Ufisadi mwingine bungeni

Ufisadi mwingine bungeni

babykailama

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2012
Posts
251
Reaction score
243
Kuzimisha mitambo ya Television au Radio kwa makusudi ili Wananchi wasisikie na kuona yale yanayoendelea Bungeni ambayo ni haki yao kama tulivyokubaliana ni ufisadi mkubwa unaotupaka matope Bunge lote kuwa sisi ni mawakala wa kutoa ukimbizi kwa mafisadi wanapotaka kuumbuliwa. Wabunge lazima tujitofautishe na watendaji wa Bunge na TBC wanaoshirikiana kuleta hujua za namna hii na kama wameshindwa kazi basi wapewe wengine maana wasomi wenye sifa hizo wapo wengi sana.
Kwa mujibu wa wa ibara 87 na 88 ya Katiba ya JMT, yupo Karani wa Bunge (CEO) na Sekretariet ya Bunge ambao wanatakiwa kuhakikisha kuwa shughuli za Bunge zinafanyika kwa kiwango cha juu na bila mapungufu yasiyo ya lazima kwa Bunge na kwa Wananchi kwa ujumla.

Ilisha kubalika kuwa shughuli za vikao vya Bunge zionyeshwe ‘live’ kwa Wananchi kupitia Televisheni ya Taifa (TBC). Kwamba Wananchi wanaostahili kupata taarifa hizi ndio Waajiri wakuu wa Wabunge wote, Karani wa Bunge na timu yake na hata Mkurugenzi Mkuu wa TBC maana wote wanalipwa mishahara yao tokana na kodi za Wananchi.

Cha kusikitisha, kumekuwa na matukio ya ajabu na yasiyovumilika ya matangazo ya TBC ya vikao vya Bunge kukatishwa ghafla hususani pale ambapo kuna hoja yenye vuguvugu kama ile ya leo iliyokuwa inajadili wezi wakubwa wa rasilimali za nchi yetu. Cha ajabu zaidi, pindi matangazo yanaporejeshwa hata wananchi hawaombwi msamaha wala kuelezwa chochote cha maana kama kisababishi. Hii pia hutokea katika mikutano ya kisiasa au mihadhara mbalimbali ambapo kabla mtu anayejulikana kuwa shujaa kuweza kusema yale ambayo wengine hawawezi kuyasema hadharani basi ‘hukatiwa line’asisikike na wananchi wasijue kinachoendelea. Aidha hatuwezi pia kukubaliana na fikra kuwa ni umeme huwa ndio kisababishi maana hata kama TANESCO wangepatwa na tatizo, Bunge ‘tukufu’na hata Shirika kubwa la Taifa - TBC wenyewe wanatakiwa kuwa na auto -standby generators hata tatu kubwa na nzuri zinazoweza kufanya kazi ya kutoa nishati ndani ya dakika moja ili kutoathiri shughuli za Bunge au matangazo yake yanayooneshwa moja kwa moja kwa Waajiri wetu.

Kwa vile niliomba nafasi ya kuwasilisha hoja binafsi na sikupewa, basi nakukabidhi Rais wetu wa nchi hoja hii moja kwa moja maana Mawaziri wako wenye dhamana wameshindwa na ni wewe unayemteua Karani wa Bunge na Watendaji wengine wakuu wa asasi za umma kama TBC na TANESCO ili hatua kali zichukuliwe kwa: Karani wa Bunge Dr. Kashililah na Mkurugenzi wake wa Mipango, Habari na TEHAMA ndg. Kuwite, na Mkurugenzi Mkuu TBC ndg. Mshana na Meneja wake Mkuu wa Ufundi ndg. Abenego.

Hii iwe fundisho si tu kwa Bunge na TBC bali vyombo vyote nya habari maana mnawajibika kwa umma pia. Hamuwezi kuendelea kuwa mnawachagulia wananchi habari zinazowafurahisha baadhi ya watu na zile zinazogusa maisha ya raia wa chini mnazificha! Bibi yangu aliyekimbia kuketi kitako amsikilize Mheshimiwa T. Lissu akichawambua wezi wanaofanya maisha yetu kuwa magumu, karibu apatwe na mshituko wa moyo mara ghafla matangazo ya TBC yalipotoweka asijue cha kufanya! Inauma sana! Wanahabari wote wazalendo lazima muwe washiriki wakubwa wa kupambana na rushwa kwa kuhakikisha kuwa wananchi wanapata habari kamili na za uhakika.
 
We jembe ndugu, JK amesikia uongozi wa bunge dr. thommy na kuwite wamekusikia na mwisho viongozi wa hayati TBC pia pia wamesikia
 
Mkuu inamaana na leo wamefanya uhuni kam huu TBC1? na kwa muda gani kabla ya kurusha tena matangazo? sahani kukuliza swali hili siko tanzania at the moment na sina access na TV
 
Huyu Mpare Mshana amekuja kuiua TBC,anyway watabaki wanaangalia wao na familia zao! Sisi wengine tupo ITV na STAR TV siku nyingi,Hivi niulize kumbe TBC bado ipo?
 
...Lakini pia imenishangaza kuwa Hakuna hata Redio Moja iliyokuwa Inarusha 1 kwa 1 Matangazo ya Shughuli za Bunge Leo ambazo Zilikuwa na Umuhimu wa Pekee! Hili nalo Limekaaje????? Mbona hawa Waheshimiwa wanatuona M.a.Bwe.gE hivi na siTumenyamaza Tu...?????
 
Hali hii itarekebika mara tu upinzani utakapochukua nchi. Kilichopo ni kuhakikisha kuwa upinzani unakuwa juu. Angalia yaliyomtokea Tido na Kisu
 
Kuzimisha mitambo ya Television au Radio kwa makusudi ili Wananchi wasisikie na kuona yale yanayoendelea Bungeni ambayo ni haki yao kama tulivyokubaliana ni ufisadi mkubwa unaotupaka matope Bunge lote kuwa sisi ni mawakala wa kutoa ukimbizi kwa mafisadi wanapotaka kuumbuliwa. Wabunge lazima tujitofautishe na watendaji wa Bunge na TBC wanaoshirikiana kuleta hujua za namna hii na kama wameshindwa kazi basi wapewe wengine maana wasomi wenye sifa hizo wapo wengi sana.
Kwa mujibu wa wa ibara 87 na 88 ya Katiba ya JMT, yupo Karani wa Bunge (CEO) na Sekretariet ya Bunge ambao wanatakiwa kuhakikisha kuwa shughuli za Bunge zinafanyika kwa kiwango cha juu na bila mapungufu yasiyo ya lazima kwa Bunge na kwa Wananchi kwa ujumla.

Ilisha kubalika kuwa shughuli za vikao vya Bunge zionyeshwe ‘live' kwa Wananchi kupitia Televisheni ya Taifa (TBC). Kwamba Wananchi wanaostahili kupata taarifa hizi ndio Waajiri wakuu wa Wabunge wote, Karani wa Bunge na timu yake na hata Mkurugenzi Mkuu wa TBC maana wote wanalipwa mishahara yao tokana na kodi za Wananchi.

Cha kusikitisha, kumekuwa na matukio ya ajabu na yasiyovumilika ya matangazo ya TBC ya vikao vya Bunge kukatishwa ghafla hususani pale ambapo kuna hoja yenye vuguvugu kama ile ya leo iliyokuwa inajadili wezi wakubwa wa rasilimali za nchi yetu. Cha ajabu zaidi, pindi matangazo yanaporejeshwa hata wananchi hawaombwi msamaha wala kuelezwa chochote cha maana kama kisababishi. Hii pia hutokea katika mikutano ya kisiasa au mihadhara mbalimbali ambapo kabla mtu anayejulikana kuwa shujaa kuweza kusema yale ambayo wengine hawawezi kuyasema hadharani basi ‘hukatiwa line'asisikike na wananchi wasijue kinachoendelea. Aidha hatuwezi pia kukubaliana na fikra kuwa ni umeme huwa ndio kisababishi maana hata kama TANESCO wangepatwa na tatizo, Bunge ‘tukufu'na hata Shirika kubwa la Taifa - TBC wenyewe wanatakiwa kuwa na auto -standby generators hata tatu kubwa na nzuri zinazoweza kufanya kazi ya kutoa nishati ndani ya dakika moja ili kutoathiri shughuli za Bunge au matangazo yake yanayooneshwa moja kwa moja kwa Waajiri wetu.

Kwa vile niliomba nafasi ya kuwasilisha hoja binafsi na sikupewa, basi nakukabidhi Rais wetu wa nchi hoja hii moja kwa moja maana Mawaziri wako wenye dhamana wameshindwa na ni wewe unayemteua Karani wa Bunge na Watendaji wengine wakuu wa asasi za umma kama TBC na TANESCO ili hatua kali zichukuliwe kwa: Karani wa Bunge Dr. Kashililah na Mkurugenzi wake wa Mipango, Habari na TEHAMA ndg. Kuwite, na Mkurugenzi Mkuu TBC ndg. Mshana na Meneja wake Mkuu wa Ufundi ndg. Abenego.

Hii iwe fundisho si tu kwa Bunge na TBC bali vyombo vyote nya habari maana mnawajibika kwa umma pia. Hamuwezi kuendelea kuwa mnawachagulia wananchi habari zinazowafurahisha baadhi ya watu na zile zinazogusa maisha ya raia wa chini mnazificha! Bibi yangu aliyekimbia kuketi kitako amsikilize Mheshimiwa T. Lissu akichawambua wezi wanaofanya maisha yetu kuwa magumu, karibu apatwe na mshituko wa moyo mara ghafla matangazo ya TBC yalipotoweka asijue cha kufanya! Inauma sana! Wanahabari wote wazalendo lazima muwe washiriki wakubwa wa kupambana na rushwa kwa kuhakikisha kuwa wananchi wanapata habari kamili na za uhakika.

Mwisho wa SISIM unakuja tu hata waafanyaje!!!!! Kadiri wanavyofanya haya ndio sisi wananchi tunazidisha hasira zetu kwa Serikali ya SISIM. Pia TBC wanaoshirikiana kuleta hujuma za namna hii mimi binafsi nimeshaacha kuangalia TBC toka wamfukuze Tido Mhando.
 
Back
Top Bottom