Habari wana JF. Azolla ni mmea(magugu) ambao huelea kwenye maji, mmea huu una kiwango kizuri cha protini 25 -30% na huota sana kwenye mashamba ya mpunga na madimbwi.Kutokana na tafiti mbalimbali mmea huu umeonekana kuwa na matumizi mengi katika sekta tofauti tofauti kama kwenye viwanda (Hasa katika nchi zilizoendelea), kilimo na ufugaji.
Katika nchi zetu Azolla hutumika sana kama chakula cha mifugo( Mfano Ng'ombe, kuku na samaki) tafiti pia zimethibitisha kuwa chakula hiki husaidia mifugo kukuwa vizuri na kutoa products kama ( maziwa, mayai na nyama) zenye ubora wa hali ya juu. Pia Azolla ni chakula kizuri sana kwa samaki kwa sababu ni chakula pekee cha asili kinachoelea hivo husiadia kupunguza gharama za kusafisha mabwawa kila baada ya muda fulani kutokana na kulisha samaki vyakula vinavyozama majini na kutuama.
Kilimo cha Azolla ni rahisi na kina gharama ndogo. Ili uweze kulima Azolla unahitaji kuwa na mbegu( Zinapatikana kwenye madimbwi), mbolea(Za asili au Kemikali), udongo, maji, plastic sheet( kwa ajili ya kutunza maji) na eneo. Kwa kuanzia Azolla inaweza limwa kwa kuchimba chini bwawa dogo lenye urefu wa mita 3 kwa 2 na kina cha futi moja(cm 30).
Azolla hukuwa ndani ya siku kumi na tano tu na baada ya hapo utakuwa unavuna kila baada ya siku mbili kwa mwaka mzima.Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za chakula kama pumba kwa mifugo.
Nawasilisha;
Source: Yashrag Agro Tech and Knowledge Tv.