sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,486
Ufisadi wa kutisha katika Jiji la Arusha kupitia ukusanyaji wa fedha za Usafi Mitaani.
Wakati wa kampeni mwaka jana, Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema alimtaka Meya wa Jiji ndugu Kalist Lazaro kueleza mikakati ya kuliweka jiji katika hali ya usafi, naye alijibu kuwa ameshafanya yafuatayo mbele ya makada maarufu wa Chadema; Edward Lowasa na Frederick Sumaye.
*Jiji la Arusha lina magari matatu ya kuzoa taka.
*Jiji limeshaajiri vijana wa kutosha kwa ajili ya kufanya usafi na wanalipwa na jiji.
*Jiji limeshanunua vifaa vya kutosha vya kufanya usafi.
HALI IKAWAJE BAADA YA
UCHAGUZI.
Fedha zimekuwa zinakusanywa kati ya tshs 1,000 hadi tshs 5,000 kwa kila mpangaji, kwa kila mwezi kwa ajili ya kuzoelea taka zinazokusanywa na wananchi baada ya kufanya usafi kwenye maeneo yao. Fedha hizo hukusanywa na watu ambao huambatana na migambo ili kurahisisha ukusanyaji. Wakati wa ukusanyaji, risiti zenye nembo ya jiji hutolewa. Sasa haijulikani kama zinatoka Jiji ama wanatengeneza wenyewe na kuweka nembo ya Jiji.
UFISADI UNAOFANYIKA.
Mfano chukulia mtaa wenye wapangaji 5,000 mara tsh 2,000 unapata Tshs 10,000,000/= kwa mwezi ambapo matumizi yake ni kwamba gari la kuzoa taka hukodishwa na kwa gharama za haraka hazizidi Tshs 100,000/= kwa trip kwani taka huchukuliwa asubuhi na
mapema kabla ya saa mbili za asubuhi ili wabebe chache maana muda huo watu wengi wanakuwa hawajatoa taka na hawawezi kuzikusanya nje siku inayotangulia kwani husambazwa na wanyama kama mbuzi na mbwa na hufanyika mara moja kwa
wiki na mara 4 kwa mwezi hivyo kwa mwezi hutumia Tshs 400,000 kuzoa taka,
sasa jiulize hizo nyingine huenda wapi?
Wiki mbili zilizopita katika mkutano wa wananchi na watendaji wa mtaa wao, ulivunjika baada ya mwananchi mmoja kutaka kujua mapato na matumizi ya fedha za taka, sambamba na mwingine aliyependekeza fedha zinazokusanywa kupitia vitabu, ni bora
zikakusanywa kwa kutumia EFD za TRA lakini walinyamazishwa haraka sana kwa kuwazima na jibu kwamba watu hawatoi pesa.
Jiji la Arusha lina kata 25 ila mitaa sijajua ni mingapi. Ila tuchukulie lina mitaa 50 mara
wapangaji 5,000 mara tshs 2,000/= unapata zaidi ya tshs 500Milion kwa mwezi. Huu ni
mradi haramu wa madiwani, watendaji wa mitaa pamoja na watu wengine na ndiyo maana ni kosa la jinai kuhoji mapato na matumizi yake.
Kuna wakati watu wa Afya wakiambatana na kikosi kazi huvamia tu watu na wakikuta
mazingira ni machafu, huwatisha hadi watoe hela kati ya tsh 10,000 hadi tsh 50,000 na wasipotoa hupelekwa kwa mtendaji hadi utoe.
NI VEMA SERIKALI IKASITISHA MRADI HUU HARAMU KWA WANANCHI NA KUTUMIA
MAGARI YA JIJI KUKUSANYA TAKA, AMA ZITUMIKE RISITI ZA EFD ZA TRA BADALA YA VITABU VINAVYOTUMIKA.