Kupata ninachozungumzia tafadhali angalia mpaka mwisho. ....
Tulishasema huko nyuma kwamba njia rahisi sana ya kuteka mawazo ya watu ni kuteka watoto kuanzia shuleni. Na njia rahisi zaidi kufanya hivyo ni kwa kupitia vitabu vyenye kulenga huko. Kama unataka watu wa nchi kufikiria London au Nairobi, au New York kabla ya kufikiria namtumbo na matatizo yake, basi njia ni hiyo. Huyo anyegawa hivyo vitabu hapo ni Mkenya bila shaka. Huko nyuma tulishaona wengineo, akiwemo mke wa balozi wa nchi moja ya ulaya akigawa vitabu kwa watoto, nafikiri ilikuwa magomeni au rutihinda.
Hili la kugawa vitabu ni mkakati wa kutufilisisha kama nchi. Inazaa watu wasio wazalendo. Kwa hiyo naiomba mamlaka husika isiwe inaruhusu watu kuja kugawa vitabu wanavyokuja navyo ambavyo hata havimo kwenye syllabus!
TUSIKUBALI! Kama wanagawa vitabu wagawe hivyo ambavyo vimeidhinishwa na Serikali!