Ufisadi wa waandishi wa habari kilimanjaro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi wa waandishi wa habari kilimanjaro

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by STINGER, Jan 15, 2012.

 1. S

  STINGER Member

  #1
  Jan 15, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  1. Mbunge wa rombo joseph selasini, juzi alimfunga paka kengele kuelezea jinsi baadhi ya wanahabari wa mkoa huo wanavyowanyanyasa wadau wao ili wapewe kitu kidogo. Habari hiyo imechelewa sana ila tunamshukuru haswa kwa vile ni mbunge wa jimbo ninalotoka.

  Pamoja na mambo mengine mbunge selasini amefungua mjadala ambao hauna budi kujadiliwa na jamii kwa ujumla kutokana na tasnia ya habari kuwa moja ya sekta muhimu katika jamii.

  Ni kwa sababu hiyo basi ndiyo sababu ya mimi na wenzangu tuliamua kufuatilia jambo hilo kwa undani zaidi kwa kuwasiliana na wadau wengine walioko huko mkoa wa kilimanjaro kujua kulikoni na ni ushauri gani tutoe.

  Katika kufuatilia kwanza kabisa tuligundua ya kuwa pamoja na kutokuwataja waandishi hao, sisi tulipata taarifa za majina yao nao ni gift mongi wa majira, venace maleli wa moshi fm na ambae hujitambulisha kuwa ni mwandishi wa mwananchi na rodrick mushi wa tanzania daima.


  ukiomuondoa maleli ambae namjua sana, hao wawili siwajui kabisa pengine kwa vile ni wageni kama tulivyojulishwa.

  Taarifa za ziada nikuwa mbunge alishalalamika mpaka klabu ya waandishi kilimanjaro bila kupata ufumbuzi wowote hivyo kuamua kumwaga mambo hadharani kwenye rcc hivi karibuni huku akiweka wazi ushahidi alionao kuhusiana na sakata hilo.

  Katika uchunguzi wet wetu wa ziada ni kuwa hata baadhi ya wahariri walipewa taarifa hizo na ushahidi wake lakini hakuna hatua zimechukuliwa hadi sasa.

  Hata klabu ya waandishi n ayo haijachukuwa hatua zozote hata za kuwahoji watuhumiwa hao. Inasikitisha haswa kwa vile watu wengi wamekuwa wakilalamika kuhusiana na tabia hizi mbaya za waandishi kutishia wadau ili wapewe pesa.

  Tuhuma hizi napenda niliunganishe na zingine ambazo zinawahusu baadhi ya viongozi wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa kilimanjaro, ambao ni makamu mwenyekiti rodrick makundi, katibu msaidizi nakajumo james na mweka hazina msaidizi rodrick mushi, ambae pia anatuhumiwa kwenye lile la kwanza.

  Viongozi hawa wanadaiwa kutumia huruma ya mkuu wa mkoa wa kilimanjaro ya kuwapa upendeleo katika ugawaji wa sukari kwa manufaa yao wenyewe kwa kufanya biashara ya kuuza sukari hiyo kwa kutumia jina la klabu tena kwa wakenya huku wakishirikiana na baadhi ya waofisa wa kncu.

  Cha kujiuliza hapa ni kama viongozi hawa wataweza kuwajadili watu ambao wanadaiwa kuwanyanyasa wadau wa habari.

  Kwa kweli hapa kunahitajika busara ya hali ya juu ili kuinusuru tasnia ya habari na tuhuma hizi nzito.


  2. Pia kuna tuhuma kuwa maleli alitumiwa na wafanyabiashara kadhaa wa wilaya ya rombo ili kumchafua mkuu wa wilaya hiyo ambapo walichangisha shilingi milioni 3 na kumuita mtangazaji wa itv renatus mtabuzi, ambae alitengeneza kipindi maalum cha kumchafua dc wa rombo ili aonekane mbaya wakati hali halisi ni ukakamavu wake kupinga magendo.

  Mutabuzi alipewa shilingi milioni 1.5, mbalikulipiwa malazi, chakula na vinywaji na mmoja wa mafisadi hao wakati akiwa wilaya ya rombo kwa kazi hiyo isiyo na nia njema kwa utawala bora. Kuna taarifa pia mutabuzi alipewa tiketi ya ndege urudi dar es salaam baada ya kudai wakubwa zake wanangojea taarifa yake hiyo kwa hamu kubwa.

  Maleli katika sakata hili amesikika akisema kuwa amepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa afisa usalama wa wilaya ya moshi kwa vile wa rombo alimnyima ushirikiano.
   
Loading...