walioko chini ya miaka 15, maana wao ndio watunzaji hodari wa Mbwa.

Kwa hapa Tanzania, ugonjwa wa kichaa cha mbwa uliripotiwa kwa maara ya kwanza mnamo 1932/33. Baada ya hapo, wagonjwa wameendelea kuripotiwa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kwa viwango tofauti.
Mfano Kwa mwaka 2017 kati ya mwezi Januari hadi Agosti, watu 17,326 wametolewa taarifa ya kuumwa na mbwa au wanyama wa jamii hiyo na kumetokea vifo 8.
Takwimu hizi hazijumuishi vifo vinavyotokea nyumbani na waathirika ambao hawakufika katika vituo vya kutolea huduma za afya, hivyo tatizo hili ni linaweza pia kubwa kuliko tunavyofikiri. Utafiti uliofanyika mwaka 2002 ulibainisha kuwepo na uwezekano wa kuwepo takriban vifo 1,499 kwa mwaka nchini kutokana na ugonjwa huu.

Chanzo Ummi Mwalimu, Hotuba ya siku ya kichaa cha mbwa Sept 27, 2017
 
Kwema wana jamvi, mi natafuta mbwa German sherpherd niko mwanza mwenye nao tuwasiliane kwa 0715927151
 
Back
Top Bottom