UFUNGUZI WA BARABARA YA JUU YA UBUNGO INTERCHANGE KUTOKA MWENGE HADI BUGURUNI NI USHINDI MWINGINE KWENYE VITA HII YA KIUCHUMI.
Na Bwanku M Bwanku
Jumatano ya Septemba 30 mwaka huu, Serikali ilifungua barabara ya Juu ya Ubungo Interchange kipande kinachotoka Mwenge hadi Buguruni kwenye makutano ya barabara za Morogoro, Nelson Mandela na Sam Nujoma jijini Dar es Salaam. Barabara hiyo inafunguliwa eneo ambalo limekuwa na tatizo kubwa sana la foleni na msongamano mkubwa wa magari takribani elfu 68, 872 yanayotumia barabara hiyo kwa siku na kusababisha foleni kubwa ya magari inayolilazimisha jiji kukwama na kusimama sana kwenye uharaka wa shughuli za watu kwenda maeneo mbalimbali ya jiji na kutoka.
Mradi huo wa barabara za juu wenye thamani ya bilioni 200.7 unafunguliwa ili kulifanya jiji la Dar es Salaam litembee na kuwa bize na shughuli za watu badala ya hali ya watu kutumia muda mwingi wakiwa kwenye misululu ya foleni ambayo imekuwa ikila muda halisi wa watu kufanya kazi na kuifanya nchi kupoteza mabilioni ya shilingi kwenye foleni hizo hasa kupoteza mafuta mengi sana.
Kwa mujibu wa ripoti ya Centre for Economic Prosperity ya mwaka 2010 ililitaja jiji la Dar es Salaam kuwa moja ya majiji yanayoongoza Afrika kwa kupoteza zaidi ya bilioni 4 kwa siku 1 kwa sababu ya foleni na msongamano wa magari mabarabarani kwa watu wengi kutumia muda wao mwingi barabarani kwenye mafoleni na kusababisha kupoteza mafuta, jambo linalopunguza pia masaa ya watu kufanya kazi na gharama ya watu kufika maeneo yao ya kazi kuwa kubwa sana.
Ufunguzi wa barabara hii ya juu ya Ubungo Interchange ni hatua muhimu na ya ushindi mkubwa sana kiuchumi kwa kulifanya sasa Jiji la Dar es Salaam kutembea na kurahisisha shughuli za kiuchumi za watu na kuondoa hali ya watu kutumia muda mwingi wa karibu asilimia 30 kwa siku kwenye mafoleni.
Huwezi kujenga uchumi imara na unaogusa watu wote bila ya kuwa na miundombinu mama na imara ya kiuchumi na maendeleo. Jiji kama Dar es Salaam ambalo karibu asilimia 60 ya kodi ya nchi inatoka ni lazima kuboresha miundombinu yake ya kiuchumi, biashara na uwekezaji ili kurahisisha watu kufanya shughuli zao bila ya bughudha na kero zozote zile zinazoweza kusimamisha shughuli za uzalishaji na maendeleo ili sasa kulifanya jiji liwe bize na kazi badala ya kuwa bize barabarani kwenye mafoleni.
Hii ina maana badala ya watu kutumia masaa kwa masaa kwenye foleni, sasa mtu anaweza kutoka Mwenge kwenda Buguruni na kwenda au kutoka sehemu mbalimbali za jiji kwa dakika chache tu ili akaendelee na shughuli zake za uzalishaji na uchumi wa nchi yetu.
Kama nilivyosema Dar es Salaam ni jiji la kimkakati, kitovu cha uchumi na maendeleo ya nchi yetu. Hatua hii ni kubwa na ya kupongeza sana ambayo inaenda sasa kuchochea shughuli za kiuchumi jijini Dar es Salaam kwenda kwa haraka na kwa muda mrefu sana.
Mfano, mtu ambaye angetumia masaa mawili mpaka matatu kwenye foleni jambo ambalo linapunguza moja kwa moja saa za kufanya kazi leo kwa barabara hii itamrahisishia kufika eneo lake la kazi na kuongeza muda wake wa kufanya kazi na hivyo kuongeza uzalishaji wenye tija kwenye uchumi na kupunguza gharama za uzalishaji ikiwemo mafuta.
Hii ndio tafsiri ya maendeleo ya watu kupitia vitu na miundombinu yao ya kuboreshewa mazingira ya kufanya kazi na kushiriki shughuli zao za kila siku. Ni barabara inayoenda kupunguza kama sio kuondoa kabisa msongamano mkubwa wa magari na foleni ambayo ilikuwa ikiigharimu mabilioni kwa mabilioni nchi yetu. Ni ushindi mwingine wa nchi yetu kwenye vita hii kali ya kiuchumi ambayo Rais Dkt John Pombe Magufuli ameamua kuipigana kwa maslahi ya Watanzania wote.
0657475347