Ufisadi katika kilimo: Kweli CCM imedhamria kuwauwa wananchi!

Ufisadi katika kilimo: Kweli CCM imedhamria kuwauwa wananchi!

tpmazembe

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
2,469
Reaction score
588
By Mwenyekiti wa PAC. Mhe Zitto Kabwe.

Leo nimeandika kuhusu Deni la Taifa kukua kwa kasi na kufikia tshs 27 trilioni mpaka Desemba 2013 kutoka tshs 10 trilioni mwaka 2005. Baadhi ya Watalaamu wanajenga hoja kuwa kukopa sio shida, bali kukopa kwa ajili ya nini. Nikakumbuka mzigo wa madeni ambao Taifa lilibeba miaka ya sabini na themanini kiasi cha Tanzania kukoswa koswa kuwa nchi ya Kwanza duniani kushindwa kuhudumia madeni yake. ‘heshima’ hiyo ilikwenda kwa nchi ya Nicaragua mwaka 1982. Mikopo ya nini? Mwishoni mwa miaka ya sabini Tanzania ilikopa dola za kimarekani milioni sitini (USD 60m) kwa ajili ya mradi wa Kiwanda cha viatu Morogoro. Lengo la kiwanda kiwanda kile ilikuwa ni kuuza viatu nchini Italia. Mwaka mmoja baada ya kiwanda kuzinduliwa kilikuwa na uwezo wa kuzalisha kwa ufanisi wa asilimia 4 tu ya uwezo wake na hakikuweza kuuza hata jozi moja ya kiatu nje ya nchi. Miaka ya tisini kiwanda kile kiliuzwa katika mpango wa ubinafsishaji na hivi sasa kimegeuzwa kuwa ghala. Hata hivyo Deni hili lilipwa na kila Mtanzania kupitia kodi.
Kesho Jumanne tarehe 28 Januari, 2014 Kamati ya Bunge ninayoongoza ya Hesabu za Serikali (PAC) inapokea taarifa ya ukaguzi maalumu uliofanywa kuhusu Mfumo na Mchakato wa kusambaza pembejeo za ruzuku kwa wakulima. Ukaguzi huu umefanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali (CAG). Nimeipitia Taarifa hii na kukumbuka habari ya ‘Morogoro Shoe Factory’.
Bajeti ya pembejeo za ruzuku ya mwaka 2011/12 ilikuwa tshs 122.4 bilioni, kati ya hizo tshs 88.9 bilioni ni mkopo kutoka Benki ya Dunia. Taarifa ya CAG inaonyesha uvundo wa ufisadi katika mfumo mzima wa pembejeo za ruzuku. Katika kijiji cha Lunyala wilayani Nkasi mkoa wa Rukwa asilimia 70 ya wananchi waliorodheshwa kupata mbolea walikuwa bandia, hata hao waliopata mbolea walidai mbolea ilikuwa haina ubora stahili na matokeo yake uzalishaji wa mazao ulikuwa mdogo. Hata hivyo wasambaji wa mbolea walilipwa fedha zao zote. Afisa mmoja mwandamizi wa Benki ya Dunia alipata nukuliwa kusema kuwa asilimia 60 ya Bajeti ya pembejeo za ruzuku iliporwa na wajanja wachache.
Deni hili nalo litalipwa na Watanzania wote japo waliofadika ni wezi wachache. Kinachosikitisha ni kwamba masuala haya yanayohusu wananchi hayapati msukumo kwenye mijadala ya kitaifa. Tusipobadilika tutajikuta tuna madeni mpaka kwenye kope za macho yetu.
“…mikopo haisaidii, hata tukiitumia kujenga shule au hospitali au viwanda lazima ilipwe. Mlipaji ni mkulima wa vijijini…” Azimio la Arusha, 1967.
 
Huu mpango wa ruzuku kwenye pembejeo haujawahi kuwa na ufanisi hata maramoja. Huu ni mradi mahususi kwa ma-DC na viongozi wakubwa wengi serikalini. Haohao ndiyo ma-agent wakusafirisha/kusambaza, pembejeo zinazowafikia wakulima ni chache mno na mara nyingi nje ya wakati na ikiwa imepunguzwa ujazo, imedhibitika nyingi zinavushwa nchi za jirani hasahasa Zambia na Malawi kwa biashara. Ni madudu mengi na PCCB wanayajua haya ila wanakaa kimya kuwalinda wakuu wao. Inatia uchungu sana.
 
Wabunge wanaowakilisha wakulima wasihi serikali ikope lakini deni walipe waliofaidika. Yale ya deni watumie wachache ila kulipa hilo deni tulipe wote haingii akilini. Wakulima tuambiwe ni kwa jinsi gani tutagoma kulipa. Chadema nafikiri wana jibu.
 
Hakuna mtu asiyejua hilo. kwenye pembejeo kuna maviongozi wengi wa ccm na ndipo wanapofanyia ufisadi na watu wa takukuru na usalama wanajua hili ila wanafumbiwa macho. Kuna uzi hapa wa mwaka uliokowa ukionyesha ufisadi uliofanyw na mbunge aesh wa sumbawanga kwenye mikoa ya rukwa na katavi kupitia kampuni ya noarthmead kwa kushirikiana na ma rc akina rutengwe na manyanya pia nasikia msimu huu wa kilimo ameanza tena kwa kushirikiana pia na vijana wa uvccm. ngoja niwasiliane na jamaa zangu waliopo rukwa na katavi ili wanipe habri nini kinachoendelea na nitauweka wazi ufisadi wa ccm kwenye pembejeo kwa lengo la kuweka pesa kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa na serikali kuu.
 
ufisadi hauwezi kukoma hadi hapo chama cha mizigo kitakapotoka ikulu! watz tujitambue na tuchukue hatua uchaguzi mkuu na huu wa SM!
 
Back
Top Bottom