Tanzania tutunge sheria ya kunyonga hadharani wataobainika kufanya makosa ya ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Nchi hii, ili ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma upungue kwa kiasi kikubwa(najua hauwezi kwisha), yoyote ataepatikana na hatia ya ubadhirifu, wizi na ufisadi wa mali ya umma, anyongwe hadharani mpaka kufa.

Tukiwaonea huruma, tunawaacha wanafia jela, ila sheria itamke wazi adhabu yao ni kunyongwa mpaka kufa. Tusipofanya hivyo, ufisadi nchi hii utakuwa ni donda ndugu na itafika hatua mafisadi watatudharau kwani tunalalamika na hakuna hatua za maana zinazochukuliwa dhidi yao.

Na sheria ingekuwa narudiia nyuma, tungeanza kunyonga wale wote waliohusika na kuifanya gesi yetu kuwa mali ya mabeberu kama alivyotuambia Mwendazake kuwa ile gesi kule kusini si yetu tena, bali ni mali ya mabeberu.

Ukiacha hii habari ya madini kuibiwa(kama ni ya kweli), kuna habari nyingine nimepenyezewa na mdau mmoja hapa jukwaani inayohusu mali asili zetu na watendaji wake(nimeisoma)ambayo kama ni ya kweli, basi nchi hii itakuja kutengeneza mabilionea wanaotokana na wizi wa mali za umma huku nchi na watu wake wakiendelea kubaki masikini.

It is so disgusting!

Taarifa hiyo siwezi kuiweka hapa na kwakuwa ignorance is bliss, nachoweza ni kuwapa pole tu wadanganyika wenzangu.
 
Tatizo wanalindana, sheria inaweza kuwepo lakini isitekelezwe, watakaa jela wakishasahaulika ghafla wataonekana mitaani, muhimu CCM iondoke kwanza tuanze upya.
 
Cha kwanza ni kuiondoa CCM madarakani ndio haya mengine yaweze kutekelezeka. .
 
Magufuli alivyokuwa akideal na mafisadi perpendicularly bila kupepesa macho mlifanyaje? Si mlianza kumwita dikteta uchwara? Eti hafati utawala wa sheria?

Ni hivi, no one takes seriously kelele za ufisadi kutoka kwa watu wale wale waliokuwa wakimponda Magufuli. You do not mean it nyie mnachoangalia ni kete tu za siasa.

Tunamsubiri kwa hamu sana Magufuli mwingine!
 
Ujue rangi ya njano ina uwezo wa kushika madoa kwa haraka sana? Sijui kama Kibatala et al, wanaweza mambo ya uhaini na ugaidi kwa pamoja. Ukifika nyumbani, angalia machoni wale wanaokutegemea au unaowapenda kabla hujaenda coco beach.
 
Kwa mahakama hizi, wewe utakuwa wa kwanza kunyongwa. Shauri yako. Wewe endelea kuomba kutungwa sheria zinazobeba adhabu kali katika nchi ambako mahakama haziko huru. Unless umeanza kuziamini Mahakama sasa.
 
Jiwe mwizi mkubwa aliyeiba 1.5 trilion angenyongwa na nani kama sheria inamlinda mpaka umri kiyama?
Mwizi wa mali ya umma ni mtumishi wa umma ambaye naye kaibiwa na serikali in terms of malipo. Kwahiyo watumishi wanajiongeza ili waweze kusurvive wasife
 
Mm siipendi ccm hila kuua mtu kisa pesa ni idiotism thoughts. Mawazo yakipumbavu ambayo aliyafanya jpm
 
Magufuli alivyokuwa akideal na mafisadi perpendicularly bila kupepesa macho mlifanyaje? Si mlianza kumwita dikteta uchwara? Eti hafati utawala wa sheria?

Ni hivi, no one takes seriously kelele za ufisadi kutoka kwa watu wale wale waliokuwa wakimponda Magufuli. You do not mean it nyie mnachoangalia ni kete tu za siasa.

Tunamsubiri kwa hamu sana Magufuli mwingine!
Ungeisoma hiyo taarifa, hata huyo Magu nae wala usingemtaja hapa.
 
Kwa mahakama hizi, wewe utakuwa wa kwanza kunyongwa. Shauri yako. Wewe endelea kuomba kutungwa sheria zinazobeba adhabu kali katika nchi ambako mahakama haziko huru. Unless umeanza kuziamini Mahakama sasa.
mtoa mada , haelewi anomba watu wanyongwe hadharani kisa wameiba hela
 
Matukio ya ufisadi wa mali za umma umekithiri sana nchi karibia miradi mingi na kwenye mashiraka kibao wizi umejaa , hapo tuliyoyasikia na kuona mengi haipiti miezi unasikia tu sehemu kumepigwa je yaliyofichwa na yanayofichwa ni mangapi ? kwakweli tunapaswa kujitambua .
 
Ungeisoma hiyo taarifa, hata huyo Magu nae wala usingemtaja hapa.
Utashindwaje kumtaja Magu kwenye vita kuhusu ufisadi hapa Tanzania?

Magufuli wala hata asingekuja kuwa rais kama isingekuwa sintofahamu ndani ya chama chake ccm kuhusu nani ataweza kupambana na wapinzani na akashinda kwa muktadha wa hali ilivyokuwa ya ufisadi nchini kuelekea 2015.

Jamii iliwategemea nyie wapinzani mngemuunga mkono Magufuli kwenye vita kuhusu ufisadi -- wa kimfumo na hata ule wa mtu mmoja mmoja -- ila mlichokifanya mnakijua wenyewe.
 
Nchi hii, ili ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma upungue kwa kiasi kikubwa(najua hauwezi kwisha), yoyote ataepatikana na hatia ya ubadhirifu, wizi na ufisadi wa mali ya umma, anyongwe hadharani mpaka kufa.

Tukiwaonea huruma, tunawaacha wanafia jela, ila sheria itamke wazi adhabu yao ni kunyongwa mpaka kufa. Tusipofanya hivyo, ufisadi nchi hii utakuwa ni donda ndugu na itafika hatua mafisadi watatudharau kwani tunalalamika na hakuna hatua za maana zinazochukuliwa dhidi yao.

Na sheria ingekuwa narudiia nyuma, tungeanza kunyonga wale wote waliohusika na kuifanya gesi yetu kuwa mali ya mabeberu kama alivyotuambia Mwendazake kuwa ile gesi kule kusini si yetu tena, bali ni mali ya mabeberu.

Ukiacha hii habari ya madini kuibiwa(kama ni ya kweli), kuna habari nyingine nimepenyezewa na mdau mmoja hapa jukwaani inayohusu mali asili zetu na watendaji wake(nimeisoma)ambayo kama ni ya kweli, basi nchi hii itakuja kutengeneza mabilionea wanaotokana na wizi wa mali za umma huku nchi na watu wake wakiendelea kubaki masikini.

It is so disgusting!

Taarifa hiyo siwezi kuiweka hapa na kwakuwa ignorance is bliss, nachoweza ni kuwapa pole tu wadanganyika wenzangu.
Watathubutu kutunga hiyo sheria sasa🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom