Ufisadi wa kutisha katika Jiji la Arusha kupitia ukusanyaji wa fedha za Usafi Mitaani

Sirluta
Swala la ada ya taka sio chanzo cha mapato bali ni huduma kwa jamii! Fedha zinakusanywa na wakala ambaye ni mtu binafsi au kampuni binafsi,
Kuhusu matumizi ya mashine ndio tunaelekea huko ila kwa sasa mashine zinatumika kwenye vyanzo ambavyo ni mapato na sio kwenye huduma!

Ukishirikisha ubongo utanielewa vinginevyo endelea na ushabiki
 
Tozo zote ni kwa mujibu wa sheria ndogo,kama unalipishwa zaidi ya sheria inavyosema kwa nini ulipe?ukilipa ni uzembe wako mwenyewe!
Upo kata yangu mtaa upi?enewei nipigie 0754834152
nasemea jiji la Arusha mzee! Wewe ni mjumbe wa sijui fedha na uchumi, huu ni ufisadi wa kutisha msijifanye hamjui kinachoendelea. Sasa hivi nimepata tena taarifa hapa kuna mtaa wanalipa elfu 10 kwa mwezi na gari linafika mara 2! Ufisadi unafanyika et kwakuwa wananchi havjui hiyo sheria ili tukatae kulipa? Mko busy na mapambano dhidi ya mh. Gambo kumbe mnaficha maovu yenu! Natetegemea wewe na Meya wenu mchukue hatua juu ya jambo hii soon. Hizo ambazo mshapiga zinawatosha. Pale Kilombero ukienda haja ndogo unapewa risiti ya TRA iweje buku kumi zikusanywe kwa makaratasi ya watu binafsi yenye nembo ya jiji? Acheni WIZI.
 
Sirluta
Swala la ada ya taka sio chanzo cha mapato bali ni huduma kwa jamii! Fedha zinakusanywa na wakala ambaye ni mtu binafsi au kampuni binafsi,
Kuhusu matumizi ya mashine ndio tunaelekea huko ila kwa sasa mashine zinatumika kwenye vyanzo ambavyo ni mapato na sio kwenye huduma!

Ukishirikisha ubongo utanielewa vinginevyo endelea na ushabiki
tunaelekea hadi lini? Imekuwa ile safari ya Lowasa ya kwenda Bukoba tangu aondoke Dar hadi leo hafiki? Hata kujisaidia siyo biashara ni huduma pia ila kuna usawa.
 
Ufisadi wa kutisha katika Jiji la Arusha kupitia ukusanyaji wa fedha za Usafi Mitaani.

Wakati wa kampeni mwaka jana, Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema alimtaka Meya wa Jiji ndugu Kalist Lazaro kueleza mikakati ya kuliweka jiji katika hali ya usafi, naye alijibu kuwa ameshafanya yafuatayo mbele ya makada maarufu wa Chadema; Edward Lowasa na Frederick Sumaye.

*Jiji la Arusha lina magari matatu ya kuzoa taka.
*Jiji limeshaajiri vijana wa kutosha kwa ajili ya kufanya usafi na wanalipwa na jiji.
*Jiji limeshanunua vifaa vya kutosha vya kufanya usafi.

HALI IKAWAJE BAADA YA
UCHAGUZI.

Fedha zimekuwa zinakusanywa kati ya tshs 1,000 hadi tshs 5,000 kwa kila mpangaji, kwa kila mwezi kwa ajili ya kuzoelea taka zinazokusanywa na wananchi baada ya kufanya usafi kwenye maeneo yao. Fedha hizo hukusanywa na watu ambao huambatana na migambo ili kurahisisha ukusanyaji. Wakati wa ukusanyaji, risiti zenye nembo ya jiji hutolewa. Sasa haijulikani kama zinatoka Jiji ama wanatengeneza wenyewe na kuweka nembo ya Jiji.

UFISADI UNAOFANYIKA.

Mfano chukulia mtaa wenye wapangaji 5,000 mara tsh 2,000 unapata Tshs 10,000,000/= kwa mwezi ambapo matumizi yake ni kwamba gari la kuzoa taka hukodishwa na kwa gharama za haraka hazizidi Tshs 100,000/= kwa trip kwani taka huchukuliwa asubuhi na
mapema kabla ya saa mbili za asubuhi ili wabebe chache maana muda huo watu wengi wanakuwa hawajatoa taka na hawawezi kuzikusanya nje siku inayotangulia kwani husambazwa na wanyama kama mbuzi na mbwa na hufanyika mara moja kwa
wiki na mara 4 kwa mwezi hivyo kwa mwezi hutumia Tshs 400,000 kuzoa taka,
sasa jiulize hizo nyingine huenda wapi?

Wiki mbili zilizopita katika mkutano wa wananchi na watendaji wa mtaa wao, ulivunjika baada ya mwananchi mmoja kutaka kujua mapato na matumizi ya fedha za taka, sambamba na mwingine aliyependekeza fedha zinazokusanywa kupitia vitabu, ni bora
zikakusanywa kwa kutumia EFD za TRA lakini walinyamazishwa haraka sana kwa kuwazima na jibu kwamba watu hawatoi pesa.

Jiji la Arusha lina kata 25 ila mitaa sijajua ni mingapi. Ila tuchukulie lina mitaa 50 mara
wapangaji 5,000 mara tshs 2,000/= unapata zaidi ya tshs 500Milion kwa mwezi. Huu ni
mradi haramu wa madiwani, watendaji wa mitaa pamoja na watu wengine na ndiyo maana ni kosa la jinai kuhoji mapato na matumizi yake.

Kuna wakati watu wa Afya wakiambatana na kikosi kazi huvamia tu watu na wakikuta
mazingira ni machafu, huwatisha hadi watoe hela kati ya tsh 10,000 hadi tsh 50,000 na wasipotoa hupelekwa kwa mtendaji hadi utoe.

NI VEMA SERIKALI IKASITISHA MRADI HUU HARAMU KWA WANANCHI NA KUTUMIA
MAGARI YA JIJI KUKUSANYA TAKA, AMA ZITUMIKE RISITI ZA EFD ZA TRA BADALA YA VITABU VINAVYOTUMIKA.
Mimi nakaa sakina nalipa 2000 kwa mwezi na taka zinasombwa kila wiki hakuna uchafu kma enzi ya chama chakavu.istoshe mbo ya arusha kwasasa sio tija tunataka mlipe deni la IPTL kwa hela zenu mnazofisadi kila mwaka
 
usafi unafanyika katikati ya jiji tu, mitaani ni kuchafu kwasababu ya kukosa usimamizi. Dili lipo kwenye upigaji wa hela tu. Kama wewe ni mgambo wa kuongozana na wale wanaokusanya fedha hizo, lazima useme hivyo maana ndo ulaji wako. Pia watu hutofautiana kwa viwango vya usafi na uchafu. Hivyo wewe unaweza ukaona ni kusafi kwa kuwa umezoea uchafu ila wanaojua usafi wataona ni kuchafu.
Kwani anayetakiwa afanye usafi ni nani? Halimashauli au watu binafsi.Najua wakazi wa maeneo husika wanatakiwa wafanye usafi na halimashauri wabebe taka.Swali jiji ni chafu au taka hazibebwi?
 
nasemea jiji la Arusha mzee! Wewe ni mjumbe wa sijui fedha na uchumi, huu ni ufisadi wa kutisha msijifanye hamjui kinachoendelea. Sasa hivi nimepata tena taarifa hapa kuna mtaa wanalipa elfu 10 kwa mwezi na gari linafika mara 2! Ufisadi unafanyika et kwakuwa wananchi havjui hiyo sheria ili tukatae kulipa? Mko busy na mapambano dhidi ya mh. Gambo kumbe mnaficha maovu yenu! Natetegemea wewe na Meya wenu mchukue hatua juu ya jambo hii soon. Hizo ambazo mshapiga zinawatosha. Pale Kilombero ukienda haja ndogo unapewa risiti ya TRA iweje buku kumi zikusanywe kwa makaratasi ya watu binafsi yenye nembo ya jiji? Acheni WIZI.
Mkuu bado hujaeleweka hii buku 7 Leo haitalika
 
Hapa ndio nimeona hasira za diwani kunyimwa posho. Diwani kaanzisha Uzi kwa kupaniki!
 
V
Swala la usafi limetolewa kwa wakandarasi ambao wanawajibika kuzoa taka zote.Gharama ya uzoaji wa Taka hulipwa na mzalishaji wa taka kwa mujibu wa by law ya Arusha Municipal Council ya 2003.Viwango vya uzoaji vimewekwa na hiyo sheria,kwenye eneo la CBD makazi ni 1000 elfu moja kwa mwezi kwa kaya na hiyo pesa hulipwa baada ya kazi.Nje ya CBD ni 500 mia tano kwa mwezi kwa kaya.Viwango vinatofautiana kutoka kamazi to biashara etc
Hii fedha hukusanywa na wakala mwenyewe ila anatumia vitabu vya Halimashauri maana kwenye hayo makusanyo 15% inarudi Halimashauri hivyo wakala anabaki na 85% pamoja na gharama zote za kufanya hiyo kazi....
Swala la mapato na matumizi halina msingi maana hiyo ni pesa ya wakala ukitaka mapato na matumizo kwa mtendaji sio sahihi ni kumwonea maana hajahusika na hayo makusanyo
Hayo mahesabu uliyoweka hayana uhalisia wowote maana sio kila kaya inalipa wengine hawalipi kabisa
Vipi zile tuhuma za kukusanya mil. 300 hapo stendi ndogo na kugawa maduka kwa makada wa Chadema? Una hoja
 
Ukitanguliwa na mihemko unajikuta unashindwa kujenga hoja vizuri, Kwanza kila mtaa umejipangia kiasi gani kilipwe kwa kila kaya na si 2,000/= kila kaya kwa mitaa yote kama unavyotaka kutuaminisha, Pili rudi kafanye utafiti ujue mtaa mmoja una kaya ngapi na mapato yanayopatikana kwa mwezi kwa kila mtaa ni kiasi gani na urudi uje ujenge hoja yako vizuri, Milioni moja yenyewe kwa mwezi ni vigumu kupatikana wewe unaleta story za 10,000,000/= kwa kila mtaa kwa mwezi? Nilitegemea ungesema wananchi wana haki ya kujua mapato na matumizi ya chanzo hicho cha fedha ili kubaini kama matumizi yake yamezingatia vigezo vilivyo wekwa.
 
sensa ya mwaka 2012 inaonyesha Jiji la Arusha lina watu 416,442. Sasa chukulia sasahivi wapo 600,000 maana juzi wakati wa uchaguzi waliojiandikisha ni zaidi ya laki 3. Sasa assume kila familia ina watu watatu japo wapangaji wengi ni mtu mmoja, wawili ama watatu. 600,000 gawa kwa 3 unapata 200,000 hizo ni familia. Malipo ni kati ya tsh 1,000 hadi tsh 10,000 kwa mwezi. Wengi wanasema wanalipa tsh 2,000. Kumbuka kuna wanaolipa nyumbani na kazini ama kwenye biashara zao. Ignore them. Zidisha kaya 200,000 x tsh 2,000 unapata tsh 400,000,000/= ukiweka na wanaolipa juu ya buku 2 zinafika 500milion.

Sasa ukisema makusanyo kwa mtaa hayafiki hata milion unachekesha. Kwa vyovyote hata ukisema makusanyo yawe nusu. Kuna ufisadi hapa mkubwa tu. Hizi fedha zinakusanywa by assistance ya mgambo hivyo hamna asiyetoa, labda wachache sana tena mara moja moja hawezi akakwepa kila mwezi. Na bado mitaa ni michafu hadi watu wa afya wanapita tena na vikosi kazh kukamata watu na kuwapiga faini. Penye ukweli tuwe wakweli.
 
usafi unafanyika katikati ya jiji tu, mitaani ni kuchafu kwasababu ya kukosa usimamizi. Dili lipo kwenye upigaji wa hela tu. Kama wewe ni mgambo wa kuongozana na wale wanaokusanya fedha hizo, lazima useme hivyo maana ndo ulaji wako. Pia watu hutofautiana kwa viwango vya usafi na uchafu. Hivyo wewe unaweza ukaona ni kusafi kwa kuwa umezoea uchafu ila wanaojua usafi wataona ni kuchafu.
Tatizo lako unaleta ushabiki wa kijinga kwenye mambo ya msingi
 
nina wasiwasi na matokeo yako ya hisabati darasa 7,maana nikisema sekondari na chuo huko ukifika ukisoma hisabati..takwimu zako sio za kutumia hesabu bali ni za kutumia hisabati..hongera kwa kunionesha matokeo yako ya std 7C.
 
kulingana na uwelewa wako ulivyo mdogo kuhusu namba,hapo unaniuliza "tofauti kati ya hisabati na hesabu"..kwi kwi kwi..
 
"hakuna kitu kibaya duniani kama mjinga kukataa kuelimika"..eti unajiita wa mjini na kuwaona wenzio wa shamba,labda nikusaidie hapa mbezi kimara kila nyumba inalipa sh.2000 na sio kila mpangaji,KIHIYO kabisa unaishi kwa porojo..
 
Kujifunza ni pamoja na kusikiliza ushauri wa watu wengine, Tumekushauri kuwa makadirio yako yana makosa mengi sana ikifuatiwa na msukumo wa kiitikadi ya kisiasa, Jaribu kuhudhuria mikutano ya mitaa na fika ofisi za mitaa na kata uliza chochote unachokuwa na mashaka utajulishwa, Hoja zako kiufupi zimejikita kwenye maeneo yafuatayo: 1) unahitaji kujua ni kiasi gani kinakusanywa kila mwezi kwa kila mtaa katika Jiji la Arusha (2) unahitaji kujua matumizi halisi ya makusanyo hayo (3) hufurahishwi na Jiji kuongozwa na chama cha Upinzani na unajitahidi kutengeneza bifu ya aina yeyote ili viongozi wa upinzani waonekane hawana uwezo wa kuhudumia wananchi. Hoja ya kwanza na ya pili zina mashiko na ni haki ya wananchi kupewa taarifa ya mapato na matumizi kama tenda hiyo hakupewa mtu au kampuni binafsi .hoja ya tatu inaitwa wivu wa kisiasa na nakushauri achana nayo haitakusaidia chochote na sana sana itakusaidia kupiga hatua zaidi za kurudi nyuma kimaendeleo.
 
endelea kukaa huko kijijini na ushamba wako. Njoo huku nikuonyeshe. Taka hulipiwa na kila familia, awe mwenye nyumba yake ya kuishi, awe mpangaji tena wenye nyumba na wenye biashara ndiyo hulipa kiasi kikubwa. Tatizo ni kwamba wanaokerwa na haya mambo hawapo kwenye mitandao ili waseme.
Usikariri, nyumba ya wapangaji 25 itakuwa uswahilini sana hiyo una tofauti gani na anayeishi shambani?
 
Kama nyumba moja inakuwa na wapangaji 25, kwanini mtaa usiwe na idadi hiyo ya wapangaji? Pengine hujui maana ya mtaa. Huko madongo kuinama kwenu mnaita kijiji, huku mijini wanaita mitaa. Kama Jiji lina watu milioni, unashangaa nini kuwa na kaya kati ya laki 2 hadi 3, fedha hizi kuna wanaotoa mara mbili. Nyumbani anapoishi na kwenye biashara yake. Ulaji wa bure bure lazima ufike mwisho. Fanyeni kazi halali.

Mkuu, Nyumba moja wapangaji 25 ??????
 
Back
Top Bottom