UGANDA: Wadau wa mitandao wakosoa kauli ya Rais Museveni

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekosolewa mwezi huu na wadau wa mitandao pale alipomtaka Waziri wa Fedha kutafuta njia ya kutoza kodi mitandoa ya jamii, ili kuzuia kile alichokiita ni “umbeya” katika mitandao.

Maafisa wamebadilisha maoni yao juu ya kauli hiyo, japokuwa wanasema kuwa wanafanya juhudi kuanza kutoza kodi kwa data inayotumika kwenye simu kila siku kuanzia July 2018.

Serikali ya Uganda imesema kuwa matumizi ya intaneti katika simu yameongezeka kwa asilimia 15 mwaka uliopita wakati watu wengi zaidi wamekuwa wakitumia huduma za mitandaoni kwa ajili ya huduma hiyo na kufanya malipo.

Hivi sasa, mapendekezo mawili yako mezani. Moja itatoza kodi ya asilimia moja kwa kila malipo ya fedha yanayofanyika kwa simu. Pendekezo jingine ni la kutoza ushuru wa kila siku wa kiasi cha centi tano, kwa wale wanaotumia data (bandal) ya simu.

Ni pendekezo la pili, ambalo linajulikana kama kodi ya mitandao ya jamii, ambayo inachochea mjadala mkubwa.

“Nafikiri siku hizi, kwa hakika kuna idadi kadhaa ya wafanyabiashara ambao wanatumia tu mtandao wa Instagram na Whats App na njia mbali mbali ambazo wanajitangaza kupitia intaneti. Kwa hiyo nafikiri tathmini ya rais ilikuwa haitendei haki malengo ya wale wanaotumia mitandao hiyo," amesema blogger Godiva Akullo.

Maafisa wa Baraza la Mawaziri wanatetea mapendekezo hayo ya kodi, kwamba utasaidia miundombinu kuboresha mawasiliano ya simu.

Source: VoA
 
Back
Top Bottom