Ufisadi wa mabilioni tena Nishati na Madini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi wa mabilioni tena Nishati na Madini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 20, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,064
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Ufisadi wa mabilioni tena Nishati na Madini [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 19 January 2012 20:47 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Leon Bahati
  Mwananchi

  SERIKALI kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeingia tena katika kashfa ya ufisadi wa matumizi mabaya ya rasilimali za umma, baada ya kubainika kuuza kinyemela sehemu yenye utajiri mkubwa wa makaa ya mawe Kiwira kwa kampuni ya Tan-Power Resources (TPR).

  Uamuzi huo unaelezwa na wachunguzi wa mambo kuwa utaathiri mradi wa kuzalisha umeme wa makaa ya mawe kwa kusababisha bei ya nishati itakayozalishwa eneo hilo kuwa ghali na italisababishia serikali hasara ya dola za Marekani 600 milioni sawa na Sh960 bilioni.

  Tuhuma hizo za ufisadi, ziliibuka kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na kuifanya iwaite maofisa wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini kujieleza mbele yao, jana.

  Sehemu inayodaiwa kuuzwa ilitajwa kuwa ni mlima Kabulo, ambayo aliielezea kuwa ina utajiri mkubwa zaidi wa makaa ya mawe kuliko eneo jingine la Kiwira.

  Mwenyekiti wa POAC, Zitto Kabwe alithibitisha kamati yake kuwaweka 'kitimoto' maofisa waandamizi wa wizara hiyo.

  "Tumewaita ili watupe maelezo ya kina kuhusu suala hilo," alisema Zitto akilalamika; "Hili ni tatizo la kuchezea raslimali za nchi,"

  Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni alisema tukio hilo limekuja wakati ambao serikali imetakiwa kumiliki hisa zote za mradi huo ili kuhakikisha anapatikana mbia anayeweza kuendesha mradi huo kwa faida.

  Alisema mradi huo ambao ulikuwa unamililikiwa kwa pamoja kati ya serikali na kampuni ya Tan-Power Resourses, ulitakiwa kusimamishwa pia wafanyakazi walipwe haki zao.

  Lakini mpaka sasa, alisema wafanyakazi hawajalipwa ingawa mradi huo umesimama jambo ambalo linaendelea kuisababishia hasara serikali.

  Akizungumzia athari za kuuzwa kwa eneo lenye utajiri mkubwa wa makaa ya mawe, Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka alisema mradi wa umeme unaotarajia kuanzishwa, gharama yake itakuwa kubwa kutokana na malighafi kuzalishwa na kampuni nyingine.

  Ole Sendeka alisema Serikali ilikopa Benki ya Dunia dola za Marekani 600 milioni sawa na Sh960 bilioni kwa ajili ya kuendeleza mradi huo lakini kwa kuuzwa sehemu ya Kiwira, serikali itapata hasara kwa kulipa fedha hizo na riba yake kwa mradi ambao unamilikiwa na kampuni binafsi.

  Hadi jana jioni Mwananchi lilipoondoka katika ofisi za Bunge, watendaji wa Wizara walikuwa bado hawajawasilisha maelezo yao mbele ya kamati hiyo.

  Historia ya Kiwira
  Kiwira ni moja ya miradi ambayo Serikali imeiweka katika orodha ya kuzalisha umeme ili kuliokoa taifa kwenye uhaba mkubwa wanishati ya umeme.

  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja aliwahi kuliambia bunge kuwa Serikali imeamua kubeba mzigo wa mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira ili kuhakikisha kuwa unaleta tija kwa Taifa.

  Kampuni ya TPR inadaiwa kumilikiwa na familia ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Waziri wa zamani Nishati na Madini, Daniel Yona.

  Ngeleja alikuwa ameliambia bunge kuwa baada ya uamuzi huo, serikali imeanza mchakato wa kupata uratatibu muafaka wa kuendesha mradi huo kama ilivyokusudiwa kwa kuangalia fursa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuingia mkataba wa uendeshaji na kampuni itakayopewa mamlaka ya kujenga na kuuendesha.

  “Chini ya mkataba wa uendeshaji, mkandarasi atapewa jukumu la kujenga uwezo wa mashirika ya Stamico (Shirika la Madini) na Tanesco ili kuyawezesha kumiliki na kusimamia mradi huo,” alisema.

  Kwa mujibu wa Ngeleja, hatua ya awali ya mpango wa serikali kuanza kuundesha mradi huo zilikuwa zimeanza kwa kuhakikisha kuwa wafanyakazi waliopo wanalipwa haki zao zote na kuwawekea mazingira mazuri ya kuendelea na kazi.

  “Serikali pia imezungumza na serikali rafiki ya China iliyoanzisha na kuendesha mradi huo ili kupata mkopo wa kuufufua na kuhakikisha mradi wa kuzalisha umeme wa MW 200 unakamilika mapema iwezekanavyo,” alisema

  Akizungumzia suala la Rais Mstaafu Mkapa ambaye aliomba kumiliki hisa 200,000, kupitia kampuni yake ya ANBEN Limited, Ngeleja alisema kuwa kiongozi huyo wa zamani alinyang’anywa hisa hizo Januari 10 mwaka 2005 baada ya kushindwa kuzilipia.

  “Mheshimiwa Spika, tarehe 10 Januari, 2005, (Siku 13 tangu kuanzishwa kwa TPR), ANBEN Limited iliondolewa kuwa miongoni mwa wamiliki wa hisa kwa vile haikuweza kulipia hisa ilizokuwa imechukua wakati wa usajili wa TPR.

  Hivyo wamiliki wa TPR waliobaki walikuwa ni DevConsult International Ltd, Universal Technologies Ltd, Choice Industries Ltd na Fosnik Enterprises Ltd zote zikiwa na hisa 200,000,” alisema Ngeleja.

  Wakati huo huo, Zitto alisema jana waliwahoji maofisa waandamizi wa Wizara ya Uchukuzi kwa kile kilichodaiwa ni Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuingia kwenye mikataba inayoliingizia taifa hasara.

  Zitto hakutaja mambo yaliyofanywa na ATCL na kuisababishia hasara serikali lakini taarifa zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa linatakiwa kuilipa kampuni ya kigeni dola za Marekani 36 milioni.

  Fedha hizo zinadaiwa kuwa zilitolewa kwa ajili ya kukodisha ndege ambayo hata hivyo haikuwahi kufanya kazi nchini.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hawa jamaa (Yona na Mkapa) nilidhani walirudisha kampuni yao kwa serikali. What is going on?
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,064
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jasusi hii kitu inashangaza sana. Nami nilidhani hivyo hivyo kumbe ilikuwa changa la macho!
   
 4. mjomba wa kale

  mjomba wa kale JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  hiyo ni kansa inayoendelea kuitafuna serikali na nchi yetu kwa ujumla hivyo suluhisho nionavyo mimi ni kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi na si kingine!.
   
 5. m

  mtengwa JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,745
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Tanzania zaidi ya uijuavyo
   
 6. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  As long as Ikulu iko mikononi nwa Rostam ambaye God father wake ni Benjamin William Mkapa na kwa kuwa JK pamoja na Serikali yake nzima wanamtegemea Rostam kwa fedha na ushauri itaundwa tena tume na matoke hayateielezeki. I once wrote in this Forum about three years ago " Jakaya Mrisho Kikwete is not serous" but some of you thought that I am not a great Thinker? Sasa tuone Mambo endapo the GURU behind the scenes angekamatwa na kupelekwa mahakamani in any of the multitudes of scandals hizi sarakasi zingekwisha. In this case if Mkapa has immunity provided under the current constitution at least Yona and Anna Mkapa have no immunity. Dhambi ya kutokuwapeleka mahakamani haitaishia hapo. I have been reliably told that the sale to Tan power is clandestine arrangement done under cover of course with state blessings to settle out of court ili wasidai fidia for loss of profit and investments of over Usd 15m spent on the project before government take over. Kweli nimeamini Ikulu kuna biashara tena yenye kukingiwa kifua na Katiba yetu! Inachefua saana! Hapa patamu containers of the deadly poison should be intercepted at TErminal ya Rostam hapo Bamdarini? Lowasa huna huruma na bado unataka urais 2015" CCM wafanyizieni hawa mafisadi uchaguzi wa mwaka huu. Kama kweli JK yuko serious then I want Ngeleja , Malima na mtandao wao out from MoEM jumatatu asubuhi!
   
 7. M

  Maga JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 325
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hivi hii nchi nani katuloga?
   
 8. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Do, This is very serious.
  Nchi ya wajinga kabisa, ni kama mama ntilie anavyoendesha biashara yake?????
  Hata aibu na woga hatuna?
   
 9. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Nilisha sema Mkapa ni msaliti wa taifa. Hakuna rais aliyefanya biashara ikulu kama Mkapa.
   
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Dharau nyingine kwa kweli ni za kujitakia! Hawa 'walafi' katika nchi hii watajitwalia kila kitu tukiendelea "kuwachekea"!
   
 11. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Nifahamisheni ndugu wana jamvi nani alieuza hiyo ardhi kamuuzia nani kwa sheria ipi nafikiri nchi imeuzwa tufanye hima kujikombomboa kishatutengeneze sheria nzuri watake wasitake
   
 12. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Sasa nazidi kuelewa kwanini swala la katiba mpya lilipitishwa kibabe babe na hata jk alipofatwa na cdm alichojibu ni asiposign hawatamwelewa
  sasa namwelewa ben ni mtu wa namna gani
   
 13. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kama kawaida yetu watanzania, hili nalo litapita bila mtu kuwajibika ama kuwajibishwa.

  Tunachoweza kwa hakika ni majungu na umbea pamoja na kulalamika kwanini Dr. Slaa hakumsalimia Dr. Kikwete.
   
 14. F

  FUSO JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  kama ni kweli basi ndugu yetu ngereja kashindikana kabisaa.... sasa hakuna uhakika kama ni yeye anaamua hivi au kuna kundi la watu lenye NGUVU linampatia maelekezo -- hapa ni GIZA nene.
   
 15. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Msipomwondoa fisadi papa m k w e r e mtalia na kusaga meno.
   
 16. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Hivi hii nchi inaongozwa na Watanzania au wawekezaji? Tusije kushangaa siku moja nhi yote imekodishwa na tukaanza kutozwa ushuru wa kuishi!
   
 17. K

  Kengedume Senior Member

  #17
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hili pepo la viongozi wa ngazi za juu kuigawana nchi ni hatari sana! Sijui ni kwa nini hawana hata uoga, wanakiburi wanawadharau wananch! Nahoji nguvu na kiburi wanatoa wapi! Yawezekana ni waumini wa secret society! Watanzani kunaushuru una kuja kwa ajili ya kuishi. Mi napita tu!
   
 18. W

  Wenger JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  Nchi hii imekwisha tunatakiwa kuchukua hatua za haraka kwa kuwaelimisha wakazi wa vijijini umuhimu wa mabadiliko
   
 19. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,727
  Likes Received: 1,634
  Trophy Points: 280
  Hii wizara inafanana na shule ya secondary Tambaza hapo zamani kila aliyeingia ililithi ka tabia kale kale. sasa naona wizara hii isambaratishwe na ipewe jina jipya na watu wapy labda itabadilika
   
 20. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wewe unamtaja Mkapa? ngoja waifia dini waje hapa. mimi ngoja nisepe zangu mapemaaa kwani hilo garika halitaacha hata wale waliokaribu.
   
Loading...