Ufufuko wa CCM kupitia Mwenezi Makonda

Ambros Kiwale

Member
Oct 30, 2023
27
44
Habari wataalamu, binafsi sio mtaalamu Sana wa siasa, hata hivyo nakiri kwamba tangu nimeanza kufuatilia fuatilia politics ninashawishika kwamba CCM imeanza kurudisha uhai wake kupitia MWENEZI P. MAKONDA.

Kwa ujumla Kama Kuna washauri wa Rais humu, wamjulishe kuwa wamefanikiwa Sana kuifanya CCM kuwa "talk of the Town" kwa Sasa, ndani ya muda mfupi tangu MAKONDA kushika nafasi mojawapo nyeti ya CCM amedhihirisha utaalamu katika eneo la political propaganda na kuteka umma wa watanzania kumjadili na kukijadili chama Cha mapinduzi zaidi kuliko issues nyinginezo.

Hata hivyo binafsi nashauri, mheshimiwa Rais SSH, ashughulikie kwa nguvu miradi ya kimkakati ambayo mtangulizi wake aliicha hususani suala la SGR na bwawa la Mwl. Nyerere.

Aidha kwa jicho langu binafsi naona turn off nyingine kwake ni kukawia kuchukua hatua ama maamuzi magumu dhidi ya wanaotajwa kuhusika na ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma hususani ambao taarifa ya CAG imebainisha.

Nahitimisha kwa kukazia tu kwamba Kuna haja kwake ku harmonize atmosphere ya kisiasa ambayo kwa Sasa kupitia MWENEZI, heshima ya chama inarejea na utekelezaji wa miradi mbalimbali hususani ya kimkakati ambayo kutokukamilika kwake kwa muda inaibua hoja.

#istandtobecorrected
 
SGR na bwawa la nyenyere ni vitu ambavyo viko juu ya uwezo wa ccm. Hi miradi aliiweza Magufuri tu ila Hawa wengine tusuburi neema tu ya Mungu
 
SGR na bwawa la nyenyere ni vitu ambavyo viko juu ya uwezo wa ccm. Hi miradi aliiweza Magufuri tu ila Hawa wengine tusuburi neema tu ya Mungu
suala la kumalizia miradi ya kimkakati ndilo litakaloleta shida kubwa,maisha kupanda na watu wa chini kutopata attention ya kutosha. Ubadhirifu ulioshamiri na rushwa CCM waviangalie sana.
 
suala la kumalizia miradi ya kimkakati ndilo litakaloleta shida kubwa,maisha kupanda na watu wa chini kutopata attention ya kutosha. Ubadhirifu ulioshamiri na rushwa CCM waviangalie sana.
Natamani ikulu wangekua na page hapa wapate MAONI yetu moja kwa moja
 
Back
Top Bottom