Ufisadi wa EPA, Richmond wadhalilisha Watanzania Marekani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi wa EPA, Richmond wadhalilisha Watanzania Marekani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nikifufukammekwisha, Apr 5, 2008.

 1. Nikifufukammekwisha

  Nikifufukammekwisha JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2008
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Who is this guy? Why did he do this & under what capacity? Is he the "de-facto spokesperson" for Tanzanians living in the US? Aliwakusanya akina nani na kukusanya maoni yao halafu baadaye kuyapeleka uko Mwananchi? Anafanya kazi ubalozini?

  Mimi naichukulia hii kitu kama ni "kujikweza kusiko na maana yoyote". I suggest aachane na kujitafutia "cheap publicity at the expense of Tanzanians living in the US.

  Sasa kaanza kupost articles kwenye gazeti la Mwananchi kutoa mawazo-wakilishi. Did the Tanzanians living in the US vested him with such powers?  link: http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=5303

  Mwananchi
  Habari za kawaida
  Posted Date::4/3/2008

  Ufisadi wa EPA, Richmond wadhalilisha Watanzania Marekani
  Na James Magai  BAADHI ya Watanzania wanaoishi Marekani, wamesema kashfa ya ufisadi iliyoibuka Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) na Kampuni ya Kuzalisha Umeme wa dharura ya Richmond Development Company LLC, imewadhalilisha.

  Katika barua pepe aliyotuma kwa Mwananchi kutoka Jimbo la Carolina kwa niaba ya wenzake, John Mashaka alisema, kutokana na kashifa hizo, wamekuwa wakijiuliza kama wahusika ni wazawa au majambazi kutoka nchi za nje.

  Mashaka alisema kutokana na hali hiyo, lazima wahusika wote wakamatwe na isipofanyika hivyo, itakuwa ni kejeli na matusi makubwa kwa walimu, polisi na wafanyakazi wengine wanaofanya kazi katika mazingira magumu.

  Ni jambo la kusikitisha na kutoa machozi, unapowaona watu wachache waliopewa dhamana ya kulinda nchi, wanajaribu kuifilisi na kuchezea jasho la Watanzania wengi, huku watoto wakifa hospitalini kwa kukosa tiba, alisema Mashaka.

  Kuhusu ufisadi, Mashaka alisema unasababishwa na watu kukosa uzalendo na kufanya uamuzi ambao hauna maslahi kwa Watanzania.

  Mtu mwenye ubinadamu katika nafsi yake na mwenye uzalendo na uchungu kwa nchi yake, kamwe hawezi kushiriki vitendo vya aibu kama vile vya Richmond na BoT, alisema Mashaka.

  Akitoa mfano wa Israel, Mashaka alisema nchi hiyo ina uwezo mkubwa kitaaluma kuliko mataifa makubwa yenye uwezo wa uchumi, kutokana na viongozi wake kutanguliza maslahi ya taifa mbele.

  Mashaka alisema, Watanazania waishio Marekani, wameridhika na juhudi za Rais Jakaya Kikwete kuboresha maisha ya wananchi na kuweka Tanzania katika ramani nzuri.

  Pia, alielezea kuridhishwa na jinsi wabunge wa chama tawala na vyama vya upinzani, walivyoungana na kushirikiana katika sakata la Richmond na kufanikiwa kuwang'oa mafisadi.

  Licha ya ufisadi, Mashaka alisema wamefurahishwa na juhudi za serikali kutangaza Tanzania kimataifa hasa vivutio vikubwa vya utalii vilivyopo nchini.
   
 2. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  HApa hakuna kosa labda utwambie ndio umefufuka sasa!!
  Kwani kuna kosa gani yeye kusema kuwa watanzania wanaohishi USA hawajafurahiswa na mwenendo halisi wa mambo ndani ya TZ, kwani ni uwongo, kama mpo ambao mnafurahia basi ni wale msiokuwa na upendo na nchi yetu
  Ila ukweli ni kuwa waTZ kibao hatuna imani na serikali yetu na ndo hivyo ukweli ulivyo
   
 3. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Mkuu hapa hakuna kosa lolote swala la EPA na Richmond ni kutudhalilisha kabisa watanzania. Hili suala limezagaa dunia Nzima katika hali ambayo huwezi kuamini.

  Hili litafanya hata watu wenye vibarua vinavyoeleweka waanze kuwekewa ulakini kwamba watanzania ndivyo walivyo. Hili suala siyo la kutafuta sijui nani kasema nini?

  Nafikiri hata JK kama Rais wa nchi anaweza kusema maswala haya yamemdalilisha sana pamoja na kwamba yeye anaouwezo na ndiye mwenye dhamana ya kuiondoa nchi yake katika matope haya.

  Mashaka kama mtanzania na ninyojua anayohaki ya kusema amedhalilika.

  Mkuu ni watanzania wachache na walio uhusiano na wahusika ndo wanapendezwa na suala hili.
   
 4. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  jamani kibanda kinawaka katika hoja binafsi !
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Haina haja ya kuwakusanya waTz uwajue wanahisia gani na ufisadi uliofanywa na Serikali za CCM,ikiwa utakusanya mawazo kwa kusikiliza tu mazungumzoni bila kuuliza utajua na kupata suluhisho kuwa WaTanzania hawakufurahishwa na ubadhirifu uliotokea na zaidi hata hatua zinazochukuliwa hazijawaonyesha au hazijawaridhisha WaTanzania ili liwe somo na fundisho kwa wengine.
  CCM inafahamu wazi kuwakamata na kuwafunga vigogo wa ufisadi ni kukipunguzia Chama chao nguvu ya wapiga kura kwani inaamini ,wakiwakamata na kuwafunga basi inaweza kupoteza jimbo zima.Hivyo ni bora wawemo na kuhangaika nao hivyo hivyo liwalo na liwe lakini hafukuzwi wala hafungwi mtu watahamishana tu.
   
 6. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  His intentions are in RED... aonekane anatoa sifa kwa Serikali! Duh...tricky guy!

  Anyway nadhani angesikitishwa zaidi na kitendo cha Balali kuendelea kuishi Marekani wakati anastahili kuwepo bongo ili kuisaidia timu ya JK kupata ukweli halisi wa jinsi 133b zilivofisadiwa na makampuni hewa wakishirikiana na BOT!!!
   
 7. M

  Mutu JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Hakuna tatizo kama amesema baadhi ya wa bongo waishio USA kwa kuwa haimaanishi wote kwenye red color.

  Kwa kifupi wanaposema watanzaia wanachukizwa/kupendezwa na kitu fulani haijawahi hata siku moja kuwa wote ndio maana hakuna ideal statistic .Kwa hiyo kama bwana Mashaka alikuwa na ujumbe wa watu fulani Basi sawa.

  Ila kama bwana J.Mashaka hakuhusisha kikundi fulani cha watu wa TZ waishio USA hasa hapo Carolina basi madai yako yatakuwa sahihi mkuu.
  Kwenye rangi ya lime sidhani kama rais JK ameboresha maisha ya watanzani bwana J.Mashaka!!Bali unaweza sema anaimba maisha bora kwa kila mtanzania.
  Mimi anachonitia shaka huyu bwana J.Mashaka ni kwamba amedai kuwa anafanya kazi Wall st. na mimi nafahamu ipo down Town Manhattan(A street in lower Manhattan that is the original home of the New York Stock Exchange),hapa yeye anadai amewakilisha wa Tz wakazi Carolina (sijui south or North Carolina haijatajwa) Swali langu je Carolina kuna Wall st pia?Kama ipo bwana J.Mashaka atakuwa kanitoa shaka langu.And if so you should specify that.
   
Loading...