Ufanye nini baada ya kupoteza kazi?

Ufanye nini baada ya kupoteza kazi?

Ingia mtaa pambana anzisha kitu cha kukuingizia kipato kilichoko ndani ya uwezo wako halafu ndio uanze kutafuta kazi utakuja kunishukuru baadae. Nilikaa benchi mwaka moja nikapambana nikaanzisha kitu mpaka leo nakula faida yake hiyo ilikuwa miaka 9 iliyopita. saa zingine ni fursa ya kujijenga tunapewa.
 
namaanisha professional. kama uliajiliwa kwa professional maalum ambayo ipo nje ya kidato cha 6, 4, la 7 au kibarua tu...sheria ya sasa ya nssf kwa professional awapewi mafao yao yote😭😭😭

wewe uliajiliwa kwenye kundi lipi...?

​
Niliajiriwa kwa professional bro
 
Kama una mke ujue ni vita:

- Reaction ya mke itategemea sana kwa na sababu ya wewe kusimamisha, kama ni uzembe tegemea shida.

- Hata kama mke ana ajira, usikae tu ukafikiri atakusaidia kifedha, ndugu yangu, hilo sahau.

- Weka saikolojia ya mwanamke sawa, usilie lie, pambana jitahidi utimizie vitu vidogo vidogo.

- Usishinde Nyumbani tu hapo na Dada wa kazi, toka mda ule ule unatokaga, mke asikuache na kukukuta hapo.

- Lazima mke abadilike, na hana kosa wala, usitegemee kupewa tamu kama awali, atakuwa na mawazo na anaweza asiwe na hisia kabisa.

- Usiwe na gubu na kelele kwa mke za kulazimisha kuheshimiwa, nakueleza kama Kaka yako, **** mahusiano kati ya kutimiza wajibu wako kama Baba kifedha na kuheshimika.

- Maombi ni muhimu sana, ila achana na manabii wa hovyo nenda ibada za kueleweka, na kama wewe muislam watakuja kukushauri.
Hapa kaka nashukuru sana kwa muongozo itanijenga sana hii na wakat ndo hakuna kusubir ,ila kiukwel mi msaada wa mwanamke wangu kifedha sitegemei kbsa wanasema hela ya mwanamke ya kwake
 
Ingia mtaa pambana anzisha kitu cha kukuingizia kipato kilichoko ndani ya uwezo wako halafu ndio uanze kutafuta kazi utakuja kunishukuru baadae. Nilikaa benchi mwaka moja nikapambana nikaanzisha kitu mpaka leo nakula faida yake hiyo ilikuwa miaka 9 iliyopita. saa zingine ni fursa ya kujijenga tunapewa.
Msaada mkubwa sana huu mkuu, naufanyia kazi nashukuru sana🙏
 
Back
Top Bottom