Ufisadi waivuruga ngome ya Dk. Slaa

Ufisadi waivuruga ngome ya Dk. Slaa

Serikal ya ccm ndiyo inayoshika dola kama inaona halmashauri ya karatu kuna watu mafisadi si iwapeleke mahakamani,kama serikali inalalamika tu bila kuchukua hatua nani atachukua hatua sasa?
 
Very cheap politics...kwan huo mfuko wa jimbo ...cunakaguliwa ..wamfikishe Mahakaman...na pia wananchi waseme tatizo ccm wanahofu na Lissu pamoja na dr.slaa
 
Aliweka nyaraka kuthibitisha tuhuma zake kama wanavyofanya wanaoituhumu serikali sikivu ya CCM? Au maneno yake matupu yatosha?

kweli nimeamini kupenda ni ugonjwa tena ni ugonjwa mbaya sana, waweza penda chongo ukasema kengeza
 
Hahahaaaaaa hii wiki mnamwandama Dr wa ukweli Slaa hii ni uzi takribani wa nne wiki hii mmemuandama Slaa,poleni sana na bado mtaanzisha mada nyingi lakini zote zimeshachuja njooni na single nyingine magamba.
 
tunahitaji mapinduzi yatakayofanywa na wananchi sasa,,, maana naona hivi vyama sasa kunayanayoendelea nyuma ya pazia halafu kumbe mnaonekana mnajuana......... WATANZANIA WENZANGU NI WAKATI SASA WA KUINGIA BARABRANI NA KULIOMBA JESHI LISHIKE NCHI WALAU KWA MIAKA 20 KWANZA TUONGOZWE NA MAGENERAL KWANZA WAWANYOOSHE HAWA WATANZANIA KWANZA NA KURUDISHI HESHIMA KWA BINADAMU AMBAYO HAPA KWETU IMEPOTEA..... BUNGE MUHIMU LA BAJETI VITI HAVINA WATU, WALIOPO BAADALA YA KUUJADILI HOJA NI FULL MIPASHO.... yaani hatuna direction si upinzani wala watawala...
 
Kama ccm inaona watu wa aina hii na wakina Lusinde ndio watetezi wao basi kwa kweli "wamechoka" hivi sii ndio wanazidi kuonyesha jinsi serikali yao ilivyochoka? Kwa nini hayo asemayo kama wanayajua wasichukue hatua?
 
two wrongs cannot justify a misconduct!!
Dr. Slaa na Lisu kuwa wezi si kigezo cha ccm kukwiba pesa za umma!
By the way Tuambieni ruzuku ya ccm inatumika vipi maana angalau tunawaona chadema wanafanya maandamano na mikutano ya hadhara!
 
Data zenyewe umezitoa kwa Mary Chatanda, si bora hata zingekuwa zimetoka kwa taahira Lusinde.
 
Nani aamini huo uharo wa huyo Chatanda? maccm yameshikwa pabaya na sasa yanatapayapa kwa vijituhuma vya kuokoteza
 
Kama Lissu na Slaa ni mafisadi, kwa nini policcm na pcbccm haichukui hatua? Yaani Lissu aibe ccm na Vyombo vyake visimkamate? hats chekechea hawezi kudanganyika
 
Mleta mada kama ni Chatanda mwenyewe au kama ni msukule wake tumekusikia kama ni kweli viongozi wa CHADEMA wamefanya ufisadi mkubwa kiasi hiki tena kwa kufisadi mali ya wananchi sijui mpaka sasa bado mnasubiri nini kuwapeleka Mahakamani.

Ndiyo hapo Lissu akiwaambia kuwa ni wachovu mnaanza kulialia, mnalialia nini wakati mali ya wananchi inaliwa?mnakimbilia majukwaani kulialia badala ya kuwapeleka wahalifu Mahakamani au siku hizi sheria mmehamishia kwenye majukwaa?na kulialia bungeni?.

CHADEMA hamtaweza kuisambaratisha kwa mbinu hii,kama ni kuvunja ngome ya CHADEMA kwa mbinu hii hamtaweza,kama ni hivyo basi CCM ndiyo itakuwa ya kwanza kuvunjika kwa kuwa viongozi wake ndio waliofanya ufisadi wa kweli unaoigusa nchi nzima ambayo kila mahali ni ngome ya CCM.
 
Halmashauri mnaifanyia ufisadi tukiwapa nchi si si itakuwa balaa kabisa.
 
kweli nimeamini kupenda ni ugonjwa tena ni ugonjwa mbaya sana, waweza penda chongo ukasema kengeza

Kuwa na kawaida ya kujibu hoja maana unaweza kuniambia kitu ambacho sikijui nikaelimika hata kama sitokwambia, mipasho hulitendei haki jukwaa letu adhimu
 
KINYUME cha taswira ya miaka mingi kwamba Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia viongozi wake wakuu, hasa Katibu Mkuu, Dk. Wilbroad Slaa, ni chama kinachopinga ufisadi, mambo yameripotiwa kugeuka katika baadhi ya ngome za chama hicho nchini.

Kwa muda mrefu sasa, Dk. Slaa amekuwa akijipambanua kuwa kinara wa kupinga ufisadi na akiwa Mbunge wa Karatu hadi kufikia mwaka 2010, amekwishafanya kazi ya kufichua uozo mkubwa uliopata kufanywa na watendaji wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), lakini sasa Halmashauri ya Karatu inayoongozwa na chama hicho imekubwa na kashfa za ufisadi.

Hali hiyo ilibainishwa bungeni mjini Dodoma jana na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mary Chatanda, ambaye aliweka bayana kwamba si tu Halmashauri ya Karatu ambayo ni ngome ya kisiasa ya Dk. Slaa, imeoza kwa ufisadi bali hali pia hali ni hiyo hiyo kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, akisema mbunge huyo ‘ametafuna’ kifisadi fedha za maendeleo ya mfuko wa jimbo.

Akichangia mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) jana bungeni mjini Dodoma, Chatanda alidai hakuna mbunge fisadi kama Lissu katika kutafuna fedha za mfuko wa jimbo.

“Nawashangaa hawa wapinzani wanapiga kelele hapa kuhusu ufisadi wakati ndio wanaoongoza kwa ufisadi. Hakuna mbunge ambaye anatafuna fedha za mfuko wa jimbo kama Lissu, tunaomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akamfanyie ukaguzi maalumu,”alisema Chatanda

Alisema wapinzani wamekuwa wakipiga kelele kukemea mafisadi na kudai kwamba CCM ndio wanaofanya ufisadi wakati Halmashauri ya Karatu inayoongoza na Chadema ndiyo kinara katika kuendeshwa kwa ufisadi uliopindukia.

“Halmashauri ya Karatu ambayo ni ya Chadema ndiyo fisadi kuliko, kuna mbunge wa upinzani, Cecilia Pareso, nilimuuliza kuhusu yule fisadi ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ya Karatu, kwamba amechukuliwa hatua gani akanijibu…yule hatagombea tena au hatapita,”

“Kwa hiyo wao wanapiga kelele za nini hapa ndani (bungeni) wakati maeneo machache tu wanayoongoza wananuka ufisadi? Wakipewa nchi itakuwaje?,” alihoji Chatanda ambaye amewahi kuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha na kwa sasa ni Katibu wa CCM, mkoani Singida.

Akizungumzia kauli iliyotolewa na baadhi ya wabunge wa Chadema kwamba Mbunge wa Viti Maalumu wa Chama hicho, Rose Kamili, alipigwa na kusababishiwa ulemavu na baadhi ya wanaCCM alisema huo ni uongo uliokithiri, akisistiza kwamba mbunge huyo alipata ajali kabla ya kwenda kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga.

“Wapinzani mkiwa hamna hoja ni vyema mkanyamaza kuliko kuongea uongo, Kamili ni rafiki yangu siku nyingi lile tatizo la mkono alilonalo hakusababishiwa na CCM bali alipata ajali na hata kipindi akiwa anataka kwenda kwenye kampeni nilimuuliza kuhusu mkono wake uliokuwa umepachikwa chuma, akajibu kwamba hawezi kuacha kwenda kwenye kampeni chama chake kitamuelewa vibaya,”


“Yaliyotokea Kalenga kipindi kile siyo yaliyomfanya Kamili kuumia mkono bali alikuwa tayari ana chuma kwenye bega hivyo alitoneshwa kidonda, acheni kuudanganya umma kwamba CCM imeumiza mtu. Hakuna kitu kama hicho,” alisema Chatanda.

Hata hivyo kauli hiyo ilimfanya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, kuomba kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mussa Azzan Zungu, ambapo alisema wakati tukio hilo likitokea katika uchaguzi huo mdogo wa Kalenga alikuwapo na alishuhudia mbunge huyo akipigwa na kuumizwa na CCM.

Chanzo
: Raia Tanzania

Yaani unaquote mambo yanayoongelewa bungeni na kuyaleta huku, kwanza kanuni zao zinasema mtu hata akikutukana akiwa bungeni huwezi kumshitaki. Bungeni si ndiko wanakosema serikali ya chama cha mapinduzi imechoka na wala haijafanya lolote, je unayaamini hayo. Kule wanasema mengi kwa lengo la kuchafuana hasa wakati huu tukielekea uchaguzi mkuu. Kama huyo Chatanda ana uhakika na anayoyasema kwa nini basi haendi kuripoti polisi, Takukuru au hata kwa CAG. Tundu Lissu wanaccm wote hawampendi kama wakipata fursa ya kumshitaki hawatamwachia kwa sababu wanajua yule ni mwiba kwao. Kama kala pesa zote za mfuko wa jimbo ambazo kimsingi ni fedha za serikali kwa nini basi hapelekwi polisi. Porojo za kisiasa za bungeni ziacheni kule kule. Mh. Sugu alisema jana kuwa watu waume kwa wake huongopa lakini takwimu haziongopi. Haya huyo mbunge wako wa CCM na atuletee takwimu zilizofanyiwa utafika kama anazo, thubutu yake.
 
Itakua ajabu la dunia iwapo Slaa au lisu watafanya ufisadi kisha serikali ikawaacha tu.
 
Back
Top Bottom