BUSHMEN 88
Member
- Sep 3, 2022
- 25
- 31
Habarini wanajukwaa natumai ni wazima wa afya tele na pia natanguliza shukrani zangu kwenu.
Nimeanzisha mradi wa ufugaji wa sungura ili niweze kukuza kipato na kupambana na changamoto za maisha baada ya kuona ugumu wa maisha kila kukicha kheri ya jana. Hivyo basi niliamua kuanza kufuga na sungura kumi lakini nilifanikiwa kuanza na sungura watano kulingana na mtaji nilikuwa nao wa shilingi laki moja yani nilinunua majike manne na dume moja.
Mradi huu yapata miezi miwili na nusu mpaka sasa hivi lakini sungura majike watatu wamefanikiwa kuzaa jumla ya watoto ishirini na moja yani uwiano wa kila mmoja kuzaa watoto saba.
Sasa naomba nielimishwe nifanyaje ili niweze kuwanusuru kutunza vizuri watoto wasipate na magonjwa, kufa ukizingatia mimi ndio mara ya kwanza naanza kufuga sungura naombeni mchango wenu na ushauri wadau na watalaamu wa ufugaji wasungura.
Ahsanteni.