Nia ilikuwa nzuri lakini kama wanavyosema wahenga ni safari ndefu kati ya mkono na mdomo. Makosa yalitendeka na ndiyo maana tukafika hapo tulipo. Kuna wengine walionewa, kuna wengine walipendelewa n.k. Haya yote yalitokea kwa sababu mpango mzima wa kuuza haukuandaliwa vyema na kikamilifu zaidi. Pengine yangeweza kuepukwa kama pangekuwa na uwazi zaidi. Kwa bahati mbaya hiyo sio hulka yetu.
Haya na tuongee kisomi ingawa mimi huko simo. Mkuu naona unaishi Marekani. Je huko serikali inatoa huduma hii kwa wafanyakazi wake wote? Condoleeza anakaa katika nyumba ya serikali? Au uingereza? Brown kabla hajaukwaa uPM alikuwa anaishi katika nyumba ya serikali? Au Afrika kusini? Au nchi yeyote iliyoendelea? Wafanyakazi wa serkali wanapewa nyumba za kuishi bure na serikali kuu?
Suala la kutoa huduma hii halikuwa sustainable kwa jinsi lilivyokuwa likifanyika. In the long run huduma hii inatakiwa itolewe na soko la nyumba. Mfanyakazi alipwe vizuri na sokoni pawe na nyumba za kutosha zinazokidhi mahitaji yake kwa bei atakayomudu. Kwa sasa hivi hapa kwetu hilo soko halipo. Mahitaji yamezidi mno production kiasi cha kuwafanya wenye nyumba hizo kutoza pango wanavyotaka.
Serikali kwa muda mrefu ilikuwa haitoi fungu kwa ajili ya kuzikarabati wakati pango lilikuwa pegged kwenye mshahara wa mkazi. Mshahara wa wengi waliokuwa kwenye nyumba hizo ulikuwa kati ya 100,000 na 200,000. Hawa walikuwa wanalipa asilimia 10 ya mshahara kama pango hivyo kufanya pango kwa mwezi kuwa sh 10,000 hadi 20000. Hii pango ilikuwa haitoshi hata kunua kitasa na ilikuwa chini ya pango la chumba Mwananyamala chenye umeme! Serikali kwa hiyo ilitakiwa aidha iamue kusubsidise huduma kwenye nyumba hizi ( kitu ambacho katika soko hilo la huria halikubaliwi), kuongeza mshahara wafanyakazi wake wanaoishi katika nyumba hizo ili pango liwe linaloendana na mahitaji halisi ya uendeshaji, kupangisha nyumba hizo kwa wakaaji wake kwa market rates, kuziuza n.k. Uamuzi uliochukuliwa ni huo wa kuziuza. Taratibu za uuzaji wa mali ya serikali unasema mali hiyo itauzwa kwa mnada. Hivi hizo nnyumba zingeuzwa kwa mnada wamatengo wangapi wangeona ndani? Tukumbuke hatuzungumzii za Masaki tu bali hata zile za Chang'ombe! Matokeo yangekuwa kuwa nyumba hizi zimenunuliwa na wafanyabiashara na tukiwa zaidi, wafanyabiashara ambao wengi wao wangekuwa ni wahindi, waarabu au makaburu tungesema nini?
Huyo atakayeamua ku'nationalize' hizi nyumba tena itakuwa uamuzi wake na bila shaka atafanya hivyo baada ya kujiridhisha kuwa ni uamuzi utakaoangalia maslahi ya taifa letu. tulitaifisha nyumba kibao, tukaanzisha Msajili wa Nyumba, zikatushinda kuzihudumia hadi hapa tulipo ambapo tunazirudisha tena katika soko huria.
Katika sera za soko huria ambzo tunazo bongo sasa hiv, serikali huwa haimiliki nyumba, ila inakusanya kodi kutoka kwenye nyumba n property, uamuzi wa kuuza nyumba za serikali ulipitishwa na bunge hilo hilo kwa kushinikizwa na IMF na World Bank, under Mkapa,
Kwenye zoezi hilo, taifa letu limewanusuru viongozi wetu wasafi na waovu kuanzia kina Sozigwa mpaka kina Makani, ambao hawakuiba wakiwa madarakani, the ishu ni kuwa kuna waliouziwa ambao hawastaili, lakini sio otherwise, bila ya hili zoezi kina familia ya marehemu Mnauye, ambaye hakuiba hata senti tano ingeishi wapi?
Mimi nashindwa kuelewa kitu kimoja mtu kama aliyekuwa Katibu mkuu wa CCM Mangu'la aliuziwa hizo nyumba kwa vigezo gani ? Mimi nadhani ingekuwa bora kama hizo wangepewa NHC ili wazirekebishe halafu wapangishwe watu wa serikali !
FM,
Nafikiri sio kila jambo linatuhitaji tujilinganishe na US, UK au nchi nyingine zilizoendelea. Mazingira ya miundo mbinu ya nchini kwetu pamoja na mishahara ya wafanyakazi wetu ni tofauti sana nchi ulizotumia kama mifano. Kwa hiyo utendaji wetu, tokea enzi za mkoloni ulikuwa tofauti hata ukilinganisha na wa wale waliokuwa wanatutawala.
Nakubali kuwa mazingira yetu ni tofauti na hizo nchi. Lakini swali langu lilikuwa kwenye milki ya nyumba na si kuwa tuwaige. Bin maryam ameeleza vizuri zaidi yangu kwa nini mfumo wa kuwapa nyumba wafanyakazi ulikuwepo tangu wakati wa wakoloni. Cha muhimu ni kuangalia kwa nini wamejitoa kwenye kutoa huduma hii na kuona kama kuna tunachoweza kujifunza kutoka kwao.
Sustainability ni suala la planning iwe ni huduma au biashara. Tukiplani vizuri hakuna linaloshindikana, hasa wakati huu ambao tuna wasomi wengi na kama mambo yataendeshwa kiuwazi. Kwa mfano, kwa nini hizo nyumba za serikali zisiwe chini ya kampuni binafsi kuziendesha kibiashara kama NHC? Maana kama ulivyosema, sidhani kama huko sokoni kwenye kila mji/kituo cha kazi TZ atakachohamia mtumishi wa serikali kuna nyumba za kupanga anazoweza kutumia.
Pia unasema kuwa mfanyakazi anatakiwa alipwe vizuri ili alipe kodi at market value, Je hili limefanyika tokea zilipouzwa hizo nyumba?
NHC ndiyo mfano mzuri wa shirika kujiendesha kibiashara? Huko nako matatizo si yale yale? Tulibinafsisha nyumba zilizokuwa na bei zaidi ya sh laki moja miaka ya sabini, tukaanzisha chombo kinachoitwa msajili wa Majumba, zikatushinda. Leo unamuona NHC ndiyo mkombozi? Planning, Mkuu, has never been our strong point. Hatuna patience.
Nilisema moja ya njia za kuwezesha serikali kuhudumia hizo ilikuwa ni serikali iongeze mishahara hadi level ambayo mtumishi ataweza kulipa kodi iliyo katika market value. Hii haikufanyika kwa sababu serikali iliona haitaweza kubeba mzigo huo mara moja. Alternative nyingine ilikuwa ni serikali ilipie moja kwa moja huduma hizo bila kuangalia makato ya watumishi. Hii nayo ilionekana haifai maana neno subsidy limekuwa anathema kwetu.
Nafikiri hapa unajichangaya, upande mmoja unaunga mkono soko huria, upande mwingine hutaki soko huria kutumika kuuza nyumba, wapi kwa wapi....
Lakini mchanganyo wako mkubwa ni pale unaposema kuwa nyumba ziuzwe kwa vile mishahara ya wanaokaa ndani yake ni midogo kulipia kodi at market rate, sasa sijui una-solve nini hapa. Kama mishahara haiwezi ongezwa kufikia hali ya soko kwa nini basi nyumba ziuzwe? Cha kushangaza ni kuwa wanunuzi ni hao hao tunaosema kuwa hawawezi kulipa kodi? Kweli wanajua kutuchezea....
Unayejichanganya ni wewe mwenyewe Mkuu. Hakuna mahalli niliposema naunga soko huria au la. Nimejaribu kuweka pros and cons za suala lote na watu kama nyinyi ndiyo muamue kipi kingekuwa bora zaidi. Kuwauzia wafanyakazi wa serikali kwa controlled process ( bei iliyo chini ya market value, sheria za kutoziuza tena n.k.) au kuziweka kwenye soko huria ili wenye uwezo wazinunue kadri wanavyotaka. Serikali inaelekea iliona njia ya kwanza ni afueni sasa wewe ni haki yako kupinga na kusema kwamba hayo niliyoainisha si kweli. Pengine unawajua waswahili kibao wana uwezo wa kushindana katika mnada na kununua hizo nyumba! Nenda kahudhurie hiyo minada ya serikali ( wanakouza samani, magari n.k) halafu utuambie kama nako haki kweli inatendeka. Tukumbuke kuwa nyumba tunazozingumzia ni pamoja na zile za Chang'ombe.
Serikali ina limit cha kiasi ambacho kinaweza kunkata mtumishi kama pango. Haiwezi ikasema, kwa mfano, kuwa wafanyakazi wanaokaa kwenye nyumba ya serikali watakatwa asilimia 80 ya mshahara wao kama pango. Hii haiwezekani hata kama mtumishi huyo ana miradi yake na anaweza kuishi bila mshahara. Vile vile ukumbuke si watumishi wote wenye miradi yenye kuwawezesha kuishi bila kujali mshahara. Kilichoonekana ni lesser evil ni kumuizia nyumba kwa bei nafuu ambayo ataweza kulipa kwa namna anavyojua. Kwa sababu malipo haya si lazima yatoke kwenye mshahara wake kama ilivyokuwa pango la nyumba. Naamini kuwa pamoja na hii, kuna walioshindwa. Sasa wapi nimejichanganya?
Nafikiri nyumba sio tu kuwa ziliuzwa kinyume cha sheria, bali pia zimeliingiza taifa hasara kubwa. Ushauri wangu kwa JK ni kwa serikali kuzirudisha nyumba zake mikononi mwake na kuunda kampuni ya kusimamia upangishwaji wake kwa watumishi wa uma, at a market rate subsidised by the govt.
]kwa hotuba ya Mkapa wakati akiwaaga? Nimeishakuambia angalia unalozungumzia. Una base yote hii kutoka[/B
Bila shaka nae uko karibu nae.
Wanasiasa wanatumia IMF na World Bank kama bogey figures pale wanapobanwa.
Kushauriwa na bunge imekuwa lini sawa na kupitishwa na bunge?
Nimekuuliza kuhusu hayo maghorofa ya Tabata, bei ya nyumba Obei umeshindwa kujibu. Kama haujui, nyamaza tuu, There is no shame in it.
Wewe ndio unyamaze maana unaonyesha kwa maneno yako kuwa ni huelewi kitu, nina marafiki kibao wamenunua nyumba Tabata, tena ilifikia mahali Magufuli mwenyewe ndiye aliyekuwa anaidhinisha kuuzwa, kwa mkuu tafuta facts kabla ya kurukia hapa utaaibika mkuu!
Unanifanya nijisikie sifa kuwa fundi mchundo. Couldn't have said it better!
Natumaini kwa vile msomi mwenzao umesema, watakuelewa!
Fundi Mchundo:
Sawa Fundi. Lakini unafanya kazi nzuri hapa ingawa safari yenyewe bado ni ndefu sana.
Kuna ukweli na siasa. Hapa wengi ni siasa na katika siasa unahitaji point moja iliyo vague na baadaye ku-spin. Katika ukweli inabidi uwe na facts zinazokuwa na data.
Ukweli ni kuwa model ya serikali kuwa na nyumba kwa wafanyakazi wake umepitwa na wakati.
Na tatizo la Mawaziri kuwa hotelini baada ya nyumba kuuzwa sio geni na ni kawaida kwetu kufanya vitu kinyume na utaratibu. Kuna viwanda vingi tu vilijengwa wakati nguvu za umeme hazijulikani zitapatikana wapi. Dodoma umechaguliwa mji mkuu wakati mawasiliano yenyewe yalikuwa ni treni tu.
Na wenzetu wanaofanya mambo yao vizuri wame-refine mambo yao kwa miaka mingi. Na kwa sisi wageni wa uendeshaji wa serikali za kisasa tunaweza kuiga vile vinavyowezekana katika mazingira yetu. Au kuanza upya na kutumia muda mwingi wa ku-refine makosa yetu.
Hivyo tukitaka kuongoa matatizo ya maafisa wa juu kukaa hotelini ni lazima tueleze katika taratibu zetu kuwa ni viongozi gani wa juu wanapewa nyumba. Na siku muda wao unapokwisha basi waondoke na wanaofuatia wachukue nafasi hizo. Tunaweza kuiga kwa Marekani, kwa miaka mingi idadi ya wizara zimebaki zilezile (ukiondoa mabadiliko yaliotokea baada ya september kumi na moja) na rais hana uwezo wa kuanzisha wizara mpya bila mabadiliko ya kikatiba. Hivyo ukubwa wa baraza lao ni karibu lilelile na majengo ni yaleyale. Hivyo mabadiliko ya serikali hayaongezi mahitaji ya nyumba kwa watumishi wa serikali.
Ni rahisi sana viongozi wa Tanzania kuiga jinsi kiongozi wa Marekani anavyotembelea kwenye Limo, F1 au Marine 1 kuliko kuiga mfumo wenye wizara zisizo badilika badilika.
Kwa nini aunde kampuni nyingine wakati National Housing ipo? Na nani atakayetoa hiyo subsidy? Ukumbuke kuwa sio kila mfanya kazi wa serikali aliyestahili alikuwa na nyumba. Hata wakati huo, wengi tu walikuwa wakiishi mahotelini. Dawa ni badala ya kugombea hiki kidogo tulichoshindwa kukiendeleza, serikali ingefanya jitihada za kuweka mazingira ambamo watu binafsi, makampuni binafsi na vyombo vya umma vitaweza kujenga nyumba nyingi kwa ajili ya kupanga au kuuza.
Wakati umefika ambapo makazi bora iwe ni haki ya KILA mtanzania na si wafanyakazi wa serikali tu.
Baada ya serikali kuuza nyumba kwa nini bado inawagharimia watumishi wake kuishi hotelini?
Mimi nilidhani nyumba za serikali zimeuzwa ili kila mtumishi wa serikali ajiju?
unapewa mshahara wako jua wapi utaishi, uwe waziri au katibu wa wizara ni lazima ujiju.
Huu ni wenda wazimu mkubwa kusema serikali za dunia hazihodhi nyumba wakati huohuo sisi bado tunaendelea kulipia gharama za nyumba za watumishi wa serikali?
Haya tena kuna mradi mkubwa wa nyumba zaserikali ulianzishwa mara baada ya kuuza nyumba za serikali. Sasa usemi kwamba serikali haihodhi nyumba ni wa kweli aua MH Field Marshal unatetea policy yenye kila aina ya ukinyonga?
Madilu:
Mbona umeacha kutumia neno lako takatifu SISIEMU.