Ufisadi wa wabunge katika biashara ya Nguzo za TANESCO

Tumeliwa kwa miaka mingi, sasa ukweli umethihirika. Naomba wote waliohusika kulihujumu taifa kupitia njia hiyo wafunguliwe mashtaka.

Isitoshe basi yule aliyekua akionekana Mbunge machachari, mtetezi wa wanyonge, kamanda na nyota ing'arayo upande wa upinzani , ndiyo muuza nguzo na mla rushwa mahiri ktk kadhia hii .
 
Mi nakuambia mkuu kwa wale wanaojua mirija ya kunyonya nchi hii wamekwishaiharibu. Kuna namna wenye mamlaka ya juu kabisa katika nchii hii kujisafisha na baadaye kuanza upya. Lakini vilevile kama njia hii inakuwa ngumu kuna njia mbadala. Mwaka 2015 hauko mbali. Bakora za kuwaondoa wanaoinyonya nchii hii ziko mikononi mwetu wananchi wenyewe

Mkuu usidhani nao watakaa tu kimya au hawajui athari watakazopata pindi wananchi wakifanya maamuzi magumu hiyo 2015. Ndio maana wanatumia kila njia, hila, mbinu - ziwe chafu au vinginevyo kuhakikisha hilo halitokei. Imagine hofu na propaganda za UDINI wanazopandikiza, propaganda za ukanda, ukabila, n.k. Hii yote ni kuhakikisha hilo halitokei kwa sababu "cha moto" watakiona.

Kama ni nchi ambayo dhamira ya kweli ingekuwa ni kujenga taifa lililo bora kwa ustawi wa wananchi wote kungekuwa na hofu ya nini CCM ikiwa madarakani? Au CUF? Au CHADEMA? NCCR? TLP? Lakini kwa kuwa tumechafuka na hatusafishiki tena ndio maana kila aina ya mbinu inatumika kwa usalama wetu, familia, na jamaa zetu.
 
tunaibiwa sana,na haya majibu na taarifa za jumla hayatusaidii,waziri anatakiwa awataje kwa majina wahusika then hatua thabiti ziweze kufuatia.otherwise tutaishia kuunda tume nyingine.Though its a gud start.
 
Hawa viongozi wetu ni waajabu sana.mafisadi wanawafahamu wezi wa mali za uma wanawafahamu.ni kitu gani kinacho wafanya wasiwachukulie hatua za kisheria?.
 
Prof. Muhongo amesema nguzo hizo zinatoka Mkoani Iringa zinaenda Mombasa halafu zinarudishwa Tanzania kwa jina la nguzo za South Africa!
Hili kweli shamba la bibi jamani!

Ni katika kukamilisha mzunguko wa pesa............kwani wabongo tunahusudu vitu vya nje. Wenye ubongo ndio wanakula nchi.
 
Ndiyo maana hawa wabunge vitu vingine hawajali wanajua mishiko iko kote kote Tanesco.....oilcom.....oryx etc etc etc tumekufa ufisadi umefikia hali mbaya sana wana JF tuchukue maamuzi magumu .
 
Kama na hii itakuwa ni siasa ya maji taka basi itabidi nifikirie upya namna gani Sumaye alikosa nafasi ya kuchaguliwa kuwa mgombea urais kupitia CCM mwaka 2005.
 
Ndiyo maana hawa wabunge vitu vingine hawajali wanajua mishiko iko kote kote Tanesco.....oilcom.....oryx etc etc etc tumekufa ufisadi umefikia hali mbaya sana wana JF tuchukue maamuzi magumu .
tuanzie kumpindisha yule bitoz wa bagamoyo.
 
sasa ndio naelewa kwa nini mheshimiwa rais hakumteua mbunge aliyekuwa ndani ya bunge kuwa waziri wa nishati na madini,badala yake alimteua mtu kuwa mbunge na kumpa uwaziri!
 
Back
Top Bottom