Ufisadi wa wabunge katika biashara ya Nguzo za TANESCO

GreenCity

JF-Expert Member
May 28, 2012
5,620
4,265
Waziri wa nishati na madini, prof. Muhongo ameweka wazi kuwa kuna wabunge wanaiuzia Tanesco nguzo na kwamba nguzo hizo zinatoka South Africa.

Prof. Muhongo amesema nguzo hizo zinatoka Mkoani Iringa zinaenda Mombasa halafu zinarudishwa Tanzania kwa jina la nguzo za South Africa!

Hili kweli shamba la bibi jamani!
 
Tumeliwa kwa miaka mingi, sasa ukweli umethihirika. Naomba wote waliohusika kulihujumu taifa kupitia njia hiyo wafunguliwe mashtaka.
 
Hizo nguzo za iringa si ndio za mtoto wa mkulu? Huyu rizmoko anatafuna nchi sana just imagine mti m1 wa mtiki uliokomaa unauzwa hadi million1 lkn hv vimiti vya miaka mi3 wanauza hadi 1.5m daaa riz1 tuaaacheeeeeeee!
 
DUH Aiseee kweli bongo ni shamba la bibi watu wanaiba bwana khaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Aliyekuwa akihusika na uuzaji wa hizo nguzo kwa upande wa Wabunge alikuwa Rostam sasa ameisha ng'atuka aliyebaki ni Riz 1 huyu waziri asije akawa anataka kupotosha umma na kutuchanganya atutajie majina ya hao wabunge ndo tutamuamini la sivyo ni uongooooooooooooooooooooo!
 
Duu kali kweli kweli, kwa mwenye data wabunge wanaofanya biashara na tanesco atuwekee hapa. jamaa yuko hash akiendelea hivyo labda ........
 
Waziri wa nishati na madini, prof. Muhongo ameweka wazi kuwa kuna wabunge wanaiuzia Tanesco nguzo na kwamba nguzo hizo zinatoka South Africa.

Prof. Muhongo amesema nguzo hizo zinatoka Mkoani Iringa zinaenda Mombasa halafu zinarudishwa Tanzania kwa jina la nguzo za South Africa!

Hili kweli shamba la bibi jamani!

Si hayo tu, amesema pia anayo listi ya majina ya Wabunge wote Wanakamati wanaoisimamia TANESCO ambao wana makampuni yanafanya biashara na TANESCO na hivyo kuwa na mgogoro wa kimaslahi na kushindwa kuisimamia.

Amesema pia kuwa wamemwomba CAG afanye ukaguzi na hivyo hakuna haja ya kuunda tume.

Badala ya kuunda tume, amesema kila kutakapokuwa na jambo au scandal, watendaji watawajibika kutoa report ambayo itasikilizwa katika Public hearing.
 
Waziri wa nishati na madini, prof. Muhongo ameweka wazi kuwa kuna wabunge wanaiuzia Tanesco nguzo na kwamba nguzo hizo zinatoka South Africa.

Prof. Muhongo amesema nguzo hizo zinatoka Mkoani Iringa zinaenda Mombasa halafu zinarudishwa Tanzania kwa jina la nguzo za South Africa!

Hili kweli shamba la bibi jamani!

Ati nini? Tunajikaanga kwa mafuta yetu wenyewe? Wakenya pia wanatuhujumu?
 
Hao ni wezi wachache kwenye manguzo ya Iringa! Awataje na wanaoiuzia Tanesco Mafuta ya kuendeshea mitambo! Ni mult million project ya wajanja!
 
Waziri wa nishati na madini, prof. Muhongo ameweka wazi kuwa kuna wabunge wanaiuzia Tanesco nguzo na kwamba nguzo hizo zinatoka South Africa.

Prof. Muhongo amesema nguzo hizo zinatoka Mkoani Iringa zinaenda Mombasa halafu zinarudishwa Tanzania kwa jina la nguzo za South Africa!

Hili kweli shamba la bibi jamani!

wapo tayari kupitisha mkataba wa NSSF Wa kijinga maana wanauhakika wa kutokea TANESCO
 
Aliyekuwa akihusika na uuzaji wa hizo nguzo kwa upande wa Wabunge alikuwa Rostam sasa ameisha ng'atuka aliyebaki ni Riz 1 huyu waziri asije akawa anataka kupotosha umma na kutuchanganya atutajie majina ya hao wabunge ndo tutamuamini la sivyo ni uongooooooooooooooooooooo!

Muangalie vizuri huyo Prof kaka...yuko njema academically na hata kwenye uwaziri. Ni suala la muda tu
 
Hao ni wezi wachache kwenye manguzo ya Iringa! Awataje na wanaoiuzia Tanesco Mafuta ya kuendeshea mitambo! Ni mult million project ya wajanja!

Issue nzito iko hapa! Mambo ya Eng. Mhando ni vijimambo vidogo tu! Umeona jinsi Mama speaker, alivyokwepesha issue?
 
Back
Top Bottom