buswelu moja
JF-Expert Member
- Aug 24, 2014
- 226
- 147
Ugomvi, chuki na uhasama baina ya mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na mkurugenzi wa jiji la Arusha, Dkt Madeni unazidi kuchukua sura mpya baada ya Gambo kumwambia kwamba usemaji wake una mipaka na kumwonya awe makini.
Wawili Hawa wana Hali ya kutoelewana huku chanzo kikidaiwa ni kugombea mradi wa ujenzi wa kituo kikuu Cha mabasi ya mikoani jijini Arusha.
Wakati mkuu wa mkoa na timu yake wakipendekeza ujenzi huo ufanyike mahali pengine mkurugenzi naye ameibuka akitaka mradi huo ufanyike sehemu nyingine.
Lakini pia inadaiwa mkurugenzi amekuwa akipingana na maagizo ya Rc Gambo kwa madai kwamba yeye anaripoti moja kwa moja kwa mkuu wa nchi hususani kufuatia nafasi yake akitajwa kwamba ni ofisa mwandamizi wa idara ya usalama wa taifa (TISS).
Katika madai hayo Rc Gambo anahisi Mkurugenzi amekuwa akipenyeza taarifa mbalimbali kwa mkuu wa nchi ili kumharibia kitumbua chake.
Lakini ugomvi huu unazidi kuchukua sura mpya baada ya DC wa Arusha, Gabriel Daqaro kumtabiria Mkurugenzi wa jiji kwamba huenda siku moja akawa mkuu wa mkoa wa Arusha na alitabiri hivi Karibuni alipokuwa akihutubia mkutano wa walimu wa shule za msingi na sekondari wilaya Arusha.
Itakumbukwa ya kwamba Daqaro ni afisa usalama wa taifa na aliwahi kuwa mlinzi wa Rais Magufuli kabla ya kupewa cheo cha ukuu wa wilaya.
Sinema ni ndefu macho na masikio ni yetu tutaendelea kuwajuza.