MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,016
- 16,811
Huyu dada kadri siku zinavyoenda nashindwa kumuelewa kwani tokea Lowassa ahamie CHADEMA/UKAWA kila anapokuwa anatangaza habari inayohusu tu CHADEMA/UKAWA huwa anakuwa na furaha ambayo hata huwa anashindwa kuificha, lakini Ufo Saro huyu huyu akiwa anatangaza tu taarifa ya kuhusu chama kizuri, cha Mungu, kitakatifu, bora na chenye mafanikio makubwa ndani na nje ya Tanzania cha CCM huyu dada tena bila hata ya aibu huwa anakunja sana sura yake na hata " tonation " yake huwa ni ya kukasirika na ni kama analazimishwa tu kusoma taarifa za CCM.
Kwenu uongozi wa ITV hebu lifuatilieni hili na mlifanyie kazi vinginevyo huyu binti atawaharibieni kabisa kituo chenu na hatimaye tutajua kuwa pengine anatumika. Halafu na nyie CHADEMA
/UKAWA, kwanini msianzishe tu vituo vyenu vya habari ili mtuondolee hawa waandishi wenye kuacha maadili ya kazi zao na kuweka ushabiki? Kama mtakuwa hamna hela ya mtaji wa kuanzisha hivyo vituo tafadhalini njooni CCM na tutawapeni kama siyo kuwakopesheni na mtaturudishia taratibu tu.
Ufo Saro badilika dada au kama vipi chepuka basi huko CHADEMA/UKAWA ili tujue moja.
Tuvumiliane tu kwa sasa.