Ufisadi Tumaini university

Inkognito

Member
Feb 13, 2011
86
108
Wanafunzi wa chuo Tumaini kampus ya Iringa wameibua ufisadi uliokuwa ukifanywa na Rais wa serikali ya wanafunzi ambaye ni kada wa ccm.
Tukio hilo limetokea leo mchana na kusababisha vurugu zilizopelekea kuitwa kwa askari wa kutuliza ghasia.
Rais huyo wa anatuhumiwa kwa kuzifanyia ufisadi fedha za wanafunzi kwa kujinunulia gari pamoja na kufungua mgahawa karibu na maeneo ya chuo
Utata ulianzia katika kikao cha baraza la mawaziri,wabunge na wawakilishi kutoka vitizo mbalimbali baafa ya kuhoji mapato na matumizi ambapo baada ya kumbana rais huyo alikiri kufanyika kwa ufisadi huo huku waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi akitoa ushahidi mzito kuonesha namna rais huyo alivyofanya ufisadi huo
Rais huyo alipotakiwa kujiuzuru alikataa hali iliyosababisha kutokea kwa mvutano uliopelekea kuvunjika kwa kikao na wajumbe wa kikao hicho wakatoka nje kuwataarifu wanafunzi kile kilichojili.
Baada ya wanafunzi kupata taarifa hizo walionekana kukerwa na matendo ya rais huyo na kuchukua maamuzi ya kumnyang'anya rais huyo funguo za ofisi,kuvunja mgahawa na kupora vitu huku wengine wakiendelea kulisaka gari lake ili walichome moto.
Wanafunzi wengi wanaonekana kumuunga mkono waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi ambaye ana itikadi za people's power
 
Back
Top Bottom