Uganda kufanya usajili wa ng'ombe

miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Messages
2,094
Points
2,000
miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined May 18, 2014
2,094 2,000

Serikali nchini Uganda imedhamiria mpango wa kuwasajili wakulima na ng'ombe wao kwa ajili ya kurahisisha utambuzi na kuwawezesha fursa za soko la Kimataifa

Hayo yameelezwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Vincent Ssempijja alipokuwa akizindua maonesho ya wakulima katika viwanja vya Nile mjini Jinja, ambapo amesema soko la Kimataifa linataka nchi zinazozalisha mazao hayo kusajili.

"Wanahitaji kujua bidhaa wanazonunua zinatoka wapi, wamekuwa wakikataa kulipa na kuzuia bidhaa zilizosafirshwa kutoka Uganda pindi wanakuta boksi moja lina shida", amesema Waziri Ssempijja.

"Wakulima watasajiliwa na bidhaa wanazozalisha zitapewa utambuzi wa 'barcodes', ili kama wakigundua box lina kasoro, wafuatilie chanzo na kurekebisha. Hatuwezi kuingia katika soko la aina hiyo hadi hapo tutakapowasajili".

Pia kuhusiana na suala la usajili wa ng'ombe, Waziri huyo wa Kilimo amesema, "kwa wafugaji wa ng'ombe watasajiliwa wenyewe na ng'ombe wao pia watasajiliwa na kupewa vyeti vya kuzaliwa kwa sababu walaji wanahitaji nyama ya ng'ombe yenye umri kati ya miezi 15 hadi 24. Kwahiyo tunakwenda kuuza kutokana na umri wao".
 

Forum statistics

Threads 1,325,699
Members 509,266
Posts 32,199,856
Top