Ufunuo wa Mchungaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufunuo wa Mchungaji

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Apr 15, 2010.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Naam, nami nikapewa maono ya hatima ya Taifa letu katika njozi.

  Tanzania itaruhusu Uraia wa zaidi ya nchi moja, maarufu kama Uduo mwaka huu 2010 kabla ya uchaguzi mkuu.

  Kutakuwa na Serikali ya mseto Zanzibar na wagombea huru wa Ubunge, Uwakilishi na Urais wa Serikali ya Mapinduzi na Serikali ya Muungano mwaka huu na maamuzi yameshafanyika ila kinachoendelea ni kupumbazana ili kujenga joto kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010.


  CCM itapoteza nafasi yake kuwa chama tawala kwa kipindi cha miaka kati ya mitano hadi kumi, kuanzia uchaguzi mkuu huu wa 2010.

  Rais wa Tano wa Tanzania hatatokea CCM, bali atatokea hama kingine kwenye uchaguzi mkuu wa 2010 ama sivyo uchaguzi mkuu 2015.

  CCM itameguka makundi mawili makubwa bila ya kuanzishwa kwa chama kipya cha Upinzani na ugomvi ndani ya CCM ndio utakaosababisha utata uliopo sasa hivi kuhusu mgombea huru, serikali ya mseto kupatiwa ufumbuzi ambao umeshapatikana mapema na kinachoendelea sasa hivi ni mazingaombwe kuzidiana akili ndani ya chama na kuachiana lawama.

  Mafisadi ndani ya CCM, wataachia ngazi kugombea madaraka na kuridhika na neema walizozipata na watakazoendelea kuzivuna kwa miezi sita ijayo.

  Wapiganaji wa CCM, watapoteza nguvu ndani ya chama, watapoteza umaarufu katika Taifa na wataangushwa kwa kishondo kikali kuanzia uchaguzi mkuu huu na wataachiwa CCM itakayopoteza nguvu kwa miaka 5 na kufilisika kisiasa ili kutoa nafasi kwa CCM mpya kuzaliwa.

  Chama kipya tawala na hata mkusanyiko na umoja wa vyama vinavyopingana na CCM vitakuwa na wakati mgumu kuleta maendeleo kwa Taifa na watapoteza muda mwingi katika miaka yao ya uongozi kujaribu kutatua matatizo yaliyoachwa na CCM kwa makusudi na watashindwa kazi kama mfupa uliomshinda fisi na hivyo kupoteza kabisa imani ya Watanzania kuwa vina uwezo wa kuongoza nchi.

  Vyama ya upinzani vitaendelea kuwa na msuguano na migongano ndani ya vyama vyao na katika umoja wao dhidi ya CCM na hili litasababisha Wananchi wakose imani na kuililia CCM.

  CCM hata baada ya kupoteza hatamu za uongozi, itakuwa na mtaji mkubwa kupindukia wa kifedha na kisiasa utakaoambatana na msukumo kutoka kwa sekta binafsi na wawekezaji kujiunda upya na kujirudisha tena madarakani.

  CCM itaanza kujiundaa upya kisiasa na kimfumo kuchukua madaraka tena kama chama tawala na Rais mpya (kiongozi mpya wa chama) ambaye hayuko kwenye ulingo wa siasa sasa hivi bali katika sekta binafsi na za kimataifa ambaye amekulia katika mazingira ya Wazazi ambao ni Wanasiasa. Kujisuka huku upya kwa CCM kutaleta sura mpya za CCM ikiwa chini ya vijana kama Heri Bomani, Deo Mwanyika, Nape Mnauye, Januari Makamba na wengineo ambao watakuwa chini ya huyu kiongozi mpya ambaye si kutoka kundi la wapambanaji au la mafisadi.

  Kiongozi mpya huyu wa CCM (si Lau Masha) atatokea ukanda wa Magharibi na anapikwa na wazee marufu kutoka ukanza wa Kaskazini Magharibi ambao sasa hivi wamefanya kazi chini ya Mkapa hata mtandao wa Kikwete.

  Uhujumu wa hali ya juu na kisayansi umefanyika, unafanyika na utaendelea kufanyika bila kugundulika kwa urahisi au kueleweka katika kipindi kijacho cha miezi 6 kabla ya kuapishwa Rais na Bunge jipya hapo Disemba 2010, nao utafanywa kwa makusudi ili kuambatana na hali ya mfukuto wa kisiasa na ulevi utakaotokana shangwe na maadhimisho kutokana na matokeo ya maamuzi ya ugombea huru, Serikali ya Mseto Zanzibar na Uraia wa nchi mbili.

  Hapatakuwa na umwagaji damu, vurugu au kuvunjwa kwa haki za watu kutokana na maamuzi yatakayotokea, ila Watanzania watapumbazwa na matokeo huku wakihujumia bila kujijua na watakapoamkaa hapatakuwa na nafasi nzuri kwa yeyote yule kupata ufumbuzi wa haraka bila kupoteza takriban miaka 5 hadi 10 kujaribu kufumbua mafumbo na hivyo kupoteza na kukosa nafasi ya kujenga nchi na kuishia kukimbiza mzuka.

  Katiba ya Tanzania itaendelea kuwekwa viraka na si kuundwa upya.

  Nami nikazinduka kutoka kwenye maono nikiwa natetemeka na kutokwa jasho kupita kiasi kwa kuona ukweli wa kinachoendelea.....!
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,300
  Likes Received: 22,102
  Trophy Points: 280
  Sheikh yahya .com part ||
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Not at all, its pure science and reality on ground, just wait and watch!
   
 4. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Rev Kishoka,

  Umenikumbusha ule wimbo "the long term benefits of sunscreen have been proved by
  scientists whereas the rest of my advice has no basis more reliable than my own meandering experience¬Ö"
   
 5. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mimi nasubiri utimilifu wa huo unabii, endelea kusogea barazani pa BWANA
   
Loading...