Ufisadi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Kimweri2012, Jun 4, 2012.

 1. K

  Kimweri2012 New Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UFISADI MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO UNATISHA

  PAMOJA NA MALENGO (MISSION) MENGINE YA NCAA LENGO MOJAWAPO NI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA UTALII ILI KUBORESHA HUDUMA ZA KITALII (TO PROVIDE HIGH QUALITY TOURISM SERVICES) KWA KUTEGENEZA BARABARA KWENDA KWENYE VIVUTIO KAMA NASERA ROCK ,OLKARIAN GORGE NA AINA MBALIMBALI ZA MIUNDOMBINU YA UTALII NA SIYO KUFANYA KAZI ZA TTB (TANZANI TOURISM BOARD).

  KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO AMBACHO BODI YA WAKURUNGENZI YA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO CHINI YA UONGOZI WA MHESHIMIWA MSEKWA KIASI CHA ZAIDI YA TSHS. BILIONI 15 (WASTANI WA ASILIMIA 10% YA FEDHA ZILIZOKUSANYWA KWA MWAKA) ZILITUMIKA KWA AJILI YA SAFARI ZA KUTANGAZA UTALII ZIKILIPWA KWA WAKURUGENZI , HAYA NI MATUMIZI MABAYA YA FEDHA KWANI UTANGAZAJI WA AINA HII HAUNA TIJA KATIKA KUKUZA UTALII KAMA ILIVYO ONYESHWA NA MTAALAM WA UTALII DR.VICTOR RUNYORO KATIKA UTAFITI WAKE ALIPO SEMA HAKUNA UHUSIANO WA MOJA KWA MOJA WA WATALII KUJA NCHI NA SAFARI ZILIZOFANYWA NA MALAKA ("Market strategies employed by TTB and other Government Institutions in Tanzania including NCAA had shown no obvious impacts").

  THE QUETION IS WHY NCAA STILL USE SUCH AMOUNT OF MONEY NOTWITHSTANDING THE FACT THAT NO VALUE FOR MONEY. UTALII HUTEGEWA 14% WAKATI MAJUKUMU MENGINE YANATEGEWA; UHIFADHI 7% NA MAENDELEO YA JAMII 10%. HIVYO HUU NI UFISADI NA MATUMIZI MABAYA YA RASILIMALI FEDHA KWA KUTEGA 10% KWA SAFARI ZA NJE PEKEE, KUONYESHA KWAMBA FEDHA ZA KUTANGAZA UTALII NA ZINGINE HAZINA USIMAMIZI NA HUTUMIKA KUNUFAISHA WATU BINAFSI, WAKURUGENZI NA MAOFISA WANAO HUSIKA NA MPANGO HUO HUJIPATIA WASTANI WA Tshs.30, 000,000 milioni KWA MWAKA. MENEJA ANAYE HUSIKA NA HUDUMA ZA UTALII BI .VERONICA UFUNGUO ALIWEZA KUJICHOTEA ZAIDI YA BILIONI MOJA KWENYE VOTE NO.700905-100 KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI TANGU AWE MENEJA HIVYO KUMILIKI MAGARI ZAIDI YA MAWILI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA TSHS.MILIONI 300 NA NYUMBA YENYE THAMANI YA ZAIDI YA TSHS. MILIONI 400 MAENEO YA NJIRO ARUSHA.

  HADI LEO HII HAKUNA BARABARA ZA KWENDA KWENYE VIVUTIO KAMA NDUTU, ORKERIANI NA NASERA ROCK KWA SABABU YA UKOSEFU WA FEDHA LAKINI BODI ILIRUHUSU MATUMIZI YA ZIADA (OVER EXPENDITURE) YA TSHS.692, 000,000TSHS KWA AJILI YA TOURISM EXHIBITIONS MWAKA 2011-2012 BAADA YA ZAIDI YA BILIONI 3 ZILIZOPANGWA KUTUMIKA KUTOKUTOSHELEZA KUGAWANA. INASHAGAZA KWANI TANGU BODI HII ILIPOIGIA HAKUNA GARI LA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA WA ENEO LILILONUNULIWA,YOTE YANAZAIDI YA MIAKA 10 HIVYO KUNA UHABA WA VITENDEA KAZI KATIKA IDARA YA UHIFADHI. WAJUMBE WA BODI WAMEKUWA WANAENDA ZIARA ZA KIMAFUNZO NA SAFARI ZA KUTANGAZA UTALII AMBAZO KIMSINGI WALITAKIWA WATENDAJI NDIYO WAENDE HIVYO PESA NYINGI KUTUMIKA BILA TIJA KWENYE UTENDAJI(OPERATIONAL EXPENDITURE).

  KWA MFANO KATI YA TAREHE 29.04.2012 HADI 4.06.2012 OFISI ZA NGORONGORO ZILIKUWA WAZI MENEJIMENTI (MANEGERS) WALIKUWA SAFARI NJE YA OFISI NA ZIARA MBALIMBALI ZENYE LENGO LA KUJIKUSANYIA FEDHA BILA KUJALI SHUGHULI ZINGINE ZA OFISI ZITAFANYWA NA NANI.MANAGERS HUONEKANA OFISINI ILI KUCHUKUA MALIPO MENGINE NA KUONDOKA.

  HII IMEPELEKEA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA NA MAGARI ; WAKUU WA IDARA AMBAO WANATUMIA FEDHA ZILIZOTENGWA KWENYE BAJETI ZA IDARA ZAO KAMA MALI YAO BINAFSI WAMEWEZA KUJINUFAISHA KADIRI WALIVYOTAKA NA WASHIRIKI WAO. HII NI KUTOKANA NA MENEJIMETI KUAMUA KUJICHUKULIA CHAO MAPEMA KWA KUWA BODI IMEKOSA UWEZO WA KUDHIBITI MAPATO NA MATUMIZI YA SHIRIKA KWANI NAO WANAHUSIKA KWENYE UFISADI KUPITIA VIKAO VYA DHARURA VYA MARA KWA MARA, ZIARA ZA KAMATI ZA BODI ZA MARA KWA MARA PAMOJA NA SAFARI ZISIZOKUWA ZA KUTANGAZA UTALII NJE YA NCHI ZISIZOKUWA NA TIJA KWANI KILA MKURUNGENZI HUPANGIWA SAFARI TATU (3) NA MWENYEKITI SAFARI NNE (4) KWENDA NCHI ATAKAYO ICHANGUA KWAKILA MWAKA WA FEDHA. KILA MKUU WA IDARA HUTUMIA GARI LA SHIRIKA KAMA MALI YAKE BINAFSI KWA SHUGHULI ZAKE BINAFSI BILA KUIGILIWA NA MTU; MFANO KILA MWISHO WA WIKI WAKUU WA IDARA HUONDOKA NGORONGORO KWENDA KUONA FAMILIA ZAO ZILIZOPO ARUSHA KWA KUTUMIA MAGARI YA UMMA, MAFUTA NA KUJILIPA PAMOJA NA DREVA POSHO ZA KUJIKIMU,KWA WASTANI GARI MOJA HUTUMIA MAFUTA YA 100,000/= KILA WIKI ,POSHO KWA WAKUU WA IDARA NI WASTANI WA 160,000*12 NA MADREVA 105,000 *12.

  HII NI KUSEMA KWAMBA WAKUU WA IDARA ZAIDI YA TSHS500,000,000 HUTUMIKA KUWALIPA KWENDA KUONA FAMILIA ZAO NA KUTUMIA MAGARI YA SHIRIKA AMBAYO HUGHARIMU MAFUTA YA ZAIDI YA MILIONI 400. HATIMAYE PIUS MSEKWA ALIKUBALI KWA SHINGO UPANDE KUSTAAFU KWA BWANA MRUNYA BENARD BAADA KUSHIRIKIANA KWENYE UFISADI KWA ZAIDI YA MIAKA MINNE, LAKINI CHA AJABU NI KULE KUKAIMISHA OFISI YA MHIFADHI MKUU WA NGORONGORO KWA BWANA SHADDY KIAMBILE AMBAYE NI MKURUNGENZI WA FEDHA NA UTAWALA AMBAYE AKIWA MSIMAMIZI MKUU WA MAPATO NA MATUMIZI ALICHUKUA MKOPO KWA NIABA MAMLAKA KWENYE BENKI YA NBC WA TSHS. 800, 000,000. NA OVERDRAFT YA ZAIDI YA TSHS.16,000,000,000 KWENYE BENKI YA EXIM BILA KUFUATA KANUNI ZA FEDHA KWA AJILI YA SHUGHULI ZA KAWAIDA KAMA KUSAFIRI NJE YA NCHI NA KULIPA MISHAHARA.

  MAMBO HAYA YALIFANYAKA BILA KUJADILIWA NA MENEJIMENTI, KIBALI CHA BODI WALA WIZARA KAMA ILIVYO DHIBITISHWA NA TAARIFA ZA WAKAGUZI WA NJE (EXTERNAL AUDITORS) ZILIONYESHA UKWELI NI KWAMBA MSEKWA AMEKUWA AKIINGILIA SHUGHULI ZA UTENDAJI WA KILA SIKU WA HIFADHI KIASI CHA KUIFANYA MENEJIMENTI KUKOSA MAAMUZI (RENDUNDANT ) ILI KUFANIWA ALIMSHAWISHI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUMTEUA BWANA MRUNYA AMBAYE KWA JAMII Y A WATAAM WA UHIFADHI HAKUWA NA SIFA HATA MOJA KUIONGOZA MAMLAKA(INCOMPETENT) LAKINI ALIWEKWA ILI KULINDA UKIRITIMBA NA UBWENYENYE KUMWEZESHA KUINGILIA UTENDAJI WA HIFADHI KWENYE MAENEO KAMA!

  • KUGAWA MAENEO YA UJENZI WA MAHOTELI
  • UPITISHWAJI WA TENDER KUBWA KAMA ZA BARABARA, UNUNUZI WA MAGARI NA MITAMBO.
  • MIKATABA YA MAHOTELI NA WADAU WENGINE ISIYO NA MASLAHI MAPANA KWA MAMLAKA YA HIFADHI.
  • MCHAKATO WA SHERIA MPYA YA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO
  • UHUISHAJI WA MPANGO MKAKATI (GMP) YA MAMLAKA YA NGORONGORO

  BWANA BENARD MRUNYA ALIPO LAZIMIKA KUSTAAFU KWA MUJIBU WA SHERIA, MHESHIMIWA MSEKWA ALITUMIA MADARAKA NA UZOEFU WAKE WA KUWEPO KWENYE UONGOZI WA NCHI KWANI AMEKUWANAKIJITAPA KWAMBA WAO NDIYO WENYE NCHI HIVYO HAKUNA WA KUMZUIA KUFANYA LOLOTE HIVYO KUFANIKISHA YAFUATAYO:
  • KUMPELEKA BWANA BENARD MRUNYA KWENYE UBUNGE WA AFRICA MASHARIKI ILI KULIPA FADHILA AKIJUA BAYANA HANA UWEZO WA KUWAKILISHA WATANZANIA KWENYE BUNGE HILO.ILI KUFANIKIWA FEDHA ZA MAMLAKA ZILITUMIKA KUFANYIA KAPEINI ILI WABUNGE WAMCHAGUE.
  • KUMKAIMISHA BWANA SHADDY KIAMBILE AMBAYE ALIKUWA MSHIRIKA MKUBWA WA BWANA MRUNYA ILI KUENDELEZA MTANDAO WA UFISADI WA KUKOPA FEDHA AMBAZO HAKUNA ANAYE JUA ZILIPELEKWA WAPI IGAWA KUNA TETESI KWAMBA ZILIDAIWA KUCHUKULIWA NA CCM KWA AJILI YA KAMPEINI ZA UCHAGUZI WA 2010 KWA MAELEKEZO YA MAKAMU MWENYEKITI AMBAYE PIA NI MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI.
  • PIUS MSEKWA ALIHAKIKISHA ZOEZI LA KUMTAFUTA MHIFADHI WA NGORONGORO LINAGUBIKWA NA MIZENGWE ILI KUHAKIKISHA ANALETWA MTU AMBAYE HAJUI HALI YA UFISADI ULIFAONYWA CHINI YA UONGOZI WA BODI YAKE.

  KITENDO CHA KUMWACHIA BWANA KIAMBILE SHADDY. KINASHAWISHI MTU YEYOTE KUAMINI KWAMBA MHESHIMIWA MSEKWA NA BODI YAKE WANA MASLAHI BINAFSI ILI KUENDELEA KUCHOTA FEDHA ZA SHIRIKA HASA KIPINDI WAKIWA WAMEBAKIZA MIEZI MITATU KUMALIZA KIPINDI CHA UHAI WA BODI.

  MFANO:
  FINANCIAL REGULATIONS REQUIRES DIRECTOR OF FINANCE, CHIEF ACCOUNTANT AND CONSERVATOR TO APPROVE LPO WHICH ARE CONTRACTUAL DOCUMENTS. HIVYO KWA SASA BWANA S.KIAMBILE NDIYE ANAYE APPROVES LPO KAMA DFA NA CONSERVATOR NA MHASIBU MWENZAKE??? JE LENGO NI NINI KAMA SIYO KUHUJUMU MAMLAKA YA NGORONGORO KUENDELEZA UFISADI NA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA UNAOFANYWA KWA BARAKA NA USHIRIKI WA MHESHIMIWA MSEKWA.

  WAZIRI WA MALIASILI NA UTALIII MHESHIMIWA KAGASHEKI UMEKABIDHIWA TAARIFA YA TUME YA JAJI MSTAAFU THOMASI MIHAYO ISHUGHULIKIE ILI KUINUSURU MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO IONDOKANE NA MTANDAO WA KIUHALIFU UNAO ONGOZWA NA KIONGOZI MBINAFSI ASIYE MWADILIFU LAKINI MWENYE UJASIRI WA KUDANGANYA UMMA WA WATANZANIA NA WAKIMATAIFA KWAMBA NI KIONGOZI WA KUIGWA NA KIZAZI CHA SASA NA KIJACHO.

  KWA MAONI YANGU MHESHIMIWA MSEKWA ATAKUMBUKWA NA WATANZANIA KAMA KIONGOZI HODARI WA KUZIMA HOJA ZENYE MASLAHI YA TAIFA KWENYE BUNGE NA NJE YA BUNGE AKIWA SPIKA WA BUNGE, MWENYEKITI WA BODI YA CHUO CHA USIMAMAZI WA WANYAMAPORI - MWEKA, MWENYEKITI WA BODI YA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO AMBAKO AMEKUWA AKIFANYA KAZI KAMA MWENYEKITI MTENDAJI NA SIYO WA VIKAO NA MFANO MZURI WA UTENDAJI WA OVYO USIOSTAHILI KUIGWA NA VIJANA WA TANZANIA PIA AKIWA MAKAMU WA CCM.

  NAOMBA NIMPONGEZE MHESHIMIWA SANING'O OLE TELELE MBUNGE WA NGORONGORO BILA KUUMA MANENO WALA KUJALI VITISHO VYA MAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA CHAKE ALISIMAMA NA KUELEZA UFISADI UNAENDELEZWA NA MHESHIMIWA MSEKWA KATIKA KUGAWA MAENEO YA MAMLAKA YA HIFADHI KWA WAWEKEZAJI BILA KUJALI USHAURI WA KITAALAMU NA KUIGILIA UTENDAJI WA KILA SIKU WA HIFADHI KAMA MWENYEKITI MTENDAJI.

  NAOMBA IELEWEKE KWAMBA MSEKWA NI AINA YA VIONGOZI WALIOJIZOLEA SIFA KWA KUTUMIA UNAFIKI, HILA, GILIBU, UJANJA NA USTADI KUWAHADAA, KUWAAMINISHA WATANZANIA KUWA NI LULU NA JOHARI YA UONGOZI KWA NUSU KARNE KUMBE NI CHANZO CHA OMBWE LA UONGOZI LIUNALO ENDELEA HAPA NCHINI, NDIYO MAANA ALIPATA UJASIRI WA KUSIMAMA KIDETE KUJITETEA KWAMBA HAJAWAHI KUTUMIA MADARAKA VIBAYA NA WATU WANAMWONEA WIVU, NI UNAFIKI NA UZADIKI WA HALI YA JUU!!

  KWA KIFUPI BWANA KIAMBILE KABLA YA KUJA NGORONGORO ALIKUWA BODI YA KAHAWA AKIFANYA KAZI KAMA MKURUGENZI WA FEDHA NA UTAWALA, ALISABABISHA KUFILISIKA KWA BODI HIYO NA KWA SASA BADO ANAKESI YA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA YA ZAIDI YA 300,000,000 TSHS. INAYOSIMAMIWA NA TAKUKURU. HIVYO HANA REKODI YA UTUMISHI WA KUTUKUKA KUWEZA KUKAIMISHWA KUWA KAIMU MHIFADHI WA NGORONGORO KWA MAZINGIRA YALIYOPO YA YEYE KUSIMAMIA MAPATO NA KUIDHINISHA MATUMIZI YA FEDHA ZA MAMLAKAI!!

  UTARATIBU HUU WA BODI KURUHUSU DFA KUKAIMU UMEIPOTEZEA MAMLAKA UWEZO WANDANI KUDHIBITI NA KUKINGA (INTERNAL PREVENTIVE CONTROLS) KWANI KWA SASA HAKUNA:
  ยทMGAWANYO WA KAZI(SEPARATION OF DUTIES)
  ยท
  UIDHINISHWAJI SAHIHI WA FEDHA (PROPER AUTHORIZATIONS).

  MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO KWASABABU YA UFISADI ULIOKOMAA MATABAKA MATATU YAMEJENGEKA:
  1.
  TABAKA LA UTAWALA LIKIJUMUISHA BODI NA MENEJIMETI.
  HAWA WANAGAWANA FEDHA ZINAZO PATIKANA KWANI HAKUNA WA KUWA ZUIA KUFANYA HIVYO WALA WA KUMWONGOPA KWANI MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ANAOGOPEWA NA VYOMBO VYA USIMAMIZI WA SHERIA KAMA PCCB NA VINGINE.TABAKA HILI NDIO LINALO NEEMEKA NA FEDHA ZA MAMLAKA KWA KUJILIPA POSHO KWA WAKURUGENZI PAMOJA NA MISHAHARA MINONO .
  2.
  TABAKA LA WATEULE AMBAO NI WAPAMBE WA WATAWALA WANAO PENDELEWA KWA SABABU MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA UKABILA AU URAFIKI (NEPOTISM AND FAVOURATISM) .
  3.
  TABAKA LA WAFANYAKAZI WALALAHOI AMBAO WAMEPOTEZA MATUMAINI KWA KUISHI KWENYE UMASKINI ULIOKITHIRI UKIZINGATIA CHANGAMOTO ZA ENEO LENYEWE KUTOKUWA NA FURSA ZA KIJAMII NA KIUCHUMI.

  MATABAKA NDIYO YANAYOLETA HALI YA KUTORIDHIKA KWA WENGINE HIVYO KUSABABISHA MADHARA KAMA YALIYO TOKEA TANAPA KULE SERENGETI NATIONAL PARK AMBAKO MAASKARI AMBAO NDIYO WASIMIZI WA RASILIMALI KAMA FARU HULIPWA POSHO YA TSHS.10,000 KWA SIKU HIVYO KWA MWEZI WANALIPWA TSHS.300,000 WAKATI MAOFISA WENGINE WAKISAFIRI KWENDA KUTANGAZA UTALII HULIPWA DOLA 400-600 KWA SIKU.

  HATA WALIPOLALAMIKA HAWAKUSIKILIZWA NA HIVYO KUSHUSHA MORALI YA KUFANYA KAZI,KIMSINGI HILI NDILO TATIZO KUBWA KUNAPO KUWA NA WACHACHE WANAO NUFAIKA WAKATI WENGINE HAWANUFAIKI. HIVYO TUNAOMBA WAZIRI MWENYE DHAMANA ACHUKUE HATUA MADHUBUTI KULINUSURU ENEO HILI LA URITHI WA DUNIA KWANI TAYARI AMEKABIDHIWA TAARIFA NA TUME NA MHESHIMIWA JAJI TUME YA MSTAAFU YA JAJI THOMAS MIHAYO ILIYOTUMIA ZAIDI YA Tshs.130,000,000. KUANDALIWA KAMA BUNGE LILIVYO AGIZA BAADA YA HOJA BINAFSI YA MHESHIMIWA MBUNGE WA NGORONGORO KUHUSU TUHUMA YA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA DHIDI YA BWANA PIUSI MSEKWA.

  KWA MUJIBU WA TUME YA JAJI THOMAS MIHAYO TUHUMA ZA MATUMIZI YA MADARAKA NA RASILIMALI ZIKO WAZI IGAWA TAARIFA HII BADO IMENDELEA KUWA SIRI KUBWA NDANI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII HATA BAADA YA WAZIRI KAGASHEKI KUKABIDHIWA!

  MWISHO TUNAKUOMBA MHESHIMIWA WAZIRI UIFANYIE KAZI TAARIFA YA TUME YA MHESHIMIWA JAJI MSTAFU THOMAS MIHAYO ILI KULINUSURU ENEO AZIZI LA BONDE LA NGORONGORO URITHI WA DUNIA. USHAURI KWA MHESHIMIWA RAIS ZIGATIA USHAURI WA WATAAM USITEUE WATU WA AINA YA PIUS MSEKWA AMBAO WANA MAWAZO MGANDO YA KUDHANI KWAMBA NI WATU MAALUM (V.I.P) WASIO HESHIMU MAWAZO YA WENGINE NA WANAOAMINI KWENYE TARATIBU BILA KUJALI MISINGI YA UADILIFU NA KWAMBA CHEO NI DHAMANA APEWAYO MTU NA SIYO MALI YA MHUSIKA. MUNGU IBARIKI TANZANIA IPATE VIONGOZI WAADILIFU NA WASIO WANAFIKI NA WABINAFSI. MASWALI YA MUHIMU YA KUJIULIZA KWANINI BODI CHINI YA UENYEKITI WA MHESHIMIWA P.MSEKWA ILAZIMISHE MTU MMOJA ASIMAMIE UKUSANYAJI WA MAPATO, AIDHINISHE MATUMIZI NA KURATIBU MASUALA YOTE YA FEDHA YEYE MWEYEWE?

  KWANINI BODI IRUHUSU OVER EXPENDITURE YA TSHS.692, 000,000TSHS KWA AJILI YA TOURISM EXHIBITIONS MWAKA 2011-2012?

  4. WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII ATACHUKUA HATUA STAHIKI?

  KWANINI NGORONGORO IWE NA OVER EXPENDITURE HADI KUSABABISHA BANK OVERDRAFT YA BILIONI 16,880,473,000TSHS NA MKOPO WA MILIONI 800 WAKATI MAKUSANYO YA MIAKA MITATU TANGU 2010 HADI 2012 NI ZAIDI YA BILIONI 120?

  BODI KUTOCHUKUA HATUA STAHIKI HATA BAADA YA KUJUA KWAMBA MHIFADHI BWANA BENARD MRUNYA NA MKURUGENZI WA FEDHA NA UTAWALA WALIKIUKA TARATIBU ZA KUKOPA FEDHA,INAMAANISHA KWAMBA WANAMASLAHI BINAFSI AU LA?

  JE? MISINGI YA UTAWALA BORA NA NATURAL JUSTICE INARUHUSU MTU MMOJA KUJISIMAMIA, KUJIHUKUMU NA KUJICHUNGUZA, NA KUJIIDHINISHIA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA?

  5. KWANINI MAMLAKA YA HIFADHI INANUNUA VIFAA MBALIMBALI KWA BEI ZA JUU SANA NA VISIVYO NA UBORA? SWALI HILI LINATUPELEKA KUANGALIA UFISADI MKUBWA UNAO ENDELEA KWENYE MANUNUZI YA VIFAA CHINI YA KAMATI YA MANUNUZI YA MAMLAKA HII. KUMEKUWA NA TATIZO LA UNUNUZI WA VIFAA VILIVYOTUMIKA NA VILIVYO CHINI YA KIWANGO CHA UBORA LAKINI KWA BEI KUBWA.MFANO MAJENERETA MAWILI YALINUNULIWA KWA TSHS.362, 330,800 HADI LEO KUNA UTATA KAMA NI MAPYA AU LA NA KAMA YANAKIDHI MASHARTI YA MKATABA.

  JE? MAKAMU MWENYEKITI ANAKINGA YA KUTOSHITAKIWA KWA MAKOSA YA JINAI? KAMA KUTUMIA MADARAKA VIBAYA KUJIPATIA FEDHA KUPITIA RUSHWA KUTOKA MAKAMPUNI MBALIMBALI YANAYOFANYA BIASHARA NA NGORONGORO,MFANO NYANZA ROAD WALIPEWA MKATABA WA BILIONI 6 KUTENGENEZA BARABARA KUTOKA LANGO LA LODOARE HADI GOLINI KWA MAELEKEZO YA BWANA PIUS MSEKWA.MKATABA HUU ULIPIGIWA KELELE NA WADAU KWAMBA ULIKUWA NA HARUFU ZA UFISADI LAKINI NYANZA WALILIPWA PESA ZAO ZOTE BILA KUJALI UBORA WA KAZI.

  JE? FEDHA ZA NGORONGORO NI MALI YA UMMA AU ZA BODI YA MHESHIMIWA MSEKWA? KAMA NI ZA UMMA KWANINI SERIKALI ISINGILIE MAPATO NA MATUMIZI?
   
 2. Godfrey Electronics

  Godfrey Electronics JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 13, 2012
  Messages: 587
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  uuuwiiiiiiiiiiiii.......! Nafa na presha mwenzenu
   
 3. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Madudu ya hivi yapo karibu kila sector, so sad!
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  NCAA is one of the organization that its management and "crafty staff" have enjoyed loose money and quick riches simply because of poor system ya accountability

  If the government is serious about NCAA kuna watu watanyongwa!!

  Kuanzia tu, Wamcheki Msekwa na wenzake...........
   
 5. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  ndugu yangu kwanza hongera kwa taarifa hii ni nzuri na nina hakika ni ya kweli nimeumia sana na nina uhakika muda si mrefu watawajibika
   
 6. m

  mabhuimerafulu Member

  #6
  Jun 6, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hebu jisomee hii Ze Comedy: Msekwa aliwahi kuwa chairman wa governing Council ya chuo cha Wanyamapori Mweka. Madudu tu. Baadaye akaingia Hifadhi ya Ngorongoro, boss wa Ngorongoro akiwa marehemu Emmanuel Chausi. Kwa wasiojua, Msekwa anatoka Ukerewe kijiji kiitwacho Bugombe na ndicho kijiji alichokuwa anatoka Chausi.
  Wakala sana. Kwa hiyo Msekwa huko kwenye wanyama ndiko kwake. Lkn kwa nini amedumu hivyo Ngorongoro? Mipesa mingi ndiyo huchotwa kwa ajili ya kampeni za CCM. Mpo hapo?Ipo siku watajibu.
   
 7. NAKAMO

  NAKAMO Member

  #7
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  :angry:IPO SIKU WATAJUA NINI KILIMTOA KANGA MADOA
   
 8. mojoki

  mojoki JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 1,333
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  If govt is real serious kuna watu watahamishiwa sector nyingine, Tangu lini mtu akanyongwa tanzania
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2012
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Aisee hii ni balaa si kidogo!
   
 10. N

  Nesindiso Sir JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2013
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 374
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii nayo ni historia sasa
   
 11. N

  Ninaa Member

  #11
  Mar 5, 2013
  Joined: Sep 3, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Bado hatujajua barabara ya kupanda crater(ascending road) ambayo ni kilometa 6 tu lakini inajengwa kwa mwaka mzima,itakua imegharimu sh ngapi?Malori ya kubeba vifusi si mapya lakini nenda uangalie bei waliyonunulia,utaanguka chini!Ni lini Watanzania tutachukua hatua stahiki?Kampuni ya Nyanza road ambayo ni ya Msekwa ilipewa tenda ya kutengeneza barabara kiwango cha vumbi kutoka golini(mpaka kati ya Serengeti na Ngorongoro)hadi Lodoare gate kwa zaidi ya bilioni nane(km kama 70)barabara yenyewe imedumu msimu mmoja tu.Kwa nini wasijifunze kwa wenzetu Afrika Kusini,barabara za lami ambayo ina rangi ya mazingira ya porini.Ufisadi mtupu
   
 12. nkure

  nkure Member

  #12
  Mar 5, 2013
  Joined: Feb 17, 2013
  Messages: 68
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Hayo ndo MADUDU ama uchafu uliojaa kwenye sector za serikali yetu. Watanzania wengi ni waoga na sii wazalendo kama ulivyoonyesha wewe, Kwa hili nakupongeza sana na umeonyesha jinsi gani hili jambo limekukera.
   
 13. Ngigana

  Ngigana JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2013
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,260
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  Mkuu umetoa taarifa nyeti sana jinsi mali ya waTz inavyofujwa, lakini mbona hujasema kuwa baadhi yenu ninyi watendaji mnaendesha zoezi la kuwang'oa meno tembo? Ni vema ukasema yote!
   
 14. Mtanga Tc

  Mtanga Tc JF-Expert Member

  #14
  Mar 11, 2013
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 228
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Spot on! Japo hii ni TZ inayoshabikiwa na wengi kwani wamepofushwa fahamu zao!
   
Loading...