Ufugaji wa Bata Mzinga, Bata Bukini na Kanga: Maoni, Ushauri, Utaalamu na Masoko

Mkuu hebu soma juu alivoandika prof Ndumilakuwili.Tembea uone mengi mkuu kama hujatambea duniani huwezi jua kwanini nimeuliza swali hili.

Nenda mahoteli makubwa ya kitalii agiza nyama inaitwa Turkey(Bata mzinga) kisha uniambie ni shs ngapi.

Bata mzinga mmoja mkubwa sana bei yake ni shs laki mbili je kuku wa mitaani wa wakaanga chips mmoja anauzwa shillingi ngapi?.

Wazungu wakati wa Christmass ni fahari kubwa sana kwao kuchinja Turkey.

Nimefanya utafiti sijakurupuka kuuliza wadau ukiwa na hivi nilivouliza soko lake sio mitaani ni mahoteli makubwa makubwa tena wanakufuata wenyewe.

Hivi vitu viko Supermarket tu kama unataka nyama yake.Sasa nikuambie kitu kingine huwezi amini je unajua Sungura ni dili moja kubwa sana mpaka mkojo wake unauzwa?

Nenda Kenya Nairobi ndio utajua.Hata hivyo mkuu watu wengine mtu mwingine anaamua kufuga kitu just for funny and hobby kama mapambo tu.

Hata hivyo nashukuru kwa changamoto kukubali kukosolewa ni jambo zuri
Moja ya mambo yanayo cost Watanzania ni kufanya vitu kwa mapenzi binafisi.

Mkuu unatakiwa kujiuliza je hao ndege hapo juu utakuwa unatatua kero ipi moja wapo?

Je pita pita zako usha kutana nao wakiuzwa sokoni? kama sio kwa nini?

Je mtaani kwako ukifanya sensa ya walio kula Bata mwaka huu utapata watu? make unaweza usipate na hata ukaambia huwa sili.

Hizo tajwa hapo juu watu hawana utamadunia naza, sawa wanaliwa ila utamaduni hakuna,

Wewe ukifuga hao na mwenzako akafuga kuku wa layers ar Broiler hutakaa ushindane yaye.

Na ukiona mteja anakuja kununua kwako basi jua anaenda kufuga na yeye sio anaenda kuchinja.

Hizo ndege ziko line moja ba Kware, Sungura, watu hawana utamaduni navyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msimu wa kanga kutaga ni upi na dalili zao za kuanza kutaga n zipi?
Mkuu sijajua kama sehemu zote msimu wa kutaga huwa ni mmoja ila kwa sehemu nilipo Kanga hutaga kuanzia mwezi wa 11 na dalili za kanga kutaga mara nyingi huwa naona dume kunamlio fulani huwa analia na huwa anafatana sana jike hadi kwenye kutaga dume linamfuata jike.
 
Ahsante mkuu kwa shule nzuri tutafutane basi
Mkuu tuko pamoja anza kuwafuga hao kanga tafuta na ule waya wa fensi ya kuku zungusha sehemu ya kuwaweka washinde wape chakula,maji na mboga za majani mchanganyiko hasa makabegi hapo kwenye kuzungusha fensi itakusaidia wasipotee na kuliwa na mbwa vilevile unaweza kuwachanganya na kuku,bata wa aina zote na wakaishi pamoja vizuri na baadaye utakuja kutupa mlejesho hapa jinsi watu watakavyokuwa wanawahitaji.

NB,mimi nilianza na kuku mambo yakaenda vizuri nikawachanganya na bata wa kienyeji mambo yakaenda vizuri nikawatupia na kanga mambo yameenda vizuri sasa hivi ndio natafuta vifaranga wa bata mzinga na najua nitafanikiwa tu hivi karibuni nilileta uzi hapa ili nipate maujuzi ya kufuga bata mzinga lakini uzi haukupata wachangiaji huu hapaPata ushauri, michango na mawazo ya ufugaji wa bata mzinga kibiashara.
 
Huyo babata mzinga ni yupi na huyo bata bikini ni yupi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu jovin607 angalia hizo picha 3 ya kwanza ni bata mzinga ya pili ni bata bikini ya tatu ni kanga ,bata mzinga anaitwa turkey bata bikini anaitwa goose kanga anaitwa Guinea fowl.Bata bikini ana tabia akitembea anaangalia juu.Sasa uzuri wa bata bikini ni mlinzi wa nyumbani mchana kama mbwa wawapo bandani au nje akiingia mtu mgeni hawajui wanapiga makelele sana na kama wako nje wanamfukuza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu mimi naomba nishare some information.Mimi nafuga bata bukini now ni mwaka wangu wa kumi na moja+ nikiwa na akili zangu timamu hawa bata ni wazuri na hawana complication na siyo gharama kuwafuga. life span ya bata mmoja ni miaka 25 na hawana magonjwa wala nini wewe ni kuwapa chakula tu.karibuni wako pia naowauza kwa mmoja ni 150,000 na utapata maelezo mazuri zaidi
 
Wakuu mimi naomba nishare some information.Mimi nafuga bata bukini now ni mwaka wangu wa kumi na moja+ nikiwa na akili zangu timamu hawa bata ni wazuri na hawana complication na siyo gharama kuwafuga. life span ya bata mmoja ni miaka 25 na hawana magonjwa wala nini wewe ni kuwapa chakula tu.karibuni wako pia naowauza kwa mmoja ni 150,000 na utapata maelezo mazuri zaidi
Nitakupataje maana nataka ukinipa unipe jike na dume ila nilikuwa sijui kuwa wana bei kubwa kihivyo.Je hawa bata wanahitaji maji maji yaani kuchezea maji kama hawa bata wa kawaida yaani kuwatengenezea kabwawa?
 
Mkuu hebu soma juu alivoandika prof Ndumilakuwili.Tembea uone mengi mkuu kama hujatambea duniani huwezi jua kwanini nimeuliza swali hili.Nenda mahoteli makubwa ya kitalii agiza nyama inaitwa Turkey(Bata mzinga) kisha uniambie ni shs ngapi.Bata mzinga mmoja mkubwa sana bei yake ni shs laki mbili je kuku wa mitaani wa wakaanga chips mmoja anauzwa shillingi ngapi?.Wazungu wakati wa Christmass ni fahari kubwa sana kwao kuchinja Turkey.Nimefanya utafiti sijakurupuka kuuliza wadau ukiwa na hivi nilivouliza soko lake sio mitaani ni mahoteli makubwa makubwa tena wanakufuata wenyewe.Hivi vitu viko Supermarket tu kama unataka nyama yake.Sasa nikuambie kitu kingine huwezi amini je unajua Sungura ni dili moja kubwa sana mpaka mkojo wake unauzwa? Nenda Kenya Nairobi ndio utajua.Hata hivyo mkuu watu wengine mtu mwingine anaamua kufuga kitu just for funny and hobby kama mapambo tu.Hata hivyo nashukuru kwa changamoto kukubali kukosolewa ni jambo zuri
Hizo hoteli ziko ngapi?
 
Nitakupataje maana nataka ukinipa unipe jike na dume ila nilikuwa sijui kuwa wana bei kubwa kihivyo.Je hawa bata wanahitaji maji maji yaani kuchezea maji kama hawa bata wa kawaida yaani kuwatengenezea kabwawa?
mkuu nitumie number yako ,Hawa bata hawahitaji maji bata wanaohitaji maji ni perkin na siyo bukini.bukini wanahitaji maji kidogo ya kuwasiadia wakati wa kula
 
Samahani wapendwa wangu naomba mnielimishe kanga ana uwezo wa out against mayai mangapi na je ana uwezo wa kutotoa? au Hana?
 
Kanga kwanza anataga kwa kuhama hama kama unamfuga nyumbani kama porini sawa anataga sehemu moja,lakini ukipata mayai yake anayotaga unamchanganyishia kwenye kuku wa kienyeji anatotoa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom