Kwa miaka 3 sasa shule za wazazi-CCM zimekuwa zikifanya mitihani ya kitaifa. Zoezi hili limekuwa na ufanisi na limezirudisha shule za CCM kwenye ufaulu mzuri.
Hata hivyo kuondoka kwa Katibu Mkuu, Gilbert Kalima kumekuwa pigo kubwa sana kwa shule za wazazi na CCM. kwa sasa shule zimebakia Yatima.
Mitihani hii imeingiliwa na fedha inaliwa na wajumbe wa kamati ya mitihani, inayosimamiwa na Mkuu wa Shule ya Sangu.
Baada ya wakuu wa shule kuchangia gharama zote za mitihani, fedha imeliwa na sasa wakuu wamelazimishwa kuchangia fedha nyingine nje ya bajeti. Wakati mitihani huchapishwa Victoria stationary pale Dodoma na hugharimu kama milioni 6, mwaka huu imechapishwa katika chuo cha Mipango bure, lakini gharama zimetajwa kuwa zilezile kama ambazo huwa zinalipwa Victoria Stationary.
Na sasa wakuu wa shule tunatishwa kulipa fedha nyingine. Fedha hizi huwa zinachangwa na wazazi wa wanafunzi moja kwa moja.
Mkuu wa shule anatoa wapi fedha kuongezea ili kamati wale fedha?
Uratibu wa zoezi la mitihani umekuwa mbovu kuwahi kutokea. Mpaka leo tarehe 7 Oktoba usahihishaji mitihani hauaanza. Izingatiwe mitihani ya taifa ya kidato cha pili inaanza tarehe 28 oktoba. Mitihani ya wazazi itakuwa na maana gani ikiwa mpaka sasa haijasahihishwa?
Nimalizie kwa kuziomba mamlaka za Chama cha Mapinduzi kuingilia haraka kuokoa zoezi la mitihani hii na kuchunguza ufisadi mkubwa unaofanywa na Kamati hiyo na wanaomsaidia makao makuu ya wazazi.
Wakuu wa shule hatufurahishwi na kuchangishwa fedha kwa ajili ya kusafirisha walimu wanaokwenda kusahihisha mitihani Dodoma wakati tulikwisha toa fedha hizo tayari.