Ugonjwa Mpya wa Slaughtersiskwasis

Ugonjwa Mpya wa Slaughtersiskwasis

Ugonjwa huu umeibukia mkoa wa Mara hasa eneo la Tarime ambapo virusi vya Slaughtersiskwasis vimesababisha watu kulewa kwa uchungu na hasira kiasi cha kujisikia hakuna ahueni isipokuwa kufanya Genocide.

Maeneo yenye uwezekano mkubwa wa kuathirika na maambukizi haya ni Mkoa wa Kagera, Mkoa wa Mwanza, Mkoa wa Arusha, Mkoa wa Manyara na Tanzania Visiwani. Historia imeonyesha kuwa watu wa mikoa hii hata mashuleni, vyuoni na makazini huwa ni watu wenye aina tofauti sana ya namna ya kutatua matatizo pindi uongozi husika unapoonekana kutojali kero zilizopo.

Leo hii ugonjwa huu mpya umeibuka Tanzania ambao kama Serikali haitakuwa makini kuutafutia tiba kwa haraka na kukinga maeneo mengine yasiambukizwe basi itafika mahala utaenea nchi nzima na matokeo yake Taifa hili litazagaa rundo la miili ya wanadamu iliyokosa mzikaji maana wote hawako, wote wamekufa, hata wawili wa mwisho waliobaki kama enzi za Nuhu na safina wameuana.

Imeanzia kwenye uchunaji ngozi, mauaji ya albino, mauaji ya vikongwe, uchomaji moto vibaka watuhumiwa, hizi zote ni dalili tu. Sasa hili la ukoo mmoja kuufuta ukoo mwingine ndiyo ugonjwa wenyewe sasa umeanza kazi.

Kuna uwezekano ugonjwa huu ukazaa ugonjwa wa Chinjamafisadilosis. Hii ni dalili kwamba sasa watanzania wameanza kuchukua Hatua mikononi.

Tufanye nini ili nchi yetu isije kushindwa kuuzuia ugonjwa huu hatari na kujikuta tunamaliza Malaria na Ukimwi laini tunamalizwa na Slaughtersiskwasis.

Wakurya na wengine wa kanda ya ziwa pamoja na wenzetu wa visiwani hasa Pemba jamani huu ndio utamaduni? Somalia haikuanza hivi?

Tamaa ikichukua mimba uzaa dhambi. Dhambi nayo ikiisha kukomaa huzaa mauti.
 
Slaughtersiskwasis ? every body is so sick except me?Let us see hata europe waliondokana na black death... nothing personal just a joke and by the way are you not one among of them? just kidding! ha ha ha
Lukwangule
 
Back
Top Bottom