Ufugaji wa Bata Mzinga, Bata Bukini na Kanga: Maoni, Ushauri, Utaalamu na Masoko

Ben255

Ben255

New Member
Joined
Dec 6, 2017
Messages
2
Points
45
Ben255

Ben255

New Member
Joined Dec 6, 2017
2 45
Nataka kufuga bata mzinga ila naomba mnifahamishe changamoto zao pia naomba kujua upatkanaji Wa masoko ya kuwauza pia ni wap nitapata vifaranga vya bata mzinga?

Naomba msaada wenu wakuu

Sent using Jamii Forums mobile app
karibu mkuu kwenye fursa ya ufugaji wa bata mzinga. bata mzinga wanafugika kirahisi kuliko kuku kwa maana kwamba hawana changamoto nyingi kama kuku, ninawafuga bata mzinga pia nafuga kuku nimeona nakuthibitisha mwenyewe kauli hii niliyotoa. uzuri wao wana uwezo mkubwa wakustahimili magonjwa labda tuseme baadhi tu ya magonjwa ya kuku kama ndui ndio inaweza kuwasumbua ila si kwamba yaweza kuwaua kirahisi. ukiwa makini kuwapa chanjo na kua makini kufanya usafi bandani kwao. nikiwa na maana ya mazingira ya banda na vyombo vyakuwalishia chakula na maji, hutaona batamzinga akifa ovyo. jambo jingine ni umakini wa mazingira unapowafugia kwani hua wanapenda kudonoadonoa vitu mbalimbali na kumeza wakati mwingine vitu vikubwa ambavyo vyaweza kuwashinda kumeza jambo linaloweza kuwasababishia kifo endapo kitawakaba na kukosa mtu wakuwasaidia kutoa vilivyowakaba kooni. kuepuka changamoto hii ni kuhakikisha unawafugia bandani kwani humo bandandi utakua na uhakika na wanachokula hivyo kuepuka hasara inayoweza kutokana na changamoto hiyo. kwa anaehitaji vifaranga waweza kunitafuta kwa namba 0714756625 :::: 0623460298: napatikana dar es salaam
 
SPYMATE

SPYMATE

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2013
Messages
936
Points
500
Age
39
SPYMATE

SPYMATE

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2013
936 500
Changamoto kubwa kwa kanga ni vifo vya ghafla kwa vifaranga. Mwanzoni nilichanganyikiwa unakuta kifaranga mzima kabisa akilowa kidogo tu na hata ukimgusa mikono ikiwa na vimajimaji ghafla anaanza kutetemeka na ndani ya nusu saa amekufa. Akipata stress kidogo amekufa.

Tatizo lingine ni udhaifu wa miguu yaani anatambalia tumbo miguu ime paralyze kabisaa na baada ya muda anakufa

Nilikuwa na vifaranga 200 kila siku wanakufa 10-20 mpaka wakabaki 92

Suluhisho:
Nilikwenda kwa mzee daktari dukani nikamueleza nahitaji chanjo ya kanga na nikampa sababu, akaniambia kanga huwa hashambuliwi na magonjwa Kama kuku na hivyo chanjo haina maana ila vifo kwa vifaranga ni kutokana na upungufu mkubwa wa vitamin A. Alinipa aminovet ya kuwachanganyia kwenye maji (bei 6000) niliwapa mchana ule ule siku ya pili walikufa 2 ambao walikuwa dhaifu na siku ya 3 hakuna kifo na ndiyo ukawa mwisho wa vifo.

Hii iminovet unawapa kila siku na wanaipenda sana, ukiwawekea maji pure hawanywi

Asante sana mzee wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Vipi dawa ya minyoo huwapi?
 
Hamza chimpaga

Hamza chimpaga

Member
Joined
Sep 25, 2018
Messages
11
Points
45
Hamza chimpaga

Hamza chimpaga

Member
Joined Sep 25, 2018
11 45
karibu mkuu kwenye fursa ya ufugaji wa bata mzinga. bata mzinga wanafugika kirahisi kuliko kuku kwa maana kwamba hawana changamoto nyingi kama kuku, ninawafuga bata mzinga pia nafuga kuku nimeona nakuthibitisha mwenyewe kauli hii niliyotoa. uzuri wao wana uwezo mkubwa wakustahimili magonjwa labda tuseme baadhi tu ya magonjwa ya kuku kama ndui ndio inaweza kuwasumbua ila si kwamba yaweza kuwaua kirahisi. ukiwa makini kuwapa chanjo na kua makini kufanya usafi bandani kwao. nikiwa na maana ya mazingira ya banda na vyombo vyakuwalishia chakula na maji, hutaona batamzinga akifa ovyo. jambo jingine ni umakini wa mazingira unapowafugia kwani hua wanapenda kudonoadonoa vitu mbalimbali na kumeza wakati mwingine vitu vikubwa ambavyo vyaweza kuwashinda kumeza jambo linaloweza kuwasababishia kifo endapo kitawakaba na kukosa mtu wakuwasaidia kutoa vilivyowakaba kooni. kuepuka changamoto hii ni kuhakikisha unawafugia bandani kwani humo bandandi utakua na uhakika na wanachokula hivyo kuepuka hasara inayoweza kutokana na changamoto hiyo. kwa anaehitaji vifaranga waweza kunitafuta kwa namba 0714756625 :::: 0623460298: napatikana dar es salaam
Vipi kuhusu upatikanaji wa masoko kuhusu hii biashara ya bata mzinga ikoje?
 
Forum statistics

Threads 1,293,770
Members 497,735
Posts 31,152,968
Top