Dume la bata mzinga linakula mayai

maramojatu

JF-Expert Member
Mar 16, 2012
1,167
1,530
Wadau, msaada tafadhali,

Nilinunua Bata mzinga siku za nyuma. Kama wiki mbili zilizopita Bata jike alianza kutaga na kufikisha mayai 6. Baada ya muda nikakuta yamepungua 2.

Nikawa na wasiwasi kuwa dume anakula mayai. Nilichofanya nikatoa mayai yaliyokuwa yamebaki. Akitaga tu natoa yai nahifadhi.

Baadae nikahamisha dume nikamrudishia mayai joke ili aatamie. Hata hivyo hakuatamia. Jirani yangu anayefuga Bata mzinga akamiambia jana kuwa dume la bata mzinga haliwezi kula mayai.

Kwa hiyo Leo asubuhi nimemrudisha Bata mzinga dume akae na joke. Lakini Cha ajabu mchana huu amekula yai moja.

Msaada tafadhali Kwa anayejua dawa ya kutibu tatizo hili. Asanteni
 
Wadau, msaada tafadhali,
Nilinunua Bata mzinga siku za nyuma. Kama wiki mbili zilizopita Bata jike alianza kutaga na kufikisha mayai 6. Baada ya muda nikakuta yamepungua 2. Nikawa na wasiwasi kuwa dume anakula mayai. Nilichofanya nikatoa mayai yaliyokuwa yamebaki. Akitaga tu natoa yai nahifadhi. Baadae nikahamisha dume nikamrudishia mayai joke ili aatamie. Hata hivyo hakuatamia. Jirani yangu anayefuga Bata mzinga akamiambia jana kuwa dume la bata mzinga haliwezi kula mayai. Kwa hiyo Leo asubuhi nimemrudisha Bata mzinga dume akae na joke. Lakini Cha ajabu mchana huu amekula yai moja.
Msaada tafadhali Kwa anayejua dawa ya kutibu tatizo hili. Asanteni
Pole sana kwa changamoto hii ktk ufugaji, naomba nikushauri jamii ya Ndege wakiwa wanakula mayai hiyo ni upungufu wa madini ya calcium sasa hapo unatakiwa uwapatie D.C. au chokaa au mifupa vyote hivyo utavipata toka kwenye maduka yanayouza vyakula vya mifugo.
Kumkata mdomo iwe suluhisho namba 2 baada ya kumpatia madini. Na ukataji unahitaji uangalifu maana huwa kunakipimo chake maalum cha kuweza kumkata hii ni kutokana usimbadili muundo wa mdomo wake asije kushindwa kula vyema. Mungu akubariki sana ktk ufugaji wako.
 
Back
Top Bottom