Ufundi Mchundo

Ufundi Mchundo

fimboyaukwaju

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2020
Posts
6,009
Reaction score
7,956
Nasogelea miaka 65 sasa,ukiachia elimu ya darasani nimejifunza ufundi wa vitu vifuatavyo:

1.Ni fundi friji au friza ambazo ni smart.Natengeneza bila shida yoyote

2.Fundi wa majiko ya gesi na ya umeme pia natengeneza bila shida

3.Fundi wa redio ai music system,natengeneza bila shida.Majirani zangu wote wanajua na wananiletea au kuniita makwao kuwatengenezea.Inapotokea spea zinatakiwa nawaelekeza kununua wakileta nawatengenezea na siwachaji pesa nyingi maana natengenezea hobby tu.

Yupo mama mmoja alinunua freezer yake 5 millions,siku moja ghafla ikazimika akijiandaa kufanya sherehe ya kupokea mahari,aisee aliliano,akatafuta mafundi,kila wakija wanafeli.Basi akawa anaongea na mke wangu,ndipo akamwambia anapigie.Akanipigie,nikaenda na tool box yanguNikaiangalia kwenye panel ikawa imetoa error ecf.

Nikamwambia atafute blower,akakodi blower na nikafungua lower back panel.Nilikuta vumbi ya ajabu ndipo nikatumia blower kwa uangalifu mkubwa maana ina condenser ya aluminium.Nilitumia saa 1 nikaisafisha vizuri sana,nikaifunga.

Nikaiwasha nikamsetia panel yake 4 na 18 na ikaanza kufanya kazi na nikaisogeza mbali na ukuta ili iweze kupumua vizuri.Hakuamini macho yako,friji iliyowashinda mafundi mie nikaitengeza bila shida,akaniuliza shem nikulipe ngapi,nilimchaji 50,000
 
Mkuu hayo yote ulikuwa unajifunzia wapi,weka muongozo mbona ni kama uneniinsipire sana.
 
Ujuzi mwingine ambao mimi ninao ni kupika,iwe vyakula vya kienyeji ama hivyo vya kutoka nje.Ni hobi yangu tu na kwakweli najua sana.Ujuzi mwingine ni wa kukata vioo na kubandika kwenye meza au makabati.Sasa mwaka jana nilienda dodoma,dada mmoja alinialika kwake.Nilikuwa hapo alimpa fundi kazi ya kubandika kioo kwenye meza ya chakula na alitaka kioo cheusi.Fundi akaleta kioo kwa guta na akaanza kushughulikia hicho kioo,kila akifanya kuweka anapata shida mno,yeye na wasaidizi wake.Mimi nilikaa kimya,almost siku ikapita bila mafanikio.Shida kubwa yule na mme wake walikuwa wanataka kioo kikishawekwa pembeni yake kisagwe ili kisije kuwakata mikono wanapokishafisha.
Yule fundi hakuweza akawa anatafuta kifaa cha kusugulia kioo hapati.
Basi nikamwambia fundi wewe bandika kioo kwanza,nikamsimamimia akakibandika vizuri sana tu.Nikamwambia fundi na yule mume wa yule dada aliyenialika,wanipeleke kwenye maduka vya hardwares.Nikanunua gloves,kinoo cha jiwe cha kunolea visu,misasa no 180, na 240 na tuka rejea nyumbani.Nikaloeka kwenye maji nusu saa,nikavaa gloves nikaanza kusugua pembeni ya kioo kwa saa 1,nikachukua msasa no 180,nikasugua sana na nikamalizia na msasa no 240 na kioo kikawa sawa unalitisha mkono na wala hakikukati.Wote walishangaa sana,yule fundi na hao wenyeji wangu.Basi nikamfundisha yule fundi akanishuluru sana,akanipeleka kiwandani kwake na kunipa zawadi ya zabibu.Huu ufundi nilijifunza maseno nilipokuwa naishi huku nikifundisha maseno university.Nilikuwa natembelea sana karakana mbalimbali ndipo siku moja nikawakuta mafundi wakisugua vioo.Nami nilivyorejea Mwanza hiyo kazi nilikuwa nafanya mwenyewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom