kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,870
- 7,752
kuna bomu limeshalipuka la wafugaji wachunga mifugo ila kama taifa tumechanganyikiwa hatujui lipi la kufanya au tunafanya ndivyo sivyo. wafugaji wachunga mifugo wanafuga kiasili. wanatumia maeneo makubwa kuchunga maeneo ambayo mfugaji binafsi hana uanisho wowote wa haki ya umiliki wa ardhi. leo hii idadi ya watu imeongezeka na maeneo kwa kila familia ya uchungaji kuendesha maisha kwa mfumo wao wa asili hakuna. familia za kifugaji zinazurura nchi nzima na kuingilia haki ya familia za wakulima kutumia ardhi zao kwa amani. kwa vyovyote ufugaji kwa mfumo wa uchungaji lazima udhibitiwe vinginevyo amani tuliyoizoea itapotea.
lazima tukubali si kila mwanafamilia wa kichungaji aruhusiwe kuridhi mfumo wa uchumi wa kichungaji. tunaweza kuanzisha utaratibu wa leseni ya mchungaji. iwe na masharti kuhusu eneo la kuendesha ufugaji. akikutwa eneo lingine aweze kudhibitiwa kwa sheria. kwa njia hiyo tutaweza kufisha mfumo wa kichungaji na kuhamasisha mfumo wa kisasa wa ufugaji wenye tija na matumizi bora ya ardhi.
karibuni wanajamvi kuchangia.