Ufugaji wa Bata Mzinga, Bata Bukini na Kanga: Maoni, Ushauri, Utaalamu na Masoko

Namba yako please inbox. Nahitaji sana vifaranga
Za muda huu wadau wa humu ndani. Kwa ishu ya bata mzinga ninao. kwa anaehitaji tunaweza kuwasiliana. Ninao wenye umri kuanzia mwezi mmoja, miwili na mitatu na bei ni nzuri ukilinganisha na umri wao. Karibu upate bata mzinga kwa manufaa yako ya ufugaji.
 
mkuu umeongelea yooote na ukasahau masoko...karibu kutupa fursa za masoko
 
Nina fuga bata nina muda mrefu sijala nyama ya kuku kabisa nyumbani labda nje ya nyumbani kitu ambacho kina nifanya nipende nyama ya Bata bata hatibiwi tibiwi kama kuku kuku kila mara chanjo!
Bata huwa nina Tafuna na mifupa kabisa bila hofu!
Kuku ma antibiotics kila mwezi wana pewa sio wa kisasa sio wa kienyeji labda kidogo kuku wa huko mikoani Ila pia dawa hawakwepi!
 
nataka bata perkin na bukin kama unao boss wangu
 
yes wanaliwa na ni watamu sana. sema tu bei yake huwa iko juu kiasi ndio maana watu wengine wanaogopa kununua
Duuh me sidhani kama nitaweza kuwala labda nipewe nyama yao bila kujua... bata wa kawaida tu nimeanza kuwazoea juzi kati tu.
 
hapa ndo huwa napenda yaani kama hujuikitu we uliza kisha utapata majibu yanayo stahili bila taabu na kuwaelewesha wengine maana hatamimi nilikuwa naitaji sana nshu hii
Nimeifurahia hii,nilikuwa sijui kanga anaatamia muda gani sasa nimeelewa.
 
Pia kanga anapiga kelele akiona kitu hatari mfano nyoka, vicheche na hivyo kuwakurupusha maadui Hawa waingiapo himaya ya mfugaji
 
Changamoto kubwa kwa kanga ni vifo vya ghafla kwa vifaranga. Mwanzoni nilichanganyikiwa unakuta kifaranga mzima kabisa akilowa kidogo tu na hata ukimgusa mikono ikiwa na vimajimaji ghafla anaanza kutetemeka na ndani ya nusu saa amekufa. Akipata stress kidogo amekufa.

Tatizo lingine ni udhaifu wa miguu yaani anatambalia tumbo miguu ime paralyze kabisaa na baada ya muda anakufa

Nilikuwa na vifaranga 200 kila siku wanakufa 10-20 mpaka wakabaki 92

Suluhisho:
Nilikwenda kwa mzee daktari dukani nikamueleza nahitaji chanjo ya kanga na nikampa sababu, akaniambia kanga huwa hashambuliwi na magonjwa Kama kuku na hivyo chanjo haina maana ila vifo kwa vifaranga ni kutokana na upungufu mkubwa wa vitamin A. Alinipa aminovet ya kuwachanganyia kwenye maji (bei 6000) niliwapa mchana ule ule siku ya pili walikufa 2 ambao walikuwa dhaifu na siku ya 3 hakuna kifo na ndiyo ukawa mwisho wa vifo.

Hii iminovet unawapa kila siku na wanaipenda sana, ukiwawekea maji pure hawanywi

Asante sana mzee wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…