Ufisadi wa Meya wa Bukoba Anatory Aman

Ufisadi wa Meya wa Bukoba Anatory Aman

Naunga mkono juhudi za meya wa Bukoba kuuendeleza mji huo wa kizamani ambao umeshlndwa kupata maendeleo kwasababu ya siasa za fitina majungu ya wanasiasa na baadhi ya wasomi wa Buhaya. Miji mingi ktk
Tanzania ni kama Slums kwasababu wahusika walishindwa kupima viwanja mapema matokeo ni ujenzi holela. Malalamiko yatakuepo lakini namtaka Meya na Mkurugenzi wa Manispaa ya Bkb msirudi nyuma.
 
nyie mnapotoshea tu meya wa watu... mbona hujatoa vithibitisho vyovyote kuhusu ufisadi wake
 
Nduguyangu hao unaowataka kuendelea na juhudi zao ndiyo hao wanaojichanganya, baada ya mbunge Kagasheki kutamka kwenye mkutano wa hadahara katika uwanja wa mayunga 24/11/2012, akawafumbua macho wananchi kuwa hakuna hatua muhimu iliyowahi kufikiwa katika upembuzi yakinifu kuhusu soko, siku moja baada ya mkutano huo lililetwa gari aina ya FUSO yenye nambari za usajiri T 975 AUJ kutoka kampuni ilioandikwa kwa MACKA PEN ubavuni kuwa ni ya GEOPINUS ENGINEERING LTD ya Dar es salaam hatahivyo lilikuwa bovu pamoja na mitambo ya kupimia maji kwenye soko lakini ni baada ya Kagasheki kusema hilo.

baada ya siku kumi ikiwa ni Desember 3, 2012, mkurugenzi huyo huyo wa manispaa unayemsema HAMIS KAPUTA akaitisha kikao cha waandishi wa habari ili kufafanua miradi ya maendeleo manispaa ya Bukoba, kama alivyotakiwa na CCM mkoa kupitia mwenyekiti wake Bi CSTANSIA NYAMWIZA BUHIE, na kusema kuwa hakuna mkataba rasmi wa ujenzi wa soko, lakini akaenda mbele zaidi kuwa hawajafanya makubaliano yoyote na chama cha mapinduzi, ili kuwapa nafasi katika jengo ambalo alijaisha ujenzi ili kuwaamishia wafanyabiashara sasa unawapongeza kwa kitu gani katika mkanganyiko huo ambao mkurugenzi aliona utambana akaamua kuoa ukweli?
 
Nduguyangu kuna mtu anawapongeza Meya na mkurugenzi lakini nakusihi waogope hao unaowataka kuendelea na juhudi zao ndiyo hao wanaojichanganya, baada ya mbunge Kagasheki kutamka kwenye mkutano wa hadahara katika uwanja wa mayunga 24/11/2012, akawafumbua macho wananchi kuwa hakuna hatua muhimu iliyowahi kufikiwa katika upembuzi yakinifu kuhusu soko, siku moja baada ya mkutano huo lililetwa gari aina ya FUSO yenye nambari za usajiri T 975 AUJ kutoka kampuni ilioandikwa kwa MACKA PEN ubavuni kuwa ni ya GEOPINUS ENGINEERING LTD ya Dar es salaam hatahivyo lilikuwa bovu pamoja na mitambo ya kupimia maji kwenye soko lakini ni baada ya Kagasheki kusema hilo.

baada ya siku kumi ikiwa ni Desember 3, 2012, mkurugenzi huyo huyo wa manispaa unayemsema HAMIS KAPUTA akaitisha kikao cha waandishi wa habari ili kufafanua miradi ya maendeleo manispaa ya Bukoba, kama alivyotakiwa na CCM mkoa kupitia mwenyekiti wake Bi CSTANSIA NYAMWIZA BUHIE, na kusema kuwa hakuna mkataba rasmi wa ujenzi wa soko, lakini akaenda mbele zaidi kuwa hawajafanya makubaliano yoyote na chama cha mapinduzi, ili kuwapa nafasi katika jengo ambalo alijaisha ujenzi ili kuwaamishia wafanyabiashara sasa unawapongeza kwa kitu gani katika mkanganyiko huo ambao mkurugenzi aliona utambana akaamua kuoa ukweli?
 
Wanasema viongozi wengine wakiwa katika harakati za kuwania nafasi, uwaahidi wananchi kuwaletea meli sehemu isiyo na ziwa wala bahari lakini mwingine kwenda mbele zaidi kuwa atawajengea daraja wakati anasema daraja sehemu isiyo na hata kajito kokote kama siyo mto.
Hiyo ndiyo njia aliyoitumia Meya wa manispaa ya bukoba ANATORY AMAN, baada ya kuwalazimisha uongo wananchi kuwa soko litavunjwa tarehe 15/01/2013, huku akijua kuwa hakuna chochote alichotimiza katika mchakato huo tofauti na wizi alioutumia kujichotea mapesa ambayo hatahivyo inawezekana akabainika.
(1) Jana nimesikiliza mazungumza ya wafanyabiashara wa soko la Bukoba katika manispaa kupitia ka-redio ka Mheshimiwa Kagasheki Kasibante, wakisema kuwa huyu Meya alitumia njia mbalimbali za kubadili uongozi wa soko hilo kwa kuwachagua viongozi wanaomuunga mkono, akiamini kuwa baada ya kuondoa uongozi huo atakaouweka utamkubali na kushawishi wafanyabiashara wengine wakubali kirahisi.
Cha ajabu wanasoko waligundua kuwa anataka kuwaingiza mitini kwasababu waliambiwa na halmashauri kuwa wakarabati mabanda ya soko wao wenyewe, baada ya kulalamika kuomba kujengewa mabnda hayo yaliyokuwa mabovu, na muda mfupi baada ya kujijengea tena kwa gharama kubwa wakasikia kauli ya kuvunja soko inaletwa kwa kasi ili walijenga wapate hasara, hapo ndipo wanakili kuwa huyu jamaa gaidi.
(2) Meya Amani anatambulika kuwa ni maarufu kwa kumwaga sumu kwenye chama au sehemu anayotaka kupata maslahi ili waliomo wakivurugana yeye apate njia nzuri ya kuwa kinara kwenye sehemu hiyo. Hii ilitokea mwaka 2001 baada ya huyu jamaa kumwaga sumu kwenye chama ili aweze kugombea uongozi wa juu wa jimbo, jambo ambalo lilipelekea CCM kukosa nafasi hiyo kwasababu hawakuwa na umoja, na katika muda huo Amani hakuwa na jina la kumpatia nafasi hivyo uongozi wa jimbo ukakamatiliwa na chama pinzani.
Baada ya kuibuliwa kwa hoja mbalimbali kuhusiana na utata wa uraia wake, jamaa alikaa kimya na kuamua kuwaunga mkono waliojitokeza kutetea chama kama mbunge wa jimbo hilo ambaye sisi tunamuita BABU KIPARA, lakini maskini ya Mungu mzee huyo hakujua kama jamaa huyo ni nyoka ambaye anapitia kwake ili aweze kujiimarisha na hatimaye kila kitu kinachotetewa na mbunge kionekane kimefanywa na Meya kwasababu ananafasi kubwa ya kuwafikia wananchi kupitia madiwani wenzake.
Pamoja na kujaribu kuwaweka karibu madiwani wachache ambao kiongozi wao ni diwani kata Kahororo CHIEF KALUMUNA, na viongozi mbalimbali wa chama na serikali.
(3) Nawashangaa baadhi ya wanahabari wanaomng'ang'ania kwasababu mwaka jana aliwaahibisha kwa kumtandika vibao mwanahabari mwenzao katika ukumbi wa manispaa, baada ya kuona mwandishi huyo akiingia kwa ajili ya shughuli za kihabari muda mfupi baada ya kuwapokea wageni waliokuwa wametembelea manispaa.
Hicho ni kitendo cha uzalilishaji walichofanyiwa wanahabari wala si mwanahabari mmoja na kama angekuwa ni yeye, lazima angesema asafishwe kupitia vyombo vya habari, lakini kwasababu ya pesa japo hatujui alimlipa au yalikwisha kwasababu mwandishi hakuwa na nguvu ya kuendesha kesi, jambo hilo liko kimya hadi sasa.
 
Nasikia leo madiani wa ccm wamepigana kwenye kikao wakati wakijadikli ufisadi wa meya na hoja ya kutokuwa na imani naye ,

nitawajuza
 
Mbivu na mbichi za meya Bukoba leo

MBIVU na mbichi za Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dk. Anatory Amani, zinatarajia kujulikana leo baada ya kikao cha madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumalizika.
Meya Amani anatuhuniwa na baadhi ya madiwani wa manispaa hiyo kuwa, ametumia vibaya madaraka yake na hivyo kujihusisha na vitendo vya ubadhirifu.
Tayari madiwani nane wa chama hicho, akiwemo pia Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki pamoja na wengine wawili wa upinzani, wametia saini hati ya kumtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo, aitishe kikao cha dharura ili kumng'oa meya huyo.
Hoja ya kumng'oa meya iliibuliwa hivi karibuni na Balozi Kagasheki, ambaye pia ni Waziri wa Malialisili na Utalii, akiunga mkono msimamo wa CHADEMA, kupinga miradi ya uuzwaji wa viwanja zaidi ya 5000 na ujenzi wa soko la kisasa.
Kagasheki aliapa mbele ya wapigakura wake kuwa, hayupo tayari kusutwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, kutokana na mikataba ya siri yenye harufu ya kifisadi aliyoisaini Meya Amani kwa kificho bila kuwashirikisha madiwani wenzake.
Hata hivyo, habari za ndani ambazo gazeti hili limezinasa zinasema kuwa, baadhi ya vigogo wa serikali na chama Mkoa wa Kagera, wamekuwa wakifanya kila juhudi kumnusuru Amani kwenye sakata hilo.
Vigogo hao ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mjini, Mwenyekiti na Katibu wa CCM Mkoa.
Chanzo hicho kilibainisha kuwa, sakata hilo limefikishwa hadi mezani kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, huku Mkuu wa Mkoa, Kanali mstaafu Fabiani Massawe akijaribu kumwangukia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia bila mafanikio.
"Massawe aliwasiliana kwa simu na Waziri Ghasia akimtaka aingilie kati sakata hilo, lakini hakufanikiwa kwani waziri huyo alimtaka awasilishe malalamiko yake kwa maandishi akidai hafanyi kazi kwa simu," alisema mtoa habari wetu.
Katika hatua ya kujaribu kuwazima madiwani hao, Katibu wa CCM Mkoa, aliitisha kikao cha Kamati ya Siasa kilichohudhuriwa pia na wabunge Kagasheki na wale wa viti maalum, Elizaberth Batenga na Bernadetha Mshashu, akiwahoji ni wapi wamepata kibali cha kuitisha kikao cha dharura.
Hata hivyo, kikao hicho kiligeuka kuwa suluba kwake baada ya madiwani hao kutoa masharti mazito kwa chama, kuhakikisha kinamshawishi Amani ang'oke kabla ya Machi 22, ambapo kikao cha ‘full council' kitaketi na kumtimua kwa kura.
"Tulihoji inakuwaje mtu anayetuhumiwa kwa ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka, anakingiwa kifua na viongozi wakuu wa chama na serikali badala ya kumchukulia hatua," kilisema chanzo chetu.
Jumatatu wiki hii, kilifanyika kikao cha Kamati ya Siasa ya Wilaya na kubariki hatua ya madiwani hao kuendelea na utaratibu wao ikiwa CCM hawatapata muafaka.
Madiwani wa CCM watakuwa na kikao cha kumjadili meya leo na baada ya hapo watapeleka taarifa yao kwenye kamati hiyo ya siasa wilaya ili kuona ni uamuzi gani wamefikia.
"Kikao hiki ndicho kitakuwa mbivu na mbichi za Meya Amani kuamua anachukua uamuzi gani, kujiondoa mwenyewe ama kusubiri kikao cha ‘full council' ili ang'olewe kwa kura," kilisema chanzo chetu.
Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba ina madiwani 24 ambapo kati yao watatu wanatoka CUF, wanne ni wa CHADEMA na 17 wanatoka CCM.
Na ili kupitisha uamuzi huo wa kumuondoa meya, ni lazima robo tatu ya madiwani, yaani 16, wapige kura ya kuunga mkono hoja hiyo.
Miongoni mwa vigogo waliosaini hati ya kutaka kuitishwa kikao cha kumng'oa meya huyo ni naibu wake, Alexander Ngalinda (Diwani wa Kata ya Buhende) na Yusuf Ngaiza (Kashai) ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Bukoba.
Sakata hilo limezua mgawanyiko mkubwa si kwa CCM tu, bali hata kwa CHADEMA kwani kuna fununu kuwa fedha zimetembezwa kwa baadhi ya madiwani ili kuwazuia wasipige kura ya kumpinga meya.
Taarifa za ndani zinasema kuwa, mgogoro huo umechukua mtazamo wa kisiasa kutokana na baadhi ya wanasiasa mkoani humo kutaka kuutumia kujiimarisha kisiasa kwa ajili ya kinyang'anyiro cha ubunge 2015.
CHADEMA ambao walikuwa ni waanzilishi wa hoja hiyo, kwa sasa madiwani wake wamegawanyika wakidaiwa kushawishiwa na kigogo mmoja wa chama hicho mkoani humo, ili kutopiga kura ya kumpinga meya Amani.
Hata hivyo, Mbunge wa Viti Maalum wa chama hicho mkoani humo, Conchester Rwamlaza, ambaye ni diwani, alisema kuwa atahakikisha kwa gharama yoyote wanasimamia hoja yao mpaka mwisho licha ya mgawanyiko unaoanza kujitokeza.


[TD="bgcolor: #ffffff"]
Mbivu na mbichi za meya Bukoba leo


na Edson Kamukara


[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
amka2.gif
[/TD]
 
Nimekuwa nikifuatilia sakata la Meya wa Bukoba pamoja na Mbunge Kagasheki.

Pamaoja na yote yanayoongelewa na pande zote mbili,inawezekana kila upande unakuwa na hoja zake.
La msingi baada ya maneno yote watu wanataka maendeleo ya vitu vinavyoonekana,kama inavyodaiwa kuwa kuna dalili ya ufisadi katika miradi hiyo,basi kaa vizuri na wataalamu wenu rekebisha hiyo mikataba na miradi iendelee kufanyika kama ilivyopangwa,vinginevyo malumbano haya hayatawasaidia kamwe.

You better hurt me with truth rather than comforting me with lies
 
kamkala vipi wewe awajakuona, maana najua ukitupiwa fupa utapoa tu, we si mwandishi,,, lakini pambana kaka.
 
Duh....
Kagasheki kumbe nae noma?
Siasa mchezo mchafu kweli. Kuna dalili huyo Meya anatumika na hao vigogo. Si bure kabisa
 
Unaonekana umekuja rasmi kummaliza huyu Meya kitu ambacho kitakuwa hakitendi haki kwa kuegemea upande mmoja na kushusha makombora ambayo hayana mjibuji. Embu nisubirie waelewa waje wakuumbue hapa

Mangapi humu jamvini ambayo mnazungumzia pande zote zinazohusika???? acha unafiki wa kipuuzi kwani tabia ya kuwa one sided humu jamvini kwa sasa imekuwa ni mila na desturi na yote haya nyinyi mliokuja \baadaye humu ndani mkabadilisha na pakawa mahala ambapo kila mtu anaweza kuandika chochote kile[short of matusi]
 
Back
Top Bottom