Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 13,036
- 11,627
Mkuu Fundi Mchindo,
Naomba uniwie radhi mkuu kama nimekukwaza, hoja zako hapa ni muhimu sana mkuu, na ndio kwanza tulikuwa tumeanza kuchota elimu yako nzito, mkuu niko chini ya miguu yako usitumie hasira mkuu, tena, ninakuahidi mbele ya mashahidi wote hapa Jambo Forums kuwa sitarudia kukuingilia hoja zako mkuu. Usikwazike na mawazo finyu kama yangu mkuu, I know na nimekusikia mkuu nitajitahidi sana kujirekebisha mkuu, lakini please baki mkuu tusingependa Jambo Forums ife mkuu, unajua tena wewe ukitoka mkuu kwa hiyo please usikasirike mkuu, tumia busara!
Ahsante Mkuu.
Wako Mzee Wa Kumkoma Nyani: Super Emergency System, Haki ya mungu I love JF!
Kwa nini aunde kampuni nyingine wakati National Housing ipo? Na nani atakayetoa hiyo subsidy? Ukumbuke kuwa sio kila mfanya kazi wa serikali aliyestahili alikuwa na nyumba. Hata wakati huo, wengi tu walikuwa wakiishi mahotelini. Dawa ni badala ya kugombea hiki kidogo tulichoshindwa kukiendeleza, serikali ingefanya jitihada za kuweka mazingira ambamo watu binafsi, makampuni binafsi na vyombo vya umma vitaweza kujenga nyumba nyingi kwa ajili ya kupanga au kuuza.
Wakati umefika ambapo makazi bora iwe ni haki ya KILA mtanzania na si wafanyakazi wa serikali tu.
Haya na tuongee kisomi ingawa mimi huko simo. Mkuu naona unaishi Marekani. Je huko serikali inatoa huduma hii kwa wafanyakazi wake wote? Condoleeza anakaa katika nyumba ya serikali? Au uingereza? Brown kabla hajaukwaa uPM alikuwa anaishi katika nyumba ya serikali? Au Afrika kusini? Au nchi yeyote iliyoendelea? Wafanyakazi wa serkali wanapewa nyumba za kuishi bure na serikali kuu?
Suala la kutoa huduma hii halikuwa sustainable kwa jinsi lilivyokuwa likifanyika. In the long run huduma hii inatakiwa itolewe na soko la nyumba. Mfanyakazi alipwe vizuri na sokoni pawe na nyumba za kutosha zinazokidhi mahitaji yake kwa bei atakayomudu. Kwa sasa hivi hapa kwetu hilo soko halipo. Mahitaji yamezidi mno production kiasi cha kuwafanya wenye nyumba hizo kutoza pango wanavyotaka.
Serikali kwa muda mrefu ilikuwa haitoi fungu kwa ajili ya kuzikarabati wakati pango lilikuwa pegged kwenye mshahara wa mkazi. Mshahara wa wengi waliokuwa kwenye nyumba hizo ulikuwa kati ya 100,000 na 200,000. Hawa walikuwa wanalipa asilimia 10 ya mshahara kama pango hivyo kufanya pango kwa mwezi kuwa sh 10,000 hadi 20000. Hii pango ilikuwa haitoshi hata kunua kitasa na ilikuwa chini ya pango la chumba Mwananyamala chenye umeme! Serikali kwa hiyo ilitakiwa aidha iamue kusubsidise huduma kwenye nyumba hizi ( kitu ambacho katika soko hilo la huria halikubaliwi), kuongeza mshahara wafanyakazi wake wanaoishi katika nyumba hizo ili pango liwe linaloendana na mahitaji halisi ya uendeshaji, kupangisha nyumba hizo kwa wakaaji wake kwa market rates, kuziuza n.k. Uamuzi uliochukuliwa ni huo wa kuziuza. Taratibu za uuzaji wa mali ya serikali unasema mali hiyo itauzwa kwa mnada. Hivi hizo nnyumba zingeuzwa kwa mnada wamatengo wangapi wangeona ndani? Tukumbuke hatuzungumzii za Masaki tu bali hata zile za Chang'ombe! Matokeo yangekuwa kuwa nyumba hizi zimenunuliwa na wafanyabiashara na tukiwa zaidi, wafanyabiashara ambao wengi wao wangekuwa ni wahindi, waarabu au makaburu tungesema nini?
Huyo atakayeamua ku'nationalize' hizi nyumba tena itakuwa uamuzi wake na bila shaka atafanya hivyo baada ya kujiridhisha kuwa ni uamuzi utakaoangalia maslahi ya taifa letu. tulitaifisha nyumba kibao, tukaanzisha Msajili wa Nyumba, zikatushinda kuzihudumia hadi hapa tulipo ambapo tunazirudisha tena katika soko huria.
Kama ulivyosema Mkuu. tuliangalie hili suala kisomi na tuache ushabiki usio na kichwa wala miguu!
Ukisoma maandiko yangu utafahamu ya kwamba nilishasema ya kwamba, Dar es Salaam city planning haiwezi kusastain viongozi kutoka Mbagala na kuja kazini posta. US kwa bahati wana city planning and that help them a lot. Kiongozi anaweza kuja capital hill wakati anatokea Delaware, sio Dar es salaam.
Mkuu kama uoga ulikuwa ni wafanya biashara wenye cash supply kubwa wangeshinda bid, then serikali ilifanya analyisis gani kuona inapata maximu return kwenye ardhi inayo appriciate more than 15% annual? Na kama swala ni soko huria basi maana yake tunaangalia worth ya eneo, kisha tunaangalia how appriciate the area is, kisha tuna set price.Jee serikali ya Ben ilichukua mesure zote hizo?
Sasa ninaposikia ya kwamba nyumba imeuzwa kwa million 40 ndani ya masaki nakuwa devastated. Watu hao walionunua kwa 40 Million kisha wanawakodisha wafanya biashara wakubwa ambao wanajenga high rising condominium. Sasa who is a looser?
Kuangalia manufaa ya taifa means, wananchi wanabenefit at the same time serikali ina benefit. Sasa kama few people ndio waliokuwa serikali, then wakaset price, then wakanunua hizo nyumba. Swala linakuja where is check and balance? Kumbuka a lot of money ilitumika kufanya maintanance hizi nyumba wakati wa mzee Mwinyi, sasa uone kwamba kuziuza kwa bei ya chini ni kuwaibia tax payer?
I think the whole business ilikuwa full of corruption, the only way ni kuzirudisha then tuangalie utaratibu ambao wananchi wanatafaidika na serikali itafaidika. Na sio wakuu wa majeshi na mawaziri wachache kufaidika na serikali kuloose million of shilling.
hata kama kulikuwa na umuhimu wa kuuza nyumba za serikali, basi haikuwa zote. nyumba za mawaziri na makatibu wakuu zilikuwa katika hali nzuri tu. na isitoshe, wameuziwa katika bei isiyostahili kabisa
kuna watu waliuziwa nyumba oysterbay, ndani ya hicho kiwanja wameweza kujenga nyumba nyengine moja.
means wameuziwa viwanja viwili na jengo moja kwa bei ya kiwanja pekee. its such a shame
Kampuni inaundwa kusimamia utunzaji wa nyumba za serikali badala ya serikali kufanya hiyo kazi. Swali ni kuwa Kama mishahara haiwezi ongezwa kufikia hali ya soko kwa nini basi nyumba ziliuzwa?
1. Nia na madhumuni ya kuuza nyumba kwa wananchi na viongozi, ilikuwa ni njema kabisa.
2. Ttaizo limekuwa kwenye utekelezaji, Tanzania as a nation hatujawahi kuwa watekelezaji wazuri wa maazimio ya chama na serikali, kuaniza Azimio La Arusha, uhamishaji wa wananchi vijijini, peration maduka, hatujui utekelezaji.
3. Katika zoezi zima, kuna wananchi waliofadika as intended, na kuna viongozi pia waliofaidika, na kuna abuse zilizofanywa n viongozi na wananchi pia, lakini the abuse asilimia ni ndogo sana kuliko waliofaidika.
4. Kama inabidi, serikali zizipitie kesi moja baada ya nyingine za the abuse, na kuzirudisha na kuziuza kwa the originally intended,
5. Majuu katika maaamuzi ya serikali, siku zote huwa kuna projected risk effect, kwamba huu uamuzi utawaathiri na kuwafaidisha asilimia ngapi ya wananchi, ikionekana kuwa wengi wataathirika zoezi husitishwa, na wengi watafaidika basi hufanyika, kwa mfano FDA inataka kupitisha madawa mapya ni lazima ifahamishwe na wanaohusika wananchi wangapia wanaweza kufa bila sababu kwa kutumia dawa hizo mpya, wao hupima asilimia na kupitisha au kusitisha, sijui kama thta is the case na sisi bongo?
6. Mkuu wangu Fundi Mchundo, mimi ni mwanasiasa tena a very serious one, niko hapa JF kujadili taifa langu, na kujifunza kutoka kwa wengine, na kufundisha pia, nimekuwa kwenye huu mchezo wa bulogu kwa muda mrefu sana, nimeona wananchi wengi sana hapa, wakiingia na kutoka, ninaiheshimu sana michango yako, wewe unaweza kunitukana as much as you want kama ulivyokwisha fanya jana kwenye ile post yako, lakini mimi sina noma ndio cause and effect ya kuwepo hapa ili kuhesabiwa as I do, na ndio siasa hiyo ninayoipenda sana, kwa hiyo usiwe na wasi wasi ndugu yangu, wewe tundelee hapa kumkoma nyani na ni matumaini yangu kuwa utabadili uamuzi wako wa kutoka na kubaki, hapa uwanja wa Golani yaani Jambo Forums.
Ahsante Mkuu.
ES = Emergency Sysstem.
Tatizo watu hamtaki kuface ukweli . Viongozi wetu walikuwa wanajua nini wanafanya walipofikiria kuuza hizi nyumba . Ni jambo ambalo walishaliona miaka mitano iliyopita , kwa nini walisubiri mpaka karibu na mwisho wa term ya Mkapa ?
Nashindwa kuelewa sababu zinazotolewa na watu kujustify vitendo vya kizandiki vilivyofanywa . Zoezi zima lilikuwa tainted na usiri mkubwa , ni nani aliyesema kazi serikalini kitumike kama kigezo cha kununua hizo nyumba ? Vipi kuhusu wafanyakazi wengine wa serikali waliostaafu huko nyuma ?
Now let me touch the point kuhusu utekelezaji, kwa wasomi bongo it is about time sasa wanahitaji kuja na solution of why wabongo tunaweza sana kuyaendesha mashirika ya nje tukipewa kazi huko, lakini hatuwezi ya nyumbani? WHY?
I mean tizama our history, we have failed na utekelezaji wa everything tulichojiamulia as a nation, Azimio La Arusha, kuhamisha wananchi vijiji vya ujamaa, Elimu, operation maduka, haiwezekani maneno ya Mwalimu yakawa mazuri kwenye kusoma tu, why not kutekeleza? yaaani mapka siasa za vyama vingi zimetushinda, WHY?
Maneno mazito hayo mkuu FMES, napenda kuongezea neno moja tu hapo kwenye "utekelezaji wa everything positive tulichojiamulia as a nation..."
Wengine wamesha anza kuziuza,pamoja na kupewa masharti wasuize mpaka ifikie miaka 20.lakini wajanja wameanza kuwauzia wafanya biashara wakubwa eti anampangishia kwa miaka 20,
Kumbe tayari kesha chota nyumba wameuziwa na serikali mln 30 wanauza mln 500 masaki msasani nk
1. Wakuu kuuzwa kwa nyumba kumewasaidia wengi sana, kuliko hata mnavyofikiri au kuhisi, wafanyakazi wengi sana wa serikali na hata mawizara, wamefaidika sana ninaisema hii tena kwa uhakika sana kwa sababu I know a lot of people ambao ni wa hali ya chini walionufaika na hili zoezi.
2. Kuna mengi sikubaliani na Mkapa, lakini I am not so sorry kwamba kwenye hili la kuuza nyumba, ninakubaliana na Mkapa 100%, wakati akiongea kuhusu hiii ishu I looked in his face, na siasahau point moja muhimu aliyoisema, kuwa "...mimi Mkapa, nliamua kwa kuwajali wananchi na not anything else, and I stand for my decision....." I mean nimezoea viongozi wetu wakipiga hadithi, lakini this was a very serious tone kutoka kwa head of state taking responsibility.
3. Pia kuna masharti ninayoyaheshimu kwenye ununuaji, kwa mfano huwezi kuiuza for the next 25 years, na ukishindwa kulipia mortgage, nachukuliwa na serikali I like that ingawa najua sio rahisi.
Now let me touch the point kuhusu utekelezaji, kwa wasomi bongo it is about time sasa wanahitaji kuja na solution of why wabongo tunaweza sana kuyaendesha mashirika ya nje tukipewa kazi huko, lakini hatuwezi ya nyumbani? WHY?
I mean tizama our history, we have failed na utekelezaji wa everything tulichojiamulia as a nation, Azimio La Arusha, kuhamisha wananchi vijiji vya ujamaa, Elimu, operation maduka, haiwezekani maneno ya Mwalimu yakawa mazuri kwenye kusoma tu, why not kutekeleza? yaaani mapka siasa za vyama vingi zimetushinda, WHY?