Uganga wa jadi ni tiba au ushirikina?

Kwekitui

JF-Expert Member
Oct 29, 2017
1,070
1,078
HIVI karibuni, serikali imeendesha na inaendeleza, zoezi la kupiga marufuku waganga wa tiba za jadi na “watabiri” wapigao ramli kwa kutumia zana mbalimbali za jadi, kwa madai ya kuchochea imani za kishirikina na kusababisha mauaji ya “albino” na vikongwe nchini.
Zoezi hili limekuja wakati huduma za tiba za kisasa kwa wananchi nchini zimefifia, kufuatia serikali kujitoa kuchangia huduma za jamii na hivyo kufanya watu wengi wakimbilie tiba mbadala za jadi kwa kutoweza kumudu gharama za tiba za kisasa.

Hapa ndipo soko la waganga wa jadi linapobubujika na kufura wateja; hapo ndipo wataalamu hao wa sayansi ya kale/jadi wanapoibuka na zana zao za kazi; shughuli ambayo kwa “ujinga” wetu na kwa kubeza jadi na utamaduni asilia, tumeipa jina baya: “Uchawi”, kwa kuyumbishwa na Sheria ya Kikoloni ya “Uchawi” – The Witchcraft Act, Cap. 18 [kama ilivyorekebishwa mwaka 2002], ambayo kabla ya hapo ilijulikana kama “The Witchcraft Ordinance”, 1928.

Chini ya Sheria hii [kifungu cha 2] “Uchawi” – au “Witchcraft” kwa Kiingereza, umetafsiriwa kumaanisha na kujumuisha Ulozi [sorcery], mazingaombwe [enchantment] kuloga [bewitching], kuzingua na kutegua; matumizi ya vifaa vya uchawi, matumizi ya nguvu za kufumba jambo [occult] na kumiliki elimu ya kufumba mambo/usiri au usihiri [occult knowledge].

Vifaa au zana za uchawi vimetajwa kujumuisha, kitu chochote ambacho kwa kawaida kinatumika au kuwakilisha au kuaminika kuwa na nguvu ya kuzuia, kuchelewesha mtu kutenda tendo lolote analotaka kufanya kisheria, au kulazimisha mtu yeyote kutenda tendo ambalo kisheria hapashwi kutenda.

Pia, kugundua tuhuma ya kijinai iliyofichika dhidi ya mtu, au kusababisha kifo, kujeruhi au kusababisha ugonjwa kwa mtu au kuharibu mali, au kumuogofya mtu; au kwa kutumia nguvu za juu za asili zilizofichika kuzalisha dhana ya kiasili, na ni pamoja na dawa zinazotumika kwa madhumuni hayo.

Kama, kwa tafsiri chini ya Sheria ya Uchawi, ni kosa la jinai kwa mtu, kutumia “wachawi” kumwogofya mtu kwa kutabiri au kumtabiria kifo, kama vile wagombea nafasi za kisiasa; au adhabu ya moto wa milele ahera baada ya kifo; au uzima wa milele kwa “fumbo la imani”, basi, vivyo hivyo, wahubiri wa “dini” za mapokeo wanaohubiri hivyo kwa misahafu nao ni wachawi, na misahafu wanayotumia kuwasilisha hayo ni zana za “uchawi”.
Kama hivyo sivyo, basi, waganga wa jadi wanaotabiri matukio, au kuagua kwa njia ya ramli si wachawi; na zana watumiazo si za kichawi, kama tutakavyoona katika makala haya.

Kwa sababu hii, kitendo chochote cha kupiga marufuku kila kitu kilicho cha jadi kinachotumiwa na wenyeji bila kudadisi kisosholojia mantiki nyuma yake, ni kuudhalilisha na kuukana Uafrika, mila, jadi na sayansi asilia ya Mwafrika kwa kutukuza vya kigeni.
Tamaduni, dini na mila za Kiafrika zimejikita kwenye zana na vitendea kazi mbalimbali vya imani [kama vilivyo vitendea kazi vya dini za mapokeo], kama vile uaguzi, ubashiri na utabiri [divination], tafsiri za ndoto, ishara [omens] na nguvu [cult] ya mizimu [spirits].
Waafrika wanaamini, kwa haki yao, juu ya nguvu ya mababu [ancestors] kama kiungo na suluhisho kati ya walio hai na Mungu. Imani hiyo na ibada zake hufanyika kupitia viwakilishi [mediums] kama vile tambiko kwa kutumia vifaa vya kidunia na matoleo [offerings] kama yalivyo matoleo mengine tu kwa dini za mapokeo.

Ugomvi uliopo ni kwa dini za mapokeo kutotambua Miungu wa dini za jadi, kuashiria ubeberu wa kiutamaduni [cultural imperialism] wa mwenye nguvu dhidi ya Mungu wa tamaduni zingine.

Ndiyo maana, Afrika hadi leo, haijaweza kutoa Watakatifu kwa misingi ya mila na tamaduni zake, ila kwa misingi na vigezo vya utamaduni wa Ulaya, kwa maana kwamba hakuna cha kutamani walichoacha mababu na hivyo wako “Jehanamu”.

Waafrika watetezi wa dini za jadi wameendelea kuuliza, “Utaabudu vipi Mungu asiyejua lugha yako?; Mungu asiyejua mizizi yako, maadili na matakwa ya mababu zako?”.
Na hii ni historia kujirudia, ya Wanaisraeli walipopelekwa utumwani Babiloni, walikokataa kuabudu Miungu ya nchi hiyo wakihoji, “Tutaimbaje Wimbo wa Bwana [Mungu wa Israeli] katika nchi ya ugenini?” Nasi tunauliza, kwa nini Mwafrika anapouliza swali hilo hilo la Waisraeli aitwe “Mchawi” na kutungiwa Sheria za kigeni?.

“Jukumu la kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini”, yasema Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya1997, ibara ya 19 (2), “litakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu binafsi….”.Kwa mantiki hiyo, kama dini ni jambo huru la mtu au vikundi vya kijamii, basi, Serikali haiwezi kuwachagulia watu jinsi na namna ya kuabudu wala zana za kuabudia, mradi tu hawavunji Sheria inayokubaliwa na wengi.

Kama wengine wanadai kuundiwa Mahakama za dini zao kwa gharama za Serikali na kusikilizwa; kwa nini hawa wa “dini” za jadi nao wasipewe fursa sawa kama hiyo, badala ya kutiwa rumande na kufungiwa “ibada” kila mara?.

Katika kutenda kazi, Mganga wa jadi huvalia mavazi aina mbalimbali, mengine ya kuogofya kwa muonekano. Haya yanaweza kuwa ngozi ya mnyama, shanga, “mgwisho”, manyoya ya ndege, bangili na mengineyo yanayoelezea mazingira yanayomzunguka mwanasayansi huyo.

Mavazi haya yana madhumuni mawili: kwanza, ni kutia imani ya mteja kwa Mganga huyo; na pili ni kumpandisha hadhi kwa kujitofautisha na watu wa kawaida na jamii yake. Hili ni suala la mavazi tu kwa kila shughuli, kama ilivyo kwa Jaji wa Mahakama, Meya na Madiwani, Daktari na wengine wenye kujikweza kwa muonekano kwa mavazi wakiwa kazini.

Lakini pamoja na hayo, hili haliondoi uwezekano na kuwapo Waganga wa jadi matapeli kama ilivyo kwa fani zingine, lakini isiwe samaki mmoja akioza, wote wachukuliwe wameoza.

Inafahamika kwa jamii na Wataalam wa Sosholojia pia kuwa, kutambua au kutibu ugonjwa na kuchawiwa [uganguzi] sio sawa na kutenda Uchawi; na pia Waganguzi hao wanatambuliwa na kulindwa na kifungu cha 37 cha Sheria, Sura [Cap] 409 kinachosema: “Hakuna kinachokataza au kuzuia katika Sheria hii matumizi halali ya mifumo ya kutambua magonjwa kwa njia za jadi na watu wanaotambuliwa na jamii waliyomo kuwa na ujuzi wa kutibu kwa njia za jadi”.

Na hili lilikwishakemewa na Mahakama katika Kesi ya Thomas Bangili na Samike Maduhu dhidi ya Jamhuri [1969] HCD 246; kwamba uganga na uganguzi wa jadi na vifaa vinavyotumiwa na waganga wa jadi, si uchawi wala ushirikina.

Katika kesi hiyo, washitakiwa hao wawili walituhumiwa na kuhukumiwa kifungo kwa kujifanya kuwa na nguvu za kichawi kinyume na kifungu 3 (3) na 5 (2) cha Sheria ya Uchawi. Tuhuma ya pili ilikuwa ni kukutwa na kibuyu cha kuagulia kinachoongea; na ya tatu, kutoa kwa matumizi kifaa cha kichawi, yaani kibuyu kinachoongea.

Wawili hao walikuwa ni waganga wa jadi waliotambua ugonjwa wa mteja kwa kutumia “mizimu” na kibuyu kinachoongea kuweza kutibu kwa dawa, na pia kuwaondolea madhara ya kutokana na kulogwa.

Akiwaachia huru, Kimicha, Jaji [alivyokuwa wakati huo], alikuwa na haya ya kusema: “…. Ni jambo linalofahamika kwamba, jamii yetu kwa miaka mingi imenufaika na utaalamu na huduma zitolewazo na waganga wa jadi waadilifu, kwa kutibu magonjwa mbalimbali katika jamii yetu….. Matabibu wa kisasa, wao wana vifaa vya kisasa vya kubaini ugonjwa, kama vile X-ray, kabla ya kutoa dawa kwa mgonjwa; lakini waganga wetu wa jadi hawana X-ray wala maabara; na kwa kutambua mapungufu hayo, hutumia mbinu za jadi zinazoweza kuitwa unajimu [fortune telling], au kile kinachoweza kuitwa “akili ya sita” [sixth sense], au mizimu [spirits] kwa kijadi kwa mafanikio na kwa sifa kubwa…..”.

Akaongeza kusema: “Sheria ya Uchawi haikutungwa kuzuia au kukataza wale wanaotambua au kutibu watu magonjwa au waliologwa kichawi. Wala kutambua au kutibu mtu aliyelogwa si sawa na kuendesha uchawi; vivyo hivyo, zana anazotumia mganga wa jadi katika kutekeleza shughuli zake, si zana za Uchawi”.

Kwa mtazamo huo wa Mahakama, ni vigumu [na si sahihi tena] kwa vyombo vya dola kuthibitisha kisheria “vitendo na vifaa vya Kichawi” kwa kuangalia zana zitumiwazo na waganga wa jadi katika kuagua,kuganga na kugangua.

Ilikuwa rahisi hapo kale, wakati wa ukoloni mkongwe, Sheria ya “Uchawi” ikitungwa; ambapo dini na ngoma za jadi zilibezwa na kudharauliwa na wakoloni na kupewa jina baya – “Wapagani, wasiostaarabika, washamba, washenzi [uncultured] waabudu mizimu na shetani”; kwa sababu tu ya kutomtambua Mungu wa utamaduni wa kigeni.

Katika kipindi hicho, uponyaji wa jadi ulihesabiwa kama kitendo cha kichawi na ushirikina, tofauti na kipindi hiki cha “mwanga” ambapo mambo yamebadilika, kwa sayansi ya jadi kupewa kiti katika jamii.

Vivyo hivyo, baadhi ya madhehebu ya dini yameruhusu Mwafrika kumwabudu Mungu katika mazingira yake kwa njia ya “kutamadunisha liturujia” kumfanya muumini afurahie “ukombozi” katika mazingira yake, badala ya kumlazimisha kuabudu kwa mazingira ya kigeni, kama walivyolalama wana wa Israeli utumwani Babylon.

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu haujatenguliwa na Mahakama yoyote ya juu, na hivyo umekuwa Sheria, kwa sababu Uamuzi wa Mahakama Kuu na za juu yake kuhusu utata wa kisheria [precedents] kwa jambo la kisheria, unabatilisha utata unaobishaniwa kuweza kusababisha marekebisho ya Sheria husika.

sKwa hiyo, kitendo cha dola kukurupuka kufungia baadhi ya waganga wa jadi bila udadisi wa kina na bila kuzingatia matakwa ya sheria, ni batili.

Lakini pamoja na juhudi za kufungia madaktari hao wa jadi, ni yupi kati ya wanasiasa na Watendaji Wakuu Serikalini, asiyetembelea Sangoma huko Bagamoyo, Sumbawanga, Tanga na Pemba ili “kuangalia njia” na kwa tiba za magonjwa yaliyoshinda madaktari wa kisasa na zama zao?

Mbona Kijiji cha Samunge, miaka michache iliyopita, kilifurika “wateja”, wakubwa kwa wadogo, wasomi kwa wasiosoma, wakipenya kwa misuli, kuonja kikombe cha Babu aliyeoteshwa tiba hiyo?.

Huko Unguja na Pemba, kati ya mwaka 1940 – 50, jina la Bi Kirembwe wa Giningi, lilikuwa maarufu kwa mambo ya utabiri sahihi, ukiwamo ule juu ya Mapinduzi ya umwagaji damu Zanzibar, ya Januari 12, 1964, miaka mitano kabla ya kutokea. Waasisi wa Mapinduzi hayo walifanya tambiko mara nyingi pale Dunga kuhakikisha Mapinduzi yanafanikiwa.
Uchawi, kwa mtazamo wa Sheria ya Uchawi tuliyoinukuu hapo juu, unajumuisha pia usomaji nyota. Kama hivyo ndivyo, vitabu kama vile “Shamsa-al-Ma’araf” na “Mamba’a Usual al Hikmah” vya Ali-al-Buni; “Sa’at al Khabar” cha Abu Ma’ashar al-Falaki, “Khazinat al-Asraar al kubra” cha Muhammad Afandi an-Nazil; “Muyarrabat” cha ad-Dayrabi na “al-Jawahir al-Lama’a” cha Ali-al-Marzuki, vinavyotumika katika unajimu, basi navyo ni zana za uchawi, kama zilivyo tu zana zingine wanazotumia waganga wa jadi kwa shughuli zao.
Kama hivyo ndivyo pia, kwa nini waandamwe Waganga wa Jadi pekee; na Wanajimu wa mjini kuachwa kufurahia “ushirikina” wao? Kama huu hauwezi kuitwa ubaguzi chini ya ubeberu wa kiutamaduni, basi jambo hili tuliite kwa jina gani?s

Hebu angalia wakubwa nao wanavyojitegemeza kwa sayansi ya jadi bila kuhojiwa: Aliyekuwa Rais wa Sudan, Jaffar Nimeiry, alijishirikisha sana na uchawi wa kikundi cha “Sufi” ili kubakia madarakani asipinduliwe. Mgangas wake aliogopwa Sudan nzima.
Rais wa Zaire [sasa DRC] wa zamani, Mobutu Seseseko, inadaiwa alidumu madarakani kwa “nguvu za giza” kwa uchawi uliokuwamo kwenye fimbo yake [mkongojo] ambao hakuachana nayo, akiamini kwamba kila alipoinua fimbo hiyo, kila jambo lilimnyookea.
Inaelezwa pia, hayati Jomo Kenyatta, Rais wa kwanza wa Kenya, nguvu zake za kisiasa zilikuwa kwenye “mgwisho” [fly-whisk], kama zilivyokuwa nguvu za Mfalme Haile Selasie wa Ethiopia, kwenye pete aliyovaa daima.

Kenyatta na wapiganaji wenzake wa vita ya “Mau Mau”, kama Dedan Kimathi na wengine, waliwachachafya wazungu vitani kwa ndoto za “mizimu” zilizowawezesha kuelewa matukio yote vitani.

Inaelezwa, alijua siku ya kufa kwake, akaamua kufia Nakuru mwaka 1978, badala ya Nairobi ili kuepusha ghasia za kuwania urithi miongoni mwa wanasiasa wa nchi hiyo.
Awali, Kenyatta alijulikana kwa jina la kigeni la Johnstone Kamau, lakini baada ya kurejea kwenye “mizizi” na maisha ya utamaduni asilia, alibadili jina na kuitwa Jomo Kenyatta, na inadaiwa alinusurika kifo na majanga mara nyingi kutokana na mzimu wa mababu ujulikanao “Mundi Mugo” ambao ndio uliompa “mgwisho” na pete ya kinga yenye nguvu.
Naye aliyekuwa Rais katili wa Guinea ya Ikweta, Marcia’s Nguema, inadaiwa alidumu madarakani kwa ukatili mkubwa wa kuuwa raia hovyo, akihofiwa kutumia nguvu za giza. Na alipopinduliwa, Septemba 1979 na kuhukumiwa kifo kwa kupigwa risasi, kazi hiyo ilibidi ifanywe na wanajeshi kutoka Morocco, baada ya askari wa Guinea ya Ikweta kuufyata wakihofu kwamba mzimu wake ungewarudia katika umbo la chui.

Je, wanaoponya kwa maombi na miujiza kwa njia ya “dini”, wana tofauti gani na wanaofanya hivyo kwa mila na jadi za Kiafrika? Kwa nini nao wasiandamwe?.
Lini tutaacha tabia na utamaduni wa kupokea pekee na kumeza kila kitu [kutoka nje]mithili ya dodoki; ili badala yake nasi tuweze kutoa utamaduni wetu asilia kwa jamii ya kimataifa?. Lini tutapata akili ya kukataa kuporwa “roho” na rasilimali chini ya ubeberu wa kimataifa? Tutafakari.
FB_IMG_1533482745965.jpg
 
Sikumbuki mara ya mwisho kushindwa kumaliza kusoma thread ni lini ila hatimae leo nimeashindwa kumaliza kusoma huu uzi, acha niwe mpenzi msikilizaji tu.
 
ndefu sana inachosha kusoma, andika fupi mkuu but reality is that, uganga wa jadi ni uchawi na no tiba hasa kwa kuzingatia imani ya mtu.
 
Lini tutaacha tabia na utamaduni wa kupokea pekee na kumeza kila kitu [kutoka nje]mithili ya dodoki; ili badala yake nasi tuweze kutoa utamaduni wetu asilia kwa jamii ya kimataifa?. Lini tutapata akili ya kukataa kuporwa “roho” na rasilimali chini ya ubeberu wa kimataifa? Tutafakari.View attachment 827712
Ushuhuda wa Tukio la ushirikina mjin Kigoma.

Habar zenu Wadau
Juzi shoga yangu alifukuzwa kazi hapa tukaelekezwa na rafiki yangu kwa mzee Kingwele anaishi Mpakan na Congo.

Tulipatiwa huduma pale siku nne tuu.
Siku ya pili na ya tatu tulivyokwenda nikashuhudia folen kubwa sana ya watu wenye shida mbalimbali ila idadi kubwa ni wanawake.

Tukiwa pale kuna mteja mmoja ndio alikuwa anahudumiwa na Babu.

Ndipo kwa mara ya kwanza kuona Babu akivuta msukule kupitia Mitambo yake.

Ndugu wa yule mgonjwa walilia sana kwa furaha.

Ikawa babu anahangaika na Madawa ili amrejeshe vizur akili yake aweze kuongea.

Wakat tupo pale baadae nikaona tena Wagonjwa wengine wakitoa shukran zao kwa kumpa Babu zawad.

Nilijaribu kudadisi kwa Wajukuu zake nikaambiwa.

A) Mzee Mangi alikuwa na kesi ya Kuua lakin file la kesi yake lilipotea hivyo kesi ikafa na yule Afande aliyeshika file alipata ajali na amelazwa hospital

B) Mama Omar alifanikiwa kurudiana na Mume wake aliyemtelekeza takriban miaka mitano.
Mama huyu alihudumiwa na Babu kwa siku saba tu

C) Ustadh Hussen nae alifanikiwa kupata utajir kwa njia nyepes tuu siyo kuua binadam bali kuchinja Mbuzi mmoja kwa Mwaka kila Tareh ikifika

D) Nikaona ...... Akimkabidhi babu Solar baada ya kufanikiwa kuua ndugu.... Aliyekuwa akimsumbua Sana.

E) Mama Zuwena alitoa sh... Ya shukran kwa Babu baada ya Mgahawa wake kujaza wateja sana na chakula hakilali.
Hivyo dawa ya Mvuto wa biashara iliyochanganywa na .... Ilifanya kazi vizur.

Note: Shoga yangu nae alirudishwa kazin baada ya wiki moja na hivisasa tupo Dar tumechukua likizo angalau tubadilishe Mazingira..

Kiufupi huyu Babu anawajukuu zake ambao ndio huwa anawatuma kuchimba dawa na anachanganya na VISIMBA na mambo mengine anayoyajua yeye....

Mmh! Najua kuna watakao toa Povu ila uhalisia ni kwamba Ushirikina/Uchawi upo na watu wanapata huduma mbali mbali wanafanikiwa ila watakaosema Uchawi haupo basi hao hawajapata matatizo.

Namba za huyo Babu.
(+255678134718) kwa ufafanuz zaid..
 
HIVI karibuni, serikali imeendesha na inaendeleza, zoezi la kupiga marufuku waganga wa tiba za jadi na “watabiri” wapigao ramli kwa kutumia zana mbalimbali za jadi, kwa madai ya kuchochea imani za kishirikina na kusababisha mauaji ya “albino” na vikongwe nchini.
Zoezi hili limekuja wakati huduma za tiba za kisasa kwa wananchi nchini zimefifia, kufuatia serikali kujitoa kuchangia huduma za jamii na hivyo kufanya watu wengi wakimbilie tiba mbadala za jadi kwa kutoweza kumudu gharama za tiba za kisasa.

Hapa ndipo soko la waganga wa jadi linapobubujika na kufura wateja; hapo ndipo wataalamu hao wa sayansi ya kale/jadi wanapoibuka na zana zao za kazi; shughuli ambayo kwa “ujinga” wetu na kwa kubeza jadi na utamaduni asilia, tumeipa jina baya: “Uchawi”, kwa kuyumbishwa na Sheria ya Kikoloni ya “Uchawi” – The Witchcraft Act, Cap. 18 [kama ilivyorekebishwa mwaka 2002], ambayo kabla ya hapo ilijulikana kama “The Witchcraft Ordinance”, 1928.

Chini ya Sheria hii [kifungu cha 2] “Uchawi” – au “Witchcraft” kwa Kiingereza, umetafsiriwa kumaanisha na kujumuisha Ulozi [sorcery], mazingaombwe [enchantment] kuloga [bewitching], kuzingua na kutegua; matumizi ya vifaa vya uchawi, matumizi ya nguvu za kufumba jambo [occult] na kumiliki elimu ya kufumba mambo/usiri au usihiri [occult knowledge].

Vifaa au zana za uchawi vimetajwa kujumuisha, kitu chochote ambacho kwa kawaida kinatumika au kuwakilisha au kuaminika kuwa na nguvu ya kuzuia, kuchelewesha mtu kutenda tendo lolote analotaka kufanya kisheria, au kulazimisha mtu yeyote kutenda tendo ambalo kisheria hapashwi kutenda.

Pia, kugundua tuhuma ya kijinai iliyofichika dhidi ya mtu, au kusababisha kifo, kujeruhi au kusababisha ugonjwa kwa mtu au kuharibu mali, au kumuogofya mtu; au kwa kutumia nguvu za juu za asili zilizofichika kuzalisha dhana ya kiasili, na ni pamoja na dawa zinazotumika kwa madhumuni hayo.

Kama, kwa tafsiri chini ya Sheria ya Uchawi, ni kosa la jinai kwa mtu, kutumia “wachawi” kumwogofya mtu kwa kutabiri au kumtabiria kifo, kama vile wagombea nafasi za kisiasa; au adhabu ya moto wa milele ahera baada ya kifo; au uzima wa milele kwa “fumbo la imani”, basi, vivyo hivyo, wahubiri wa “dini” za mapokeo wanaohubiri hivyo kwa misahafu nao ni wachawi, na misahafu wanayotumia kuwasilisha hayo ni zana za “uchawi”.
Kama hivyo sivyo, basi, waganga wa jadi wanaotabiri matukio, au kuagua kwa njia ya ramli si wachawi; na zana watumiazo si za kichawi, kama tutakavyoona katika makala haya.

Kwa sababu hii, kitendo chochote cha kupiga marufuku kila kitu kilicho cha jadi kinachotumiwa na wenyeji bila kudadisi kisosholojia mantiki nyuma yake, ni kuudhalilisha na kuukana Uafrika, mila, jadi na sayansi asilia ya Mwafrika kwa kutukuza vya kigeni.
Tamaduni, dini na mila za Kiafrika zimejikita kwenye zana na vitendea kazi mbalimbali vya imani [kama vilivyo vitendea kazi vya dini za mapokeo], kama vile uaguzi, ubashiri na utabiri [divination], tafsiri za ndoto, ishara [omens] na nguvu [cult] ya mizimu [spirits].
Waafrika wanaamini, kwa haki yao, juu ya nguvu ya mababu [ancestors] kama kiungo na suluhisho kati ya walio hai na Mungu. Imani hiyo na ibada zake hufanyika kupitia viwakilishi [mediums] kama vile tambiko kwa kutumia vifaa vya kidunia na matoleo [offerings] kama yalivyo matoleo mengine tu kwa dini za mapokeo.

Ugomvi uliopo ni kwa dini za mapokeo kutotambua Miungu wa dini za jadi, kuashiria ubeberu wa kiutamaduni [cultural imperialism] wa mwenye nguvu dhidi ya Mungu wa tamaduni zingine.

Ndiyo maana, Afrika hadi leo, haijaweza kutoa Watakatifu kwa misingi ya mila na tamaduni zake, ila kwa misingi na vigezo vya utamaduni wa Ulaya, kwa maana kwamba hakuna cha kutamani walichoacha mababu na hivyo wako “Jehanamu”.

Waafrika watetezi wa dini za jadi wameendelea kuuliza, “Utaabudu vipi Mungu asiyejua lugha yako?; Mungu asiyejua mizizi yako, maadili na matakwa ya mababu zako?”.
Na hii ni historia kujirudia, ya Wanaisraeli walipopelekwa utumwani Babiloni, walikokataa kuabudu Miungu ya nchi hiyo wakihoji, “Tutaimbaje Wimbo wa Bwana [Mungu wa Israeli] katika nchi ya ugenini?” Nasi tunauliza, kwa nini Mwafrika anapouliza swali hilo hilo la Waisraeli aitwe “Mchawi” na kutungiwa Sheria za kigeni?.

“Jukumu la kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini”, yasema Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya1997, ibara ya 19 (2), “litakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu binafsi….”.Kwa mantiki hiyo, kama dini ni jambo huru la mtu au vikundi vya kijamii, basi, Serikali haiwezi kuwachagulia watu jinsi na namna ya kuabudu wala zana za kuabudia, mradi tu hawavunji Sheria inayokubaliwa na wengi.

Kama wengine wanadai kuundiwa Mahakama za dini zao kwa gharama za Serikali na kusikilizwa; kwa nini hawa wa “dini” za jadi nao wasipewe fursa sawa kama hiyo, badala ya kutiwa rumande na kufungiwa “ibada” kila mara?.

Katika kutenda kazi, Mganga wa jadi huvalia mavazi aina mbalimbali, mengine ya kuogofya kwa muonekano. Haya yanaweza kuwa ngozi ya mnyama, shanga, “mgwisho”, manyoya ya ndege, bangili na mengineyo yanayoelezea mazingira yanayomzunguka mwanasayansi huyo.

Mavazi haya yana madhumuni mawili: kwanza, ni kutia imani ya mteja kwa Mganga huyo; na pili ni kumpandisha hadhi kwa kujitofautisha na watu wa kawaida na jamii yake. Hili ni suala la mavazi tu kwa kila shughuli, kama ilivyo kwa Jaji wa Mahakama, Meya na Madiwani, Daktari na wengine wenye kujikweza kwa muonekano kwa mavazi wakiwa kazini.

Lakini pamoja na hayo, hili haliondoi uwezekano na kuwapo Waganga wa jadi matapeli kama ilivyo kwa fani zingine, lakini isiwe samaki mmoja akioza, wote wachukuliwe wameoza.

Inafahamika kwa jamii na Wataalam wa Sosholojia pia kuwa, kutambua au kutibu ugonjwa na kuchawiwa [uganguzi] sio sawa na kutenda Uchawi; na pia Waganguzi hao wanatambuliwa na kulindwa na kifungu cha 37 cha Sheria, Sura [Cap] 409 kinachosema: “Hakuna kinachokataza au kuzuia katika Sheria hii matumizi halali ya mifumo ya kutambua magonjwa kwa njia za jadi na watu wanaotambuliwa na jamii waliyomo kuwa na ujuzi wa kutibu kwa njia za jadi”.

Na hili lilikwishakemewa na Mahakama katika Kesi ya Thomas Bangili na Samike Maduhu dhidi ya Jamhuri [1969] HCD 246; kwamba uganga na uganguzi wa jadi na vifaa vinavyotumiwa na waganga wa jadi, si uchawi wala ushirikina.

Katika kesi hiyo, washitakiwa hao wawili walituhumiwa na kuhukumiwa kifungo kwa kujifanya kuwa na nguvu za kichawi kinyume na kifungu 3 (3) na 5 (2) cha Sheria ya Uchawi. Tuhuma ya pili ilikuwa ni kukutwa na kibuyu cha kuagulia kinachoongea; na ya tatu, kutoa kwa matumizi kifaa cha kichawi, yaani kibuyu kinachoongea.

Wawili hao walikuwa ni waganga wa jadi waliotambua ugonjwa wa mteja kwa kutumia “mizimu” na kibuyu kinachoongea kuweza kutibu kwa dawa, na pia kuwaondolea madhara ya kutokana na kulogwa.

Akiwaachia huru, Kimicha, Jaji [alivyokuwa wakati huo], alikuwa na haya ya kusema: “…. Ni jambo linalofahamika kwamba, jamii yetu kwa miaka mingi imenufaika na utaalamu na huduma zitolewazo na waganga wa jadi waadilifu, kwa kutibu magonjwa mbalimbali katika jamii yetu….. Matabibu wa kisasa, wao wana vifaa vya kisasa vya kubaini ugonjwa, kama vile X-ray, kabla ya kutoa dawa kwa mgonjwa; lakini waganga wetu wa jadi hawana X-ray wala maabara; na kwa kutambua mapungufu hayo, hutumia mbinu za jadi zinazoweza kuitwa unajimu [fortune telling], au kile kinachoweza kuitwa “akili ya sita” [sixth sense], au mizimu [spirits] kwa kijadi kwa mafanikio na kwa sifa kubwa…..”.

Akaongeza kusema: “Sheria ya Uchawi haikutungwa kuzuia au kukataza wale wanaotambua au kutibu watu magonjwa au waliologwa kichawi. Wala kutambua au kutibu mtu aliyelogwa si sawa na kuendesha uchawi; vivyo hivyo, zana anazotumia mganga wa jadi katika kutekeleza shughuli zake, si zana za Uchawi”.

Kwa mtazamo huo wa Mahakama, ni vigumu [na si sahihi tena] kwa vyombo vya dola kuthibitisha kisheria “vitendo na vifaa vya Kichawi” kwa kuangalia zana zitumiwazo na waganga wa jadi katika kuagua,kuganga na kugangua.

Ilikuwa rahisi hapo kale, wakati wa ukoloni mkongwe, Sheria ya “Uchawi” ikitungwa; ambapo dini na ngoma za jadi zilibezwa na kudharauliwa na wakoloni na kupewa jina baya – “Wapagani, wasiostaarabika, washamba, washenzi [uncultured] waabudu mizimu na shetani”; kwa sababu tu ya kutomtambua Mungu wa utamaduni wa kigeni.

Katika kipindi hicho, uponyaji wa jadi ulihesabiwa kama kitendo cha kichawi na ushirikina, tofauti na kipindi hiki cha “mwanga” ambapo mambo yamebadilika, kwa sayansi ya jadi kupewa kiti katika jamii.

Vivyo hivyo, baadhi ya madhehebu ya dini yameruhusu Mwafrika kumwabudu Mungu katika mazingira yake kwa njia ya “kutamadunisha liturujia” kumfanya muumini afurahie “ukombozi” katika mazingira yake, badala ya kumlazimisha kuabudu kwa mazingira ya kigeni, kama walivyolalama wana wa Israeli utumwani Babylon.

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu haujatenguliwa na Mahakama yoyote ya juu, na hivyo umekuwa Sheria, kwa sababu Uamuzi wa Mahakama Kuu na za juu yake kuhusu utata wa kisheria [precedents] kwa jambo la kisheria, unabatilisha utata unaobishaniwa kuweza kusababisha marekebisho ya Sheria husika.

sKwa hiyo, kitendo cha dola kukurupuka kufungia baadhi ya waganga wa jadi bila udadisi wa kina na bila kuzingatia matakwa ya sheria, ni batili.

Lakini pamoja na juhudi za kufungia madaktari hao wa jadi, ni yupi kati ya wanasiasa na Watendaji Wakuu Serikalini, asiyetembelea Sangoma huko Bagamoyo, Sumbawanga, Tanga na Pemba ili “kuangalia njia” na kwa tiba za magonjwa yaliyoshinda madaktari wa kisasa na zama zao?

Mbona Kijiji cha Samunge, miaka michache iliyopita, kilifurika “wateja”, wakubwa kwa wadogo, wasomi kwa wasiosoma, wakipenya kwa misuli, kuonja kikombe cha Babu aliyeoteshwa tiba hiyo?.

Huko Unguja na Pemba, kati ya mwaka 1940 – 50, jina la Bi Kirembwe wa Giningi, lilikuwa maarufu kwa mambo ya utabiri sahihi, ukiwamo ule juu ya Mapinduzi ya umwagaji damu Zanzibar, ya Januari 12, 1964, miaka mitano kabla ya kutokea. Waasisi wa Mapinduzi hayo walifanya tambiko mara nyingi pale Dunga kuhakikisha Mapinduzi yanafanikiwa.
Uchawi, kwa mtazamo wa Sheria ya Uchawi tuliyoinukuu hapo juu, unajumuisha pia usomaji nyota. Kama hivyo ndivyo, vitabu kama vile “Shamsa-al-Ma’araf” na “Mamba’a Usual al Hikmah” vya Ali-al-Buni; “Sa’at al Khabar” cha Abu Ma’ashar al-Falaki, “Khazinat al-Asraar al kubra” cha Muhammad Afandi an-Nazil; “Muyarrabat” cha ad-Dayrabi na “al-Jawahir al-Lama’a” cha Ali-al-Marzuki, vinavyotumika katika unajimu, basi navyo ni zana za uchawi, kama zilivyo tu zana zingine wanazotumia waganga wa jadi kwa shughuli zao.
Kama hivyo ndivyo pia, kwa nini waandamwe Waganga wa Jadi pekee; na Wanajimu wa mjini kuachwa kufurahia “ushirikina” wao? Kama huu hauwezi kuitwa ubaguzi chini ya ubeberu wa kiutamaduni, basi jambo hili tuliite kwa jina gani?s

Hebu angalia wakubwa nao wanavyojitegemeza kwa sayansi ya jadi bila kuhojiwa: Aliyekuwa Rais wa Sudan, Jaffar Nimeiry, alijishirikisha sana na uchawi wa kikundi cha “Sufi” ili kubakia madarakani asipinduliwe. Mgangas wake aliogopwa Sudan nzima.
Rais wa Zaire [sasa DRC] wa zamani, Mobutu Seseseko, inadaiwa alidumu madarakani kwa “nguvu za giza” kwa uchawi uliokuwamo kwenye fimbo yake [mkongojo] ambao hakuachana nayo, akiamini kwamba kila alipoinua fimbo hiyo, kila jambo lilimnyookea.
Inaelezwa pia, hayati Jomo Kenyatta, Rais wa kwanza wa Kenya, nguvu zake za kisiasa zilikuwa kwenye “mgwisho” [fly-whisk], kama zilivyokuwa nguvu za Mfalme Haile Selasie wa Ethiopia, kwenye pete aliyovaa daima.

Kenyatta na wapiganaji wenzake wa vita ya “Mau Mau”, kama Dedan Kimathi na wengine, waliwachachafya wazungu vitani kwa ndoto za “mizimu” zilizowawezesha kuelewa matukio yote vitani.

Inaelezwa, alijua siku ya kufa kwake, akaamua kufia Nakuru mwaka 1978, badala ya Nairobi ili kuepusha ghasia za kuwania urithi miongoni mwa wanasiasa wa nchi hiyo.
Awali, Kenyatta alijulikana kwa jina la kigeni la Johnstone Kamau, lakini baada ya kurejea kwenye “mizizi” na maisha ya utamaduni asilia, alibadili jina na kuitwa Jomo Kenyatta, na inadaiwa alinusurika kifo na majanga mara nyingi kutokana na mzimu wa mababu ujulikanao “Mundi Mugo” ambao ndio uliompa “mgwisho” na pete ya kinga yenye nguvu.
Naye aliyekuwa Rais katili wa Guinea ya Ikweta, Marcia’s Nguema, inadaiwa alidumu madarakani kwa ukatili mkubwa wa kuuwa raia hovyo, akihofiwa kutumia nguvu za giza. Na alipopinduliwa, Septemba 1979 na kuhukumiwa kifo kwa kupigwa risasi, kazi hiyo ilibidi ifanywe na wanajeshi kutoka Morocco, baada ya askari wa Guinea ya Ikweta kuufyata wakihofu kwamba mzimu wake ungewarudia katika umbo la chui.

Je, wanaoponya kwa maombi na miujiza kwa njia ya “dini”, wana tofauti gani na wanaofanya hivyo kwa mila na jadi za Kiafrika? Kwa nini nao wasiandamwe?.
Lini tutaacha tabia na utamaduni wa kupokea pekee na kumeza kila kitu [kutoka nje]mithili ya dodoki; ili badala yake nasi tuweze kutoa utamaduni wetu asilia kwa jamii ya kimataifa?. Lini tutapata akili ya kukataa kuporwa “roho” na rasilimali chini ya ubeberu wa kimataifa? Tutafakari.View attachment 827712
Mkuu jifunze kuandika ufupisho, maana nimeshindwa kuelewa unatetea nini haki ya wewe kuturoga!
 
Hahaha mkuu Kwekitui leo umemaliza kabisa ubishi wangu na hawa GT wa humu JF. Kuna watu humu mwaka ulivyoanza walisema wamesoma vitabu 50, wengine walisoma vitabu 100, n.k

Lakini kinachonishangaza leo hii huu uzi sijui ni page ngapi ingekuwa vile vitabu wanavyosoma, lakini wote wanalalamika kwama uzi huu ni mrefu sana, hadi kuomba ufupishwe.

Huyu muandishi hataki maswali, topic kaipiga katafunua ile pindupindu, hakubakiza kitu, sasa wale wasomaji wa vitabu mnanitia aibu leo hamuwezi kumaliza kuusoma uzi huu.

Nilipoandika mimi sijasoma kitabu hata kimoja tangu nimalize chuo 2001, nilishambuliwa sana humu.Wasomaji walinishauri sana nianze kusoma vitabu, sasa imekuwaje kiuzi hiki kiwashinde kumaliza?

Binafsi nilifika katikati ya uzi huu nikaanza kuona paragraph zinaanza kufanana, nikaaona isiwe tabu.

Someni acheni uvivu jamani, mbona zile za ndugu yetu Mshana Jr huwa mnamaliza kuzisoma, au kwakuwa yeye huwa anatoa na dawa kabisa?
 
Hapo ndipo wazungu walipo tuweza kwenye kudharau vya kwetu na kutukuza vya kwao. Kabla ya ukoloni babu zetu walitibiwa sana kwa miti shamba na wengi walipona.
Jaribu kutofautisha tiba asili ( uganga wa jadi) na upigaji ramli ( uchawi).

Bado kuna makabila mengi yanatumia tiba asili mfano wamasai, wahaya etc na dawa zao zinafanya kazi vizuri tu.
Faida ya tiba asili nyingi hazina chemicals nyingi ?( ni natural) tofauti na tiba ya kizungu ambayo ni synthetic ambazo nyingi sio rafiki wa figo na maini yetu.
Tusibeze na kutupa asili yetu kwa ulimbukeni wa kuthamini vya watu.
 
Back
Top Bottom