Uganda kutengeza chanjo ya Covid -19

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,257
2,000
Serikali ya Uganda imeanza mchakato wa kutengeneza chanjo ya Covid 19 kama mataifa mengine duniani.

Mwaka jana Rais Yoweri Museveni alisema wanasayansi wa Uganda wanajaribu kufanya utafiti kuanza kutengeneza chanjo yao na tiba ya Covid-19 ambayo tayari iko kwenye majaribio.

''Ninafanya kazi na watu wangu kuanza kutowa chanjo yetu, sio kwamba tumekaa tu kusubiri watusaidie, tumechelewa lakini sasa tumeanza na chanjo yetu itakwenda kote duniani'' alisema Rais Museveni.

Aliendelea kusema: ''Tutaanza kufanyia majaribio panya mwezi wa june kuona kama ina madhara na baadae mwezi wa Augosti tutafanyia majaribio nyani na kusubiri kudhibitishwa na WHO.''

Rais Museveni ametowa kauli hiyo wakati alipodungwa sindano ya chanjo ya Covid-19 ya Astra Zeneca pamoja na na mkewe Janet Museveni, katika ikulu ya rais Nakasero mjini Kampala.

Bw. Museveni aidha ametowa wito kwa wananachi kujitokeza kupata chanjo kwani haina madhara.

1617003444806.gif
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom