Ufisadi hauwezi kuisha Tanzania hadi sheria ya kunyonga mafisadi iwekwe

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,527
habari..

Najua wengi tunajua vita ya ufisadi unavyopigiwa kelele miaka kadhaa sasa..

Hapa nimesikia redioni kuna watumishi wa halmashauri geita wamefisadi bilion 2 juzi tu...

Nikakumbuka hii vita ni ngumu sana..

Kwa wanaohusika wakitaka ufisadi uishe kweli tanzania tuwe kama china au nchi zingine zilizoendelea..

Vita ya ufisadi ipiganwe kwa sheria ngumu hasa hasa ya kunyonga mafisadi, au kupigwa risasi hadharani...

Mtu kama joka lenye makengeza leo anakula kuku.. halafu unazuia watumishi wasifanye ufisadi..

Angekuwa amenyongwa hadharani na wenzake hapo wengine wangeogopa
 
Kuamini Ufisadi unaweza kuisha chini ya CCM ni kuota ndoto.
 
habari..

najua wengi tunajua vita ya ufisadi unavyopigiwa kelele miaka kadhaa sasa..

hapa nimesikia redioni kuba watumishi wa halmashauri geita wamefisadi bilion 2 juzi tu...

nikakumbuka hii vita ni ngumu sana..

kwa wanaohusika wakitaka ufisadi uishe kweli tanzania tuwe kama china au nchi zingine zilizoendelea..

vita ya ufisadi ipiganwe kwa sheria ngumu hasa hasa ya kunyonga mafisadi, au kupigwa risasi hadharani...

mtu kama joka lenye makengeza leo anakula kuku.. halafu unazuia watumishi wasifanye ufisadi..

angekuwa amenyongwa hadharani na wenzake hapo wengine wangeogopa
Kesho fisadi atakuwa anayekuhusu! Weka akiba ya ushabiki!
 
Kesho fisadi atakuwa anayekuhusu! Weka akiba ya ushabiki!

hata nikiwa mimi.. ninyongwe tu.. ufisadi unaua watanzania wengi maskini kwa kukosa huduma bora.. kama dawa... so why nisinyongwe?

hujaona raisi kamuua kaka yake kisa fisadi duniani huko
 
Ufisadi umo ndani ya mfumo wa uongozi wa nchi hii. Mikataba yote ya kifisadi imeridhiwa na viongozi wakuu wa nchi hii. Ndio maana hilo joka la makengeza huwezi kulifanya kitu.

Ufisadi ni wimbo wa kisiasa .
 
hata nikiwa mimi.. ninyongwe tu.. ufisadi unaua watanzania wengi maskini kwa kukosa huduma bora.. kama dawa... so why nisinyongwe?

hujaona raisi kamuua kaka yake kisa fisadi duniani huko
unasema kwa vile una mkate mdomoni, ukikutoka utaona nini naongelea!
 
Tumuunge mkono Magufuli katika Vita dhidi ya ufisadi aliyoianzisha.upigaji na maovu yapo kila ngazi hata Huku chini tuko na jukumu la kupinga rushwa maana ndo chanzo Cha ufisadi
 
unasema kwa vile una mkate mdomoni, ukikutoka utaona nini naongelea!

kwa hiyo wizi ni sifa?? vibaka wanaochomwa moto mitaani na majambazi wanaouwawa.. je wanaonewa.. fisadi ana madhara makubwa kuliko kibaka wa kuku mtaani.. maana yeye anaua wengi kwa kuwaibia hela za kununua madawa... wamama wajawazito wanakufa wakijifungua kisa fisadi
 
Nani wa kumfunga paka kengele. Nyoka mwenye makengeza ndiye wa kutenegeza sheria za kumnyonga, si bora kujinyonga mwenyewe kama atakuwa amechoka kutambaa!
 
kunyonga tu si solution maana China kila siku watu wanakula vitanzi ila bado ufisadi upo,
 
Tuanze kwanza na ile mahakama.uko kwingine ni mbali sana kwasababu bado hatuna mifumo sahihi yakutenda haki.
 
Na tunavyopenda kukomoana, watauliwa likuki wasio na chembe ya ufisadi bali wa kabambikiwa na mafisadi watabaki!
 
Katiba tu imewashinda kwa kuogopa kukosa ulaji, leo uwaambie wajinyonge? Unaishi nchi gani?
 
Back
Top Bottom