SERIKALI INACHUNGUZA KITU GANI ZAIDI KWA AFYA YA DK MWAKYEMBE NJE YA RIPOTI YA MATOKEO YA KITAALAM ILIOTOLEWA NA JOPO LA MADAKTARI BINGWA WANASANSI WA HOSPITALI MAARUFU DUNIANI LA APOLLO NCHINI INDIA???????
I. SERIKALI ICHUNGUZE SWALA LA 'NANI AU AKINA NANI WANAAHUSIKA NA SUMU KWA MWAKYEMBE' NA WALA SI KUCHUNGUZA 'KAMA ALILISHWA SUMU AU LA'
Serikali iache mara moja kupoteza kodi za wananchi eti kuchunguza KAMA DR MWAKYEMBE ALIPEWA SUMU AU LA, kwa kuwa yeyote anayeendelea kujikita katika mstari huu ajue kwamba kwanza anatupotezea muda, napoteza rasilmali za taifa kwa malengo butu yasiokua na tija si kwa Umma wa Tanzania wala kwa Dk Mwakyembe mwenyewe kwa kuwa majibu ya hilo swali tayari tunayo kitaalam zaidi toka Apollo Hospital wa kule nchini India.
Kwa mantiki hiyo, hoja yangu hapa ni kwamba uchunguzi wa serikali ni sharti sasa ulenge kutafuta majibu ya maswali zaidi juu ya sakata hili la 'Gogoro la Afya la KUCHONGA' ambayo mpaka sasa hayapata kujibiwa. Kwa msingi huu, hivo ijulikane wazi kwa serikaali hii ya Kikwete kwambaa sisi wananchi ambao ndio wenye dhamana wanayotumikia wote hapo serikalini tunapenda kusikia kwamba kodi zetu zinatumika kwa njia ya kuleta majibu mapya yenye tija kwetu na familia ya Dk Mwakyembe na wala si kufanya kazi za kurudufu shughuli ambazo taayari yako wazi mitaani.
Kwa matarajio yetu, swala jipya na zito zaidi kuhitaji majibu mapya ni 'JENI NANI AU AKINA NANI HAO WANAOHUSIKA NA ULISHWAJI SUMU KWA DK MWAKWEMBE NA WANAFANYA HIVO KWA NJIA ZIPI NA MALENGO GANI NA KITU GANI KIFUATE', full stop!!! Hatutaki mizunguko zaidi, miduara zaidi na kule kutupiana kwingi mpira kati ya maafisa waandamizi na vyombo vyao vilivyokwishaonyesha ubutu wa kustaajabisha toka huko nyuma.
Hivyo, mpaka hapa, ni kwa kuendeleza matarajio hayo hayo ya wananchi juu ya sakata hili ambapo tungependa kuaagiza Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshugulika na maswala ya Afya na Usalama wa Raia, ifanye hima kuunda kamati murua itakayo kuna chombo huru, chenye weledi zaidi na hadidu za rejea za wazi kwenda kuchunguza swala zito zaidi kwamba 'NI NANI AU AKINA NANI HAO WANAOHUSIKA NA ULISHWAJI SUMU KWA DK MWAKWEMBE NA WANAFANYA HIVO KWA NJIA ZIPI NA MALENGO GANI NA KITU GANI KIFUATE', full stop!!!
Haya yote yanatokana na ukweli kwamba taarifa zozote juu ya afya wa kiongozi yeyote wa umma ni mali na na haki ya walipakodi wa nchi hii kuujua tena ki-undani zaidi.
Msingi wa hoja yangu hii ni kwamba mtu anapokua kiongozi anapewa dhamana na umma na pindi inapotokea kwamba ameugua tena ni umma hiyo hiyo ndiyo hugharamia tiba yake mwanzo mpaka mwisho. Hadi hapo si haki kwa mtu yeyote kuficha taarifa zozote mbali na umma kwa kuwa ndiye mwenye dhamana yake pamoja na ufadhiliya kiongozi yeyote
Kama haitoshi, nasema swala la serikali kupanga kuendelea kuchunguza sakata juu ya afya ya Dk Mwakyembe KAMA NI SUMU AU SI SUMU hadi hivi sasa ni AN IRRELEVANT ENDEAVOUR isiomsadia mtu yeyote yule ndani y nchi hii. Hivyo endapo kuna mtu au chombo kuna chombo (pengine CCM) kinataka kujiridhisha zaidi juu ya hilo bali kiendeshe uchunguzi binafsi kwa gharama binafsi na matokeo hayo yaje yatumike kwa kukidhi matakwa yao binasi huko mbali na macho yetu.
Katika eneo hili la pili nako hoja yangu nzito sana ni kwamba hadi sasa ni wazi kwamba jopo la Madaktari Bingwa na Wana-Sayansi wa hospitali Maarufu sana duniani, Apollo Hospital kule nchini India, wao walitumia MUDA MFUPI UNAOJULIKANA kuchunguza vipimo toka kwa Dokta Mwakyembe na KUTUWEKEA JIBU HADHARANI.
Katika msururu mzima wamambo ya uchunguzi wa kitibabu na kisayansi huko Apollo Hospital, katika ulimwengu wa sheria, tunatambua wazi kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kwa niaba ya Umma wa Tanzania ambao ndio wenye dhamana yote KIKATIBA na wenye kugharamia kila kitu kifedha kupitia kodi zetu) inajitokeza kuwa ni mteja na kwamba Jopo lile la Wataalam waliobobea katika Sayansi ya Tiba pale Apollo Hospital wao pamoja na vyombo vyao vya kisasa ambavyo vilipata kukiridhisha serikali yetu, wao ni waajiriwa katika mtiririko mzima huu.
Hivyo mwisho wa siku wakatoa RIPOTI YA KIUFUNDI WA SAYANSI YA TIBA ILIOTUKUKA ZAIDI DUNIANI PALLE APOLLO HOSPITAL na kuikabidhi kwa serikali hii ya JMT kwa niaba yetu ili sisi kama wateja tujiridhishe nini kinachomsibu mgonjwa wetu (Dk Mwakyembe) ambaye Umma wa Tanzania tunacho cha kupoteza kwa kiasi kikubwa endapo atadhurika zaidi na hata pindi inapotokea kibahati mbaya akapoteza maisha.
Sasa kunapotokea mtu au watu wanajipenyeza katikati ili watu tusipate kujiridhisha na ripoti hiyo ambayo serikali iliipewa tayaari nadhani hili huenda tukaidai vizuri zaidi kupitia mahakama ili mwajiriwa wetu huyo wa kumtibu Dk Mwakyembe aje akaitoe yote yote bila hata ya nukta kufutwa kwenye ripoti hiyo; and that is a fact to come sooner than later anyway!!
Naam, kitendo hiki kilitokea mara baada ya Madaktari Bingwa na Wataala wote wa Maswala ya Ngozi nchi KUKIRI KWA LUGHA YA MATENDO yao, pale hospitali yetu ya rufaa Muhimbili, kwamba kuhusu sakata la ki-afya ya Dokta Mwakyembe wao ama imewazidi utaalam au kule kukosekana kwa zana za kisasa zaidi ya sayansi ya tiba hapa nchini hivyo serikali ikalazimika kumpeka huyu kiongozi wetu huyo kwa tiba zaidi huko nje ya nchi.
Kwa kuzingatia ukweli kwamba kuna taasisi bora za tiba zaidi ya milioni moja kote duniani, kitendo cha serikali ya JMT kuamua kumpeleka mtumishi wetu Apollo Hospital na wala si kwingineko maana yaake ni kwamba kuna umakini wa hali ya juu ulitumika kufikia chaguo hilo.
Ndio, tungependa kuendelea kuamini hadi sasa kwamba serikali nayo iliamini sana chombo hicho cha hapo nchini India kwa utaalamu wake wa sayansi ya tiba, mazingira na vyombo vyake vya kisasa zaidi ya hali hlisi tulionayo kokote kule hapa nchini hivyo hata kunapotokea wao kutukabidhi RIPOTI YAO YA KIUCHUNGUZI JUU YA AFYA YA MGONJWA WETU DK MWAKYEMBE, ni imani ile ile inatarajiwa kuewndelea hadi kutafuna yale yaliomo mle ndani ya faili ile ya mgonjwa wetu.
Sasa kama hali hali ni kwa serikali ya JMT kulazimika kukidhi matarajio tajwa hpo juu kuhusiana na ripoti ya Dk Mwakyembe toka kwa wataalam wa saynsi ya tiba waliosifika kote duniani sasa hili la kuibuka mtu kama vile katoka usingizini au kwenye sayari nyingine, na ghafla tu eti anaanza kutunatangaia kundi lingine kufanya kazi ile ile ambayo tayari wao kama serikali walishawaajiri wataalam wa Apollo Hospital kufanya na kutoa hitimisho ya yote, ni nani anajaribu kuchezea akili ya nani hapa na kwa kuteketeza rasimali adimu ya taifa kwa sababu gani hadi hapo????????
Wananchi kote nchini sasa ni wakati mwafaka kusema NO kwa hilo kundi la pili la WANA-SAYANSI UCHWARA WA WAZIRI VUAI NAHODHA eti kwenda kuendesha uchunguzi juu ya uchunguzi wakati maswali zaidi yanayolilia majibu mapya yanaendelea kubaki bila kushughulikiwa.
Kero kubwa zaidi tena juu ya WANASANSI WA VUAI NAHODHA ni kwamba wao tunaambiwa kwamba WATATUMIA MUDA USIOJULIKANA kurudia kazi hiyo hiyo. Hivi tunafanyia ngonjera uhai wa mtu mzito kama Waziri wa nchi na Mpiganaji kwa fida ya wanyonge wa nchi hii kiasi hiki?
II. UCHURO WA NGONJERA ZA MAAFISA WAANDAMIZI SERIKALINI KUHUSU RIPOTI YA GOGORO LA AFYA YA DK MWAKYEMBE
KUHUSU sakata la mgogoro wa afya na 'Ngonjera na Midura Mirefu' inayoendelezwa na Maafisa Waandamizi ndani ya serikali ya Kikwete juu swala nyeti linalogusia uhaai wa Naibu Waziri wa Miundombinu, Mbunge wa Kyela na Mwanaharakati dhidi ya ufisadi nchini, Dk Harrison Mwakyembe, wananchi sasa tunasema HATUTAKI MBICHI HIZI tena!!
Katu haingii akilini hata kidogo DCI ambaye ndiye Mchunguzi Mtaalam Mkuu nchini Tanzania, awe tu amekurupuka na ki-jiripoti mbele yake tena kwa kuzingtia maelekezo ya weledi wa kazi yake inavyosema, halafu leo hii mtu aibuke na kusema bila aibu eti 'mimi kama Waziri Mwenye dhamani sikujua'.
Mchezo huu maafisa waandamizi wa serikali hii ya Kikwete wa kutupiana mpira kushoto kulia juu ya ripoti ya kitaalam toka Hospitli ya Apollo nchini India hivi sasa unakera kuliko kawaida. Mambo yalianza na Blandina Nyoni wa Wizara ya Afya kushonea faili yenye majibu ya afya ya Dr Mwakyembe kwenye gauni lake ikawa ni vigumu kupakitaka.
Waziri Mwenye dhamana ya Afya, Dk Mponda naye akageuka bubu ghaafla juu ya ripoti hiyo, na wananchi tuliposhinikiza uchunguzi wa NANI ALIYEFADHILI Dk Mwakyembe kutiliwa sumu ili tujue ukweli wa mmbo, hapo ndipo akaibuka Mtetezi wa kujitolea kwa MAFISADI kwa jina la DCI Manumba aliyeendesha uchunguzi ndani ya wiki moja na kuweka mambo hadharani kwa jinsi upeo wake unavyomwelekeza - jibu likawa HAKUNA SUMU HAPA.
Sasa leo hii kaibuka afisa mwingine serikalini kwa jina la Vuaai Nahodha ambaye mpaka hivi majuzi wengi tumekua tukimuona tu kama Waziri sawa tu na picha ukatani (kwa kipindi chake ndio kumetokea mauaji mengi zaidi ya raia mikononi mwao dola wa nchi hii kuwahi kutokea katika historia ya nchi hii), nae sasa ana-bullshit kila jitihada zilizofanywa na kijana wake Manumba na kuanza kutuaminisha juu ya uchunguzi mwingine juu ya uchunguzi ambao hata wajumbe wake hatuwajui, hadidu za rejea kwao hatuzijui, taaluma zao na uzoefu hakuna anayejua, muda gani na upana wa uchunguzi wao ni swala la kufikirika tu hewani.
Kwa kadiri tujuavyo sisi huku mitaani, DCI Manumba au Saed Mwema anapofanya kazi yoyote ile ni kwamba anayefanya kazi hiyo kimsingi ni Waziri wa mambo ya Ndani ambaye ni Vuai Nahodha. Vile vile, nae huyu waziri naye u waziri mwingine yeyote yule naye anapofanya kazi yoyote kwa jina la serikali yetu hii by extension ni kwamba mwenye kupokea pongezi na au lawama ni Rais wa nchi ambaye ndiye hasa wanayemsaidia kazi zake hizi.
Sasa kwa mtaji wa mizunguko hii yote, kupoteza kote muda zaidi juu ya swala hili sasa tunasema kweli mbichi hizi htuzitaki teeena!!
Kimsingi songombingo hizi zoote zilianzia pale mara baada ya kurejea nchini Dr Mwakyembe kutoka matibabuni nchini India, wananchi tulimbana mbavu kisawasawa AKATUAMBIE KULIKONI juu ya afya yake na kwamba wataalam huko wameona nini?
Kutokana na utaalam wake wa mambo ya sheria na pia maelekezo tu ya Malaika wanaomlinda kwa uweza wa Mwenyezi Mungu, Dk MwakyembeHapo nyuma kidogo
Hivi kweli enyi maafisa waandamizi wa serikali hii inayofanya kazi kwa niaba ya maelekezo, udhibiti na faida ya MAFISADI waliokubuhu nchini, leo hii mnadiriki kuchezea kamari kweli swala linalogusia uhai wa KIPENZI CHA WANYONGE wan nchi hii kiasi hiki!! Hivi kweli mnajua matokeo ya Ngonjera kama haya ya kutupiana mpira kwetu sisi wananchi huku mtaani kitu gani huenda kikafuatia kweli???????????
III. HITIMISHO JUU YA NGONJERA ZA SERIKALI KWA UHAI WA DR MWAKYEMBE
Wananchi kote nchini sasa ni wakati mwafaka kusema NO kwa hilo kundi la pili la WANA-SAYANSI UCHWARA WA WAZIRI VUAI NAHODHA eti kwenda kuendesha uchunguzi juu ya uchunguzi wakati maswali zaidi yanayolilia majibu mapya yanaendelea kubaki bila kushughulikiwa.