Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,706
- 149,945
Baada ya kusoma taarifa inayohusu tuhuma za wajumbe wa kamati za Bunge kujihusishwa na rushwa katika gazeti la Mtanzania, nashawishika kusema rushwa,ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka kwa waliopewa dhamana ni mambo yasiyoweza kwisha bila kuwa na sheria kali kama kutoa adhabu ya kifo kwa watakaokutwa na hatia ya kutenda makosa hayo.
Tumefika hapa kwasababu hatuko serious katika mambo haya kiasi kwamba inafikia hatua hata wale waliokuwa vinara wa kupinga wizi na ufisadi nao wameanza kuwa watuhumiwa kwasababu wanaona hata wakipiga kelele haisadi na ni bora nao wakaanza kushiriki katika dhambi hii.
Kwa mfano,wabunge walipiga sana kelele kutaka waliotajwa katika kashifa ya Escrow wachukuliwe hatua lakini leo baadhi yao ndio mawaziri kwenye serikali inayojinadi kutuletea mahakama ya mafisadi!
Kama haitoshi,mtuhumiwa wa kashifa moja kuwa leo hii nae ni mwenyekiti wa Bunge!Mbaya zaidi ni kuona wananchi wenyewe wanachagua watuhumiwa wa ufisadi kuwa wabunge, n.k
Kama haitoshi, wanaoutuhumiwa (wanaochafuliwa) kwa rushwa kutoka hadharani na kusema mwenye ushahidi aende mahakamani huku viongozi waandamizi wa serikali wanaomtuhumu kwa rushwa "wakiufyata"!
Cha kukatisha tamaa zaidi ni kuona mafisadi wakibadilishiwa adhabu kutoka kifungo cha ndani na kupewa kifungu cha nje na wakati huo huo tukiendelea na mchakato wa kuunda Mahakama ya Mafisadi!Sijui tumelogwa!
Athari ya haya yote ni hata wale wachache wenye moyo wa uadilifu nao kubadilika na kuwa wezi maana wanaona wenzao wanaiba wanatajirika na wanaendelea kupeta mtaani huku wanaopinga wizi na ufisadi wakifa masikini.
Niwambie watanzania wenzangu kuwa, tulipofikia kwa sasa tunahitaji kuwa na sheria ya kunyonga mafisadi tena sheria isiyohitaji "idhini ya raisi" kutekeleza adhabu hiyo bila ya hivyo tunatwanga maji kwenye kinu.
Ukiona mtu kama Kangi leo hii anatajwa kwenye kashifa kama hizi,mwenzenu najenga hisia huenda ameona kupiga kelele dhidi ya ufisadi ni biashira isiyolipa na ni bora kuwaza vinginevyo.