Ufisadi wa Rostam kuzimwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi wa Rostam kuzimwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Apr 3, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,591
  Trophy Points: 280
  Furaha ya Rostam kuzimwa?


  [​IMG]
  Na Jabir Idrissa - Imechapwa 30 March 2011

  [​IMG][​IMG] [​IMG]


  SHIRIKA la umeme la taifa (TANESCO) limetupa kete muhimu likilenga kusimamisha ulipaji tozo ya Sh. 94 bilioni kwa mbunge wa Igunga na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC-CCM), Rostam Aziz kupitia kampuni ya Dowans Holdings SA, MwanaHALISI limeelezwa.

  Kwa mujibu wa nyaraka ambazo gazeti hili limezipata, TANESCO wamewasilisha mahakama kuu mjini Dar es Salaam, hoja sita kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya biashara (ICC) iliyoipa Dowans tozo ya mabilioni hayo ya shilingi.

  Katika maelezo yake ambayo gazeti hili limeyaona, TANESCO kupitia jopo la mawakili wanaoongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, inataka mahakama hiyo itengue tozo hiyo kwa kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni za uadilifu na ukweli.

  Wanasheria wa TANESCO wanasema, “Jopo la wasuluhishi lilijipa mamlaka isivyo halali au lilitumia vibaya mamlaka yake, kwa kutumia sheria ya Texas nchini Marekani kuonyesha uhalali wa kuwepo kwa Richmond.”

  Jopo la mawakili wa TANESCO linaundwa na Masaju (kiongozi), Prof. Florence Lwoga, Dk. Angelo Mapunda, Dk. Alex Nguluma na wakili Mwandambo.
  Mawakili hao wanaeleza kwamba majaji wa ICC walitafsiri kinyume cha haki, sheria ya manunuzi ya umma ya Tanzania (PPRA) ya mwaka 2004 inayoelekeza kuwa mlipaji wa huduma ndiye anayepaswa kushiriki katika vikao vya majadiliano kabla ya zabuni kutolewa.

  Wanadai kwamba wasuluhishi walipuuza, kwa makusudi, ushahidi wa TANESCO kuwa ilikuwa ni kinyume cha sheria ya PPRA kuidhinisha kusainiwa kwa mkataba bila kwanza kufuatwa utaratibu wa kutangazwa zabuni ya kukaribisha waombaji; hasa kwa kuwa zabuni ya awali ilifutwa na bodi ya zabuni ya TANESCO.

  TANESCO wanadai kuwa Wizara ya Nishati na Madini au Kamati ya Majadiliano iliyoundwa na serikali, haikuwa na uwezo wowote wa kisheria kuidhinisha mkataba kati yake na Richmond na baadaye Dowans.

  Gazeti hili linaweza kuthibitisha kuwa kamati ya majadiliano ya serikali ambayo ndiyo iliyosimamia mkataba unaobishaniwa mahakamani, iliundwa kwa shinikizo la waziri mkuu aliyejiuzulu mwaka 2008 kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa.
  Mawakili wa TANESCO wanajenga hoja katika kupinga uamuzi wa ICC kuwa mahakama hiyo ilikosea kisheria kwa kutozingatia nyaraka kadhaa likiwamo tangazo la zabuni Na. PC010/2006, jambo ambalo limesababisha kufikiwa kwa makubaliano yaliyokiuka vigezo vilivyobainishwa katika zabuni hiyo.

  Vilevile, mawakili wanaeleza kwamba haikuwa sahihi mrufani (TANESCO) kulazimishwa kusaini makubaliano na Richmond Development Company (LLC) yaliyojadiliwa na kampuni ya Texas ambayo haikuwa na uzoefu wa kutekeleza mradi wala uwezo kifedha.

  Mawakili wanadai msimamo huo wa TANESCO unazingatia ukweli kwamba katika zabuni iliyotangazwa na baadaye kufutwa, ilielekezwa kwamba kabla ya kufikiwa kwa makubaliano ya kuidhinisha mkataba, sharti mambo kadhaa yazingatiwe.
  Mambo ambayo walitaka yazingatiwe ni ufungaji wa mitambo na muda kuanza kwa utoaji wa huduma, muda wenyewe wa kutolewa huduma, gharama za awali, malipo ya ushuru wa forodha na kodi nyinginezo, malipo ya uendeshaji badala ya kutumia gesi iliyopo.

  TANESCO inadai wasuluhishi walikosea walipotafsiri vibaya sheria ya manunuzi ya umma na kushindwa kuona kwamba mrufani hakuwahi kutoa zabuni yoyote kwa Richmond Development Company (LLC) ambayo ndiyo ilisababisha kuingia kwa kampuni ya Dowans katika makubaliano.

  TANESCO wanadai pia kuwa wasuluhishi walijihusisha na ukiukwaji wa utaratibu kwa kushindwa kutafsiri sheria ya manunuzi juu ya katazo la kununua mitambo ya mitumba.

  “Matokeo yake, wasuluhishi walishindwa kuamua kwamba zabuni kwa Richmond (kama ilikuwepo) ilipatikana kinyume cha sheria za kimataifa zinazoelezea hoja ya kuzingatiwa kanuni za zabuni za huduma zinazohusu suala linalogusa usalama wa nchi.”

  TANESCO inadai kwamba wasuluhishi walipuuza ushahidi uliotolewa na mrufani kuhusu uwezo wa mkataba na kule kutotambua kwao sheria ya kutumika katika usuluhishi juu ya uhalali na kuwepo kwa Richmond Development Company (LLC).
  Mawakili wa TANESCO wanadai kuwa wasuluhishi walidharau ushahidi uliotolewa kuonyesha namna mrufani alivyojengewa mazingira ya nguvu ili tu asaini makubaliano na matokeo yake kulazimisha mrufani “kufikia makubaliano” na mrufaniwa.

  TANESCO inadai kwamba kwa kutozingatia ushahidi wa kutoshiriki kwa kampuni hiyo katika majadiliano, wasuluhishi wameonyesha upendeleo wa dhahiri na kuchukulia ukosefu huo kuwa ni sababu muhimu ya kutohusika kufikiwa kwa makubaliano.
  Aidha, wasuluhishi walishindwa kutambua ushahidi wa mrufani kwamba saini kwenye nyaraka zinazohusu utoaji zabuni, kuidhinisha kutolewa kwa huduma na kuhamisha mkataba kulikofanywa 14 Oktoba 2006, zinatofautiana na saini zilizopo kwenye mkataba.

  Mrufani anasimama katika hoja kwamba utolewaji wa tozo umefanywa kwa makosa kisheria; makosa yanayotokana na kupuuza kumbukumbu na kwamba wasuluhishi walikosea kisheria waliposhindwa kutambua ushahidi mzuri dhidi ya utolewaji wa mkataba wa kutoa huduma.

  Kwa hoja hizo basi, mawakili wa TANESCO wanasisitiza, “Tunataka tozo ibatilishwe na shauri lirudishwe kwa wasuluhishi kwa ajili ya kufikiriwa upya.”
  Mbali na TANESCO, wengine waliotinga mahakamani kupinga tozo hilo, ni Kituo cha Huduma za Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na wenzake wawili, akiwamo mwandishi wa habari, Timothy Alvin Kahoho.

  LHRC inawakilishwa mahakamani na Dk. Sengondo Mvungi wa Chuo Kikuu cha Dar ese Salaam wakati Kahoho anajiwakilisha mwenyewe.
  Kesi iliyotajwa mara ya kwanza 2 Machi, inatarajiwa kutajwa JUmatano ya 30 Machi 2011, mbele ya Jaji Emilia Mushi.

  Dowans iliyorithi mkataba wa kufua umeme kutoka kwa Richmond, imepata tozo hiyo baada ya kuonekana kuwa TANESCO ilivunja mkataba nao. Dowans wamesajili hukumu hiyo kufuata utaratibu wa kutaka kukazwa kwa hukumu hiyo.
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  habari njema sana,ama ni mkakati dhid ya watanzania ama ni JK kuishiwa uvumilivu na EL camp
   
 3. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2011
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Go... Go... Tanesco... Go... Go.. Md mhando.... Go...go.... Mwenyekiti wa board!!!!
  Mambo yako wazi .. Tanesco for the country you can stop this shameful payment you were dragged on to pay by the gov't...nlifurahi majibu kwamba deni hilo halipaswi mkuwa kwenye mahesabu yenu..baali ya serikali..halafu serikali itabidi utueleze mnalipa kwa mkataba upi..yeeeba!
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Apr 3, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,595
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  BAK asante kwa taarifa, ila tumekuwa tukionya kuwa RA ni very smart any move should be careful checked and assessed.
  hao LHRC wanafanya nini?

  Japokuwa deni linaweza kuhama Tanesco na likahamia Serikalini still walipaji ni watanzania

  The best way ni kumfungulia kesi RA kesi ya uhujumu uchumi, issues ambazo wengi sijaona wakijaribu..ila wanajitokeza kipindi hali ikiwa mbaya.

  Pia je Tanesco wameishwahi kuwalipa Dowans malipo yoyote yale? hili nalo ni very questionable, tusijekuingia kwenye kesi nyingine ambayo watu wameishashindwa!

  By the way where are opposition parties mfano Tundu Lissu angekuwamo ingenoga kidogo.LHRC sikumbuki waliishampigania nani na wakashinda na kila siku kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu..RA asijepitia huko..angalizo tu
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,591
  Trophy Points: 280
  Ahsante Waberoya, lakini pia ukumbuke kwamba yule Mkullo alishatangaza kwamba Serikali haina pesa za kulipa hiyo tuzo ya shilingi 94 billioni. Na uthibitisho wa kauli hiyo ni barua mbui zilizoandikwa katika vipindi tofauti mwanzoni mwa mwaka huu na Serikali kwenda kwa nchi za wafadhili ili kuomba pesa za kuisaidia Serikali kujiendesha mpaka June 2011.

  Kwa maoni yangu pesa hii ambayo wale akina Ngeleja na Werema waliishupalia ilipwe haraka sana na haijalipwa hadi hii leo ni mafanikio yaliyotokana na kelele za Watanzania kuonyeshwa kutoridhishwa kwao na malipo haya ya kifisadi ambayo hayastahili kufanyika. Hivyo hata katika bajeti inayokuja kama hilo deni litahamishwa toka katika vitabu vya TANESCO na kuwekwa katika vitabu vya Serikali ili lilipwe bado naamini kabisa kama Watanzania tutasimama kwa nguvu zetu zote ndai na nje ya nchi yetu kupinga malipo hayo haramu basi naamini kabisa Serikali itaogopa kulipa malipo hayo haramu.
   
 6. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hapo penye nyekundu pana husika mkuu... under dutch au french law... kama washafanya malipo yoyote sidhani kama tutachomoka hata tufanye nini, sababu itakuwa inaonesha tulikuwa tuna mkataba nao by motive. Nina wasiwasi hawa jamaa kama walitumia english law ambayo sisi tunatumia kujitetea... Tuwe makini sana katika hili :bored:!!!
   
Loading...