Ufisadi Ofic ya mikopo ya wanafunzi UDOM

KWETU PAZURI

Senior Member
Oct 14, 2011
161
26
Nyaraka zinaonyesha bodi ya mikopo ilikabidhi fedha za wanafunzi kwa chuo tarehe 16/12/2011, lakini hadi leo hii wanafunzi hawajapewa fedha zao
 
yaani mpaka sasa hivi bado hawajaingiziwa boom poleni sana hii ndio tz kila mtu ni corrupt ajuavyo yeye
 
Mlacha kazipeleka kwenye sekondari yake, pumulieni mashine vijana, ndo madhara ya ushemeji na JK
 
Afadhali kwanza sikukuu zpite maana mngesu mjini na viela vya mkopo, kwanza mungeishiwa mapema na hizi sikukuu. bora
 
Poleni sana vijana,Udom kuna mafisadi ya kufa mtu hapo yaani madhara ya undugunaizeshi unaimaliza hii nji,tizama sie tulio graduate Nov ile chenchi yetu ya kwenye Majoho mpaka muda huu hawajatuingizia ni wezi wakubwa hao
 
hii ndio taabu ya kuwa na viongozi wasiowajibika kama form zinaonesha hela imeshalipwa toka tarehe tajwa inakuaje viongozi wasifuatilie hela zimepelekwa?
 
yani..tuliiambia wizara kwamba huu sio mpango mzuri lakini tunaonekana wakorofi tu!na ukienda loanboard kufuatilia wanakurudisha chuo-despite the fact you are the official representative-eg minister for loans!na huku chuo-kama huna 'intel' ya lini majina yamekuja ndo unakuwa unazungushwa tu kwenda loan board!kama kimpira!!!
 
Afadhali kwanza sikukuu zpite maana mngesu mjini na viela vya mkopo, kwanza mungeishiwa mapema na hizi sikukuu. bora

Kuchelewesha fedha sio tiba ya kuishiwa mapema kwani watakapopata tu, sehemu yake itatumika kulipa madeni waliyokopa.
 
kwa nini pesa itoke bodi iende chuoni? kwa nini isiende moja kwa moja kwa mwanafunzi? pesa klazima ichelewa kwa sababu
1.watanzania ni wavivu sanaaaaaa makazini ..na hakuna mtyu wa kukemea hili hasa wafanyakazi wa serikalini.
2.pesa ikitoka pale bodi lazima ichukue mda mrefu kuhakikiwa majina ya wanafunzi wote kila mmoja mmoja ..kwa hiyo unaweza kwa siku wanahakikiwa wanafunzi watano au kumi ..si mnajua watu walivyo wavivu kazini?
3.pesa ikitoka pale bodi iingie benki benki nazo mnajua usharobaro wao ....mtjaza hapa wenyewe.
4.zifike dodoma waanze nao kuwahakiki ..lol !! unafikiri hapa inachukua muda gani? au hamjui wafanyakazi wa serikalini walivyo na nyodo na kujivuta vuta?..Pesa kama vipi ikitoka bodo iingie kwenye account ya mwanafunzi moja kwa moja ..bila hivyo mtakuwa mnaipata pesa yenu kila siku ikiwa imechelewa sana
 
Back
Top Bottom